Chekechea Zifundishe kwa Kilugha

Petu Hapa

JF-Expert Member
Jan 2, 2008
714
55
Kutokana na kusahaulika kwa elimu ya awali haswa watoto waishio vijijini. Kutokana na umuhimu wa elimu ya awali katika mwendelezo wa elimu ya msingi na kujipanga kutengeneza jamii iliyoelimika kwa miaka ya mbeleni. Kutokana na ukata wa bajeti ya elimu na uchanga wa elimu ya awali tanzania. Kutokana na mifumo finyu ya kuendeleza lugha zetu, na utambuzi kwamba lugha za asili hazizui utambuzi wa mtu kajamii na kielimu. Je itakuwa sahihi kufikiria kuanzisha mfumo rahisi kabisa wa kuwafundisha watoto wa vijijini kwa kwa lugha mama zao katika elimu ya awali?
 
Back
Top Bottom