Cheki Mkono wa Waziri Kagasheki kwenye vyumba vya habari

KAUDO

Senior Member
Aug 10, 2011
138
67
HABARI ILIYOTUMWA NA MWANDISHI NA ILIYOCHAPISHWA NA TZ DAIMA -CHEKI TOFAUTI
Na Ashura Jumapili,Bukoba,


Waziri asikitika meya kulalamika mbele ya madiwani

MEYA wa Manispaa ya Bukoba Dkt. Anatory Amani anayetokana na chama cha mapinduzi anawatuhumu baadhi ya viongozi wa chama chake kuwa wanawarubuni baadhi ya wafanayabiashara kwa kuwashinikiza kujiorodhesha majina yao na kisha kumfungulia kesi ya madai ya shilingi bln 5 kama fidia ya kupisha ujenzi wa soko la kisasa unaotarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi bln 12.

Dk. Amani alitoa tuhuma hizo katika kikao cha baraza la madiwani wa Manispaa hiyo kilichofanyika jana kilichohudhuriwa na waziri wa maliasili na utalii ambaye ni mbunge wa jimbo la bukoba mjini kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu uliofanyika 2010.
Alisema kuna kundi dogo la chama cha mapinduzi na baadhi ya viongozi ambao aliwataja katika kikao hicho kuwa ni Abdul Kagasheki,Abubakar Kagasheki na mauled Kambuga kuwa wanaochochea mgogoro wa ujenzi wa soko la kisasa katika Manispaa ya Bukoba unaotarajiwa kutumia kiasi cha shilingi bln 12.
‘nilifanya uchunguzi wa kina na kubaini kuwa vurugu na mgogoro wa baadhi ya wafanya biashara unasabaishwa na wananchama wenzangu niliowataja lakini nikatambua kuwa nikisema chnzo ni wao hata uongozi wa juu wa chama hautakubali kuwa Kagasheki anahusika nilisali mimi na familia yangu na mungu ametoa majibu haya ninayoyasema sina mashaka nayo’’alisema Dk.Amani.
Alisema anatolewa kafara kwa kushitakiwa yeye kama Amani na siyo Meya na kutakiwa kulipa shilingi bln 5 kama fidia kwa wafanyabiasha wa soko kuu kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo inayosimamiwa na chama chake na kuzinagatia maazimio ya baraza la Manispaa hiyo.
Alisema ujenzi wa soko hauna mbadala lazima soko lijengwe wanaopiga kelele waendelee isipokuwa Manispaa inaendelea kutekeleza mipango na mikakati iliyopo ya ujenzi wa soko.
Alisema baraza hilo lina madiwani wanaotokana na vyama vya siasa vitatu ambavyo ni chama cha mapinduzi ,chama cha wananchi ( Cuf )na chama cha demokrasia na maendeleo ( chadema .
Alisema madiwani wa upinzani waliopo katika baraza hilo hawapingi mambo ya maendeleo wanaiunga mkono na kushirikiana na Manispaa lakini baadhi ya mafisadi wa ( ccm )wenye pesa zao wanataka kuyumbisha mambo ya maendeleo kwa kuhofia kupoteza nafasi zao.
Alisema mikakati ya ujenzi wa soko itasimamiwa kikamilifu na kuhakikisha ujenzi huo unaanza haraka na kumalizika kwa wakati.
Ninashitakiwa kuwa mimi siyo Raia wa Tanzania ni wa Uganda haya yote ni kunitafuta nakukwamisha miradi ya maendeleo kwa mji wa Bukoba.
‘’nimeamua niyaseme haya pamoja na mafanikio yenye mvutano na changamoto nyingi lakini tutavuka nimesimama kidete kwa msikamano uliopo wa halmashauri bila kujali utofauti wa vyama vya siasa’’alisema meya.
Madiwani walisema kuwa Manispaa ndiyo inapaswa kushitakiwa kwa sababu hayo ni maamuzi ya baraza na meya ni msemaji anayewakilisha maamuzi ya baraza kwa wananchi.
Diwani wa Kata Hamgembe Robert Katunzi alisema kuwa mradi wa ujenzi wa soko ulikubaliwa na wadau zaidi ya 100 mwaka 2009 wakiwemo madiwani na meya natekeleza miradi aliyoikuta ikiwa katika maandiko ya vitabu vya kumbukumbu.
Katunzi alisema wanaomshitaki Meya wapeleke malalamiko yao ngazi za juu baraza hilo livunjwe kwa kutekeleza maandiko yaliyokuwa yanatekelezwa yaliyoachwa na uongozi uliopita katika maandishi.
Kwa upande wake waziri wa maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki ambaye pia ni mbunge wa jimbo hilo alisema “mambo haya yananitia simanzi ninashanga kiongozi kama meya unazungumza unalia madiwani hawawezi kukusaidia kitu mimi nazungumza kama waziri nitazungumza na baraza la Kikwete”alisema waziri Kagasheki.
Alisema mambo hayo mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa wanayafahamu watayafanyia kazi “najua yanatia simanzi”alisema waziri.
Naye mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Bukoba ambaye pia ni diwani wa Kata ya Kashai Yussuph Ngaiza amemtishi meya kumchulia hatua kwa kukidharirisha chama hadaharani mbele ya wapinzani au wakosoa hoja.
“nimesikitika sana kukizungumzia chama hadharani unapozungumzia chama unamzungumzia Kiwete sasa ninaanza kuchukua hatua”alisema mwenyekiti huyo.
Akiongea na Tanzania Daima kuhusu malalamiko yaliyotolewa na Meya kwa niaba ya wenzake Abdul Kagasheki alisema malalamiko hayo yahana ukweli wowote dhidi yao.
Kagasheki alisema “sisi tuko watatu ambao ni Maulid Kambuga diwani wa Kata Kagya,Abdul kagasheki mwenyekiti wa wazazi mkoa wa Kagera ambaye pia na ( MNEC )na Abubakar Kagasheki ambaye ni mwana chama wa ( ccm )tumemfungulia kesi ya kashfa alisema kuwa tunataka kumuua’’alisema MNEC huyo.
Alisema kesi waliyoifungua ni ya kashfa ya meya kutangaza kuwa wanataka kumuua ambayo inamtaka kiongozi huyo kufika mahakamani January 21 mwaka kesho kujibu.
Alisema hawahusiki na kesi ya wafanyabiashara wa sokoni isipokuwa wakili anayetumiwa na wafanyabiashara ndiye tunayemtumia kwa dhana yake anadhani ninahusika na kesi ya wafanyabishara hao.
Alisema kuhusu tuhuma za meya dhidi yake na wenzake kuwa wana mshitaki kuwa sio raia wa Tanzania ni wa Uganda Kesi hiyo pia imefunguliwa na wafanyabiashara hao pia sio wao kama anavyadai Meya.
Alipohojiwa juu ya tetesi zinazovuma kuwa anamapango wa kuhamia chama cha demokrasia na maendeleo( CHADEMA )alisema huo ni uvumi hana mpango huo.
‘’Mimi ni ( MNEC )wa Bukoba mjini siwezi kuhamia chadema nimeisha pata nafasi ya juu katika chama tawala sasa nitahamaje chadema ‘’alihoji MNEC huyo.
Hatutumii chama kumtuhumu isipokuwa yeye anatafuta sababu za kukisingizia chama wao wamemshitaki yeye binafsi wala kesi haiusiani na chama.
clip_image001.gif
Meya Bukuba alikoroga

na Ashura Jumapili, Bukoba

clip_image002.gif

KATIKA mazingira ya kujihami baada ya kubanwa na Baraza la Madiwani akitakiwa kufafanua kiasi cha fedha kitakachotumika kutekeleza mradi wa ujenzi wa soko la kisasa mjini Bukoba, Meya wa Manispaa hiyo, Dk. Anatory Amani, amelazimika kuibua tuhuma mpya akidai anahujumiwa.

Meya huyo ambaye ni Diwani wa Kata ya Kagondo (CCM), alitumia kikao hicho cha Baraza la Madiwani kilichoketi juzi, kuibua tuhuma kwa baadhi ya wanachama na viongozi wa chama hicho mbele ya Waziri wa Mali Asili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, ambaye pia ni mbunge wa Bukoba Mjini.



Kikao hicho kilimbana Meya Amani kikitaka kujua mradi huo utatekelezekaje kwa fedha kutoka vyanzo gani vya mapato na utagharimu shilingi ngapi hadi kukamilika.


Hatua hiyo ilikuja baada ya wajumbe kumlalamikia meya huyo kuwa amekuwa akifanya maauzi yote peke yake ikiwa ni pamoja na kusaini mikataba kadhaa ya kutekeleza miradi pasipo kuwashirikisha madiwani.

Hata hivyo, katika hatua ya kushangaza, Dk. Amani ambaye alionekana kujipanga mapema pamoja na wapambe wake, aligeuza kibao kwa ndugu wawili wa Balozi Kagasheki, ambao ni Abdul Kagasheki na Abubakar Kagasheki.



Meya Amani alidai kuwa wanachama hao wa CCM wanawarubuni baadhi ya wafanyabiashara mjini hapa kwa kuwashinikiza wajiorodheshe majina yao na kisha kumfungulia kesi ya madai ya sh bilioni 5 kama fidia ya kupisha ujenzi wa soko la kisasa utakaogharimu sh bilioni 12.



Katika kikako hicho ambacho Waziri Kagasheki akihudhuria kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu mwaka 2010, Meya Amani alisema kuwa **** kundi dogo wana-CCM na baadhi ya viongozi kama Abdul, Abubakar na Mauled Kambuga, wanachochea ili ujenzi huo usifanyike.



Alidai kuwa anatolewa kafara kwa kushtakiwa yeye binafsi na si kama meya, akitakiwa kulipa sh bilioni 5 kama fidia kwa wafanyabiashara wa soko kuu kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo inayosimamiwa na chama chake na kuzingatia maazimio ya baraza la manispaa hiyo.



Dk. Amani alimweleza Waziri Kagasheki kuwa baraza hilo lina madiwani wanaotokana na vyama vitatu vya CCM, CHADEMA na CUF lakini akabainisha kuwa madiwani wa upinzani hawapingi mambo ya maendeleo bali wanaunga mkono na kushirikiana na manispaa.



“Ninashtakiwa kuwa mimi si raia wa Tanzania bali wa Uganda, haya yote ni kunitafuta na kukwamisha miradi ya maendeleo kwa mji wa Bukoba,” alisema.


Akizungumza na gazeti hili jana jioni kutoka mjini Bukoba, Waziri Kagasheki alisema yeye kama mbunge wa Bukoba amesikitishwa sana na kitendo cha meya kushindwa kujibu hoja na badala yake kuibua tuhuma zisizo za msingi.

Kagasheki alisema kuwa miradi mingi jimboni humo inalalamikiwa na wananchi kutokana na meya kutowashirikisha na kwamba hata baraza la madiwani lilitaka awaeleze fedha za ujenzi wa soko zinapatikanaje.



“Inaonekana yako mambo mengi yanafanyika wananchi hawaelewi, sasa tunapohoji fedha hizi za walipa kodi ni kwa nini tuingize mambo ambayo ni tofauti na hoje lengwa. Jumamosi nitafanya mkutano na wananchi nitawaeleza kila kitu,” alisema Waziri Kagasheki.



Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukoba ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kashai, Yussuph Ngaiza, alitishia kumchukulia meya huyo hatua kwa kukidhalilisha chama hadharani mbele ya wapinzani.



Akijibu tuhuma za meya kwa niaba ya wenzake, Abdul Kagasheki, alisema malalamiko hayo hayana ukweli wowote dhidi yao.



Kagasheki ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Kagera, alisema kuwa yeye pamoja na Maulid Kambuga ambaye ni Diwani wa Kata Kagya na Abubakar Kagasheki, wamemfungulia kesi ya kashfa meya kutokana na kuwatangaza kwamba wanataka kumuua.



Alifafanua kuwa hawahusiki na kesi ya wafanyabiashara wa sokoni isipokuwa wakili anayewatetea wafanyabiashara hao ndiye anayewatetea pia wao.



 
Back
Top Bottom