chekelea weekend hii

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
213
Muuza bangi kafungua kiwanda cha kuuza gesi inayotumiwa kwa kupikia,siku ya pili kalipua kwa makusudi slenda mbili za gesi kikaungua kiwanda chake;kwanini?eti anafanya matangazo ya biashara - wateja wapajuwe kiwandani!!!.hehehehehehe

Baba, leo wamekuja watu kuuliza ikiwa hapa panauzwa pundwa.
Uliwaambiaje?
Niliwaambia kuwa hupo umeenda bandarini kubeba mizigo

Mwalimu wa somo la sayansi darasa la nne aliingia darasani na kuwaambia wanafunzi kuwa leo tunajifunza sayansi juu ya umuhimu wa chakula kwa binadamu sawa watoto wanafunzi wakajibu kwa pamoja ndioooo! mwalimu,mwalimu akawauliza swali wanafunzi,binadamu tunakula chakula ili iweje? wanafunzi hawakunyoosha mikono kwakuwa hakufahamu jibu lake ila mwanafunzi mmoja ambaye ni mtukutu sana darasani akawaza kimoyomoyo na kujisemea mwenye mhh,hili swali mwalimu kauliza ni la kimtegmtego lakini mimi mtego wakr nishaujua akanyoosha mkono mwalimu akasema enhee tunaomba jibu akajibu mwalimu minaona binadamu tunakula ili tunye, darasa zima likalipuka kwa kicheko na mwalimu nae akashika kichwa na kujisemea kimoyomoyo hapa sina mwanafunzi,baada ya muda yule mwanafunzi akawageukia wenzie na akawauliza mnashangaa nini kwani kuna mtu asiyekunya humu ndani.

Jamaa mmoja ambaye ni mwizi maarufu sana alikamatwa na wananchi wenye hasira kali akiwa anaiba tena alikuwa amebeba fuko la hela aliloiba,wananchi waliokusanyika kwaajili ya kumkomesha mwizi huyo kwa kumtoa roho yake ili kukomesha vitendo hivyo mtaani kwao kila mmoja alikuja na silaha ya aina yake mwenye panga,rungu,sime,bunduki,na kila aina ya silaha.waliamua kumuuliza sababu ya yeye kuiba ili wajue pengine aliiba kwa bahati mbaya,andipo yule mwizi akasema jamani msiniue nikweli kabisa nimeiba lakini naomba niwaeleze jinsi ilivyokuwa,jama akasema minilikuwa napita nikaona nyumba iko wazi nikaona pengine hii ni riziki yangu niliyobarikiwa na mungu, basi ........nikanyata ........nikanyata ......nikanyata ......huku anasogea mbele wale wananchi wanamuangalia tu, ghafla akakurupuka na kuingia mitini mmoja akasikika akisema minilijua tu atakimbia huyu,heheheheheheheheeeeeee!

kulikuwa na mashindano ya watu wafupi, katika hayo mashindano mshindi wa kwanza anazawadiwa gari yenye thamani ya shilingi milioni 350 na kupewa jumba la kifahali lenye thamani ya shilingi milioni 440,watu walikusanyika kushuhudia ninani na ni kwanini ataibuka kidedea,mashindano yalianza kwa kuingia mshiriki wa kwanza ambae alikuwa mfupi kama chemli,watu walishangilia sana huku wakisema ama kweli duniani kuna watu wafupi,mshiriki wa pili aliyeingia alikuwa mfupi kama kipande cha sabuni cha shilingi mia,watu wakavunjika mbavu wakasema jamani eeeeeee kwa mtindo huu dunia imekwisha,yaani.......yaani.......yani.......yaaaani we acha tu.kabla hawajamaliza kushangaa iliingia gari aina ya benzi dereva akafungua mlango akadondosha kiberiti chini watu wakapigwa na butwaa ghafla kiberiti kikafunguka akatoka mtu amevaa suti,watu wote pale ukumbini wakajobu hundred,hahahahehehehehihihihhohohohohmmmmmmmmmmmmmm

mshikaji mmoja ambae ni mwana michezo wa kunyanyua vitu vizito huko visiwani zanzibar,yaani huyu jamaa alikuwa na uwezo wakunyanyua gari aina ya prado kwa mkono mmoja,yakatokea mashindano ya kunyanyua vitu vizito kwa nchi za afrika,mashindano hayo yalikuwa yanafanyikia nchini kenya,mashabiki wake walifurahi sana, siku ya siku ikafika jama akaandaliwa kwaajili ya safari kuelekea kwenye mashindano,akiwa kwenye basi njiani alimuona mtu amebeba magari aina ya isuzu matano kichwani na mkononi analikokota treni lenye mabehewa 40,alishangaa,akawauliza abiria wenzake hivi yule jamaa anakwenda wapi? wakamwambia yule anarudi toka kenya kwenye mashindano ya kunyanyua vitu vizito,ameshindwa ndiomaana anarudi,yule jamaa akaanza kulia mayoooooooooooooooooo

mama mmoja huko china ilikuwa anakaa kwenye jengo lenye urefu wa ghorofa laki moja na elfu hamsini,mara nyingi hupenda kukaa juu ya paa la jengo kwa mapumziko ya kawaida,siku moja akiwa huko juu ya paa akiwa amembeba mtoto wake mchanga wa miezi miwili huku akimrusharusha kwania ya kumbembeleza,ghafla akaponyoka na kudondoka chini ya ghorofa,kwa uwezo wa mungu hakupata mdhara yeyote,yule mama akatoa ripoti polisi wakaja haraka sana kwa pamoja na yule mama wakaenda kumuangalia yule mtoto kule chini,walipofika walimkuta mtu mmoja mzee sana wakashangaa na kujiuliza jamani mtoto mwenyewe yuko wapi? ghafla yule mzee akaanza kuita mama mimi hapa mwanao yaani umenisahau? yule mama akiangalia sura inakujakuja,kumbe kutokana na urefu wa lile jengo yule mtoto alikuwa anaendelea kukua njiani kabla hajafika chini,heheheheeeeeeee
Hii sio joke bali ni mkasa wa kweli, nilikuwa nikisoma darasa la sita mwaka 1966 Haile Salise School Zanzibar, na tulkuwa na kipindi cha Kilimo,mara ghafla katuingilia Abeid Amani Karume, mwalimu wetu wa kilimo kasita kutusomesha baada ya kumuona rais kuingia darasani, Abeid Karume kamuambia mwalimu andelea kusomesha, basi mwalimu akaendelea kutusomesha na kusema kuwa miti ni kama binadamu zina roho zinataka hewa na maji bila hayo haziwezi kuishi, hapo tukamuona Abedi Karume zimeshoti akaanza kumtukana mwalimu na kutuambia sisi wanafunzi kuwa huyu mwalimu mwende wazimu hana akili ati miti zina roho ? hapo hapo katoa amri mwalimu afukuzwe kazi ya uwalimu apelekwe welezo hospitali ya wenda wazimu. Masikini mwalimu wetu alikuwa mwalimu nzuri sana na kabebwa juu kwa juu mpaka welezo.

mshikaji mmoja ambaye ana ndugu yake (kaka yake)anayeishi marekani kwa miaka mingi,siku moja aliamua kumtumia zawadi ya surali na shati alizozinunua kwa bei mbaya huko mjuu,baada ya kupata mzigo huo kwa njia ya posta alikwenda nao hadi nyumbani akiwa na furaha tele,alipofika akazijaribu zikamtosha vizuri tu lakini akasema hizi nguo sizivai mpaka siku ya jumapili kanisani,hatimae jumapili iliwadia jamaa akatika viwalo vyake anaelekea zake kanisani huku anajiangalia kila mara kama amependeza,watu walimshangaa kwajinsi alivyokuwa anajipiga chabo kila wakati,basi kabla ya kufika kanisani aliingia dukani akanunua sigara akawa anavuta huku akiendelea na safari sigara ilipokwisha na kubaki kipisi akasahau na kukitia mfukoni kikiwa bado kina moto ghafla ile suruali ikaanza kuungua na kufuka moshi mtu mmoja akawa anamwambia kaka angalia suruali yako inatoka moshi,yule jamaa kwa mbwembwe akamjibu acha ushamba wewe hii suruali nimeletewa juzi tu kutoka marekani we unafikiri inatoka moshi hii, kwani we unanionaje? baada ya hatua chache akaanza kujisikia jotojoto ghafla akaanza kupiga kelele mama naunguaaaaaa,hehehehehehehehehheeeeeee
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom