IMG_20190211_154721_209.JPG
 
Hata Huddersfield City wasingekubali kupigwa hivi
Mimi bado nahisi wachezaji wanamchokoza Sari ili aongee kiitaliano tena kama ile ya Bonamouth
Jana aliulizwa kuhusu mentality na motivation akasema hapana, kwa hiyo sasa Chelsea haina tatizo la mentality wala motivation, sijui shida nini zaidi
Chelsea amepigwa sita kwa kujitakia mkuu, baada ya zile nne ilibidi warudi na mkakati wa kuzuia na kushambulia kwa kushtukiza. Khee nikashangaa eti wanataka nao kufunguka na kutaka kumtunishia misuli mtu mwenye Fernandinho huku yeye akiwa na Jorginho.
 
timu gani hili yaani mechi mbili goli kumi, ni nyingi sana aisee goli kumi yaani 10, kumi, 10 aaaah jamaniii 10!
ngoja nimuulize sheikh Ramadan Sobhi hii kwa kiarabu inaitwaje maana 3mzuka zinaitwa thalatha..........5,tano a.k.a mkono wanaita hamsa je six,6,kumi,10 wanaitaje kwa kule kwao?maana nasikia jamaa yupo jijini na jana ameswali msikiti wa mtoro hapo

Mkuu 10 kwa Kiarabu inaitwa A'SHARA

Kwahiyo Chelten au Chelsix kapigwa A'shara.
 
sasa kama simba imepigwa 5 na MO amejitokeza na kupiga mkwala mzito ikiwemo kuwafurusha baadhi ya wachezaji nyinyi mnapigwa 6,SITA,SIX baada ya kuchukua hatua munakimbia jukwaa......kweli hiki ni kikundi cha wala ganja kikiongozwa na kocha wao SARRI kheeeeeeeeeeee kheeeeeeeeeeeeeee kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee kheeeeeeeeeeeeeeee kheeeeeeeeeeeeeeeeee kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
Hichi kikundi ni ngumu kumotivate, sasa wewe umekuwa kama Sarri
 
Kwa mimi upeo wangu ma funs me naona tatizo halipo kwa sari Ila tatizo lipo kwa wachezaji Hawa tukirud nyuma Conte kasepa pale kwa kuto elewana na wachezaji wake monrinho nae ivo Ivo now linakuja kwa sari ,pale dalajan Kuna wachezaji wanajiona wao ndo wao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaa.. Wakati mwingine huu utani unaleta burudani sana. Kinachoburudisha ni utani kama huu ila kinachofurahisha zaidi ni utani wa kuamini sasa Chelsea keshakua jamvi la wageni kwa kuwa karuhusu goli sita bila majibu.



Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani hata Cardcitty watatudindishia maana huu mchezo wa jana utawapa confidence, tujiandae kisaikolojia tu nafasi 7/8 maana hata Wolves watatupita
 
Mkuu game ya jana wale jamaa walijipanga sana. Waliangalia makosa waliyafanya huko nyuma walishatusoma mistakes zetu walishaona makosa udhaifu wao. Kwa hiyo kilichotokea jana ni uzembe wetu katika defense na wao walifanyia marekebisho defense yao. Namlaumu Alonso na Luiz walikua wanafanya makosa mengi mno. Atleast Rudiger alikua anajitahidi.

Kule mbele huwezi kumlaumu Hazard walifanya kilichobidi lakini kwa ukabaji ule wanaanza kukaba kwetu wakipoteza mpira hawakusubiri ufike kati. Wanataka wao ndio wamiliki mpira. Mashambulizi yakifika kwao hawakufuati pembeni kuutafuta wanajaa pembezoni mwa 18 wanajua hazard ni mzuri kwenye ku drible anaweza kusababisha penalty au faulo wakati wowote. Wanaanza kukaba akitoa pasi hata akipiga shuti linaishia kwenye miguu yao. Yan hawa jamaa nina ubakika waliisoma game yetu kitambo na ndipo walipotumalizia hapo.

Kwa kiasi fulani bado namlaumu kocha kuzidi kumuamini Alonso na wakati kila siku hakuna kipya anacholeta.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sarri aliyajua hayo yote, kwa nini hakuja na mbinu mbadala?
 
HABARI ZILIZONIFIKIA HIVI PUNDE..
Ndugu mwanajf mwenzetu Ollachuga Oc tangu jana hali yake ni mbaya.. Alipata mshtuko wa moyo hiyo jana na kukimbizwa hospitali ya Mount MERU.. Hadi sasa hali yake haijatengamaa, madaktari wanafanya kumuhamishia hospitali ya rufaa ya KCMC..

Maombi na dua zenu ni muhimu kwa kipindi hichi kigumu kwake...
 
Sarri aliyajua hayo yote, kwa nini hakuja na mbinu mbadala?
Ndio maana nikasema kocha katuangusha. Naona ni heri tungemchukua Luis Enrique kuliko hiki kimbunga tulicho nacho sasa. Ngoja tuendelee kumpa muda kwa sababu bado nafasi anayo.

Tupo fainali Carabao, bado tupo EUROPA league. Hata nafasi ya kurudi top 4 ipo pia. Anaweza akashtuka badae

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom