Cheka Unenepe: Nafasi za Masomo kwa kina nanihii

Jonogomero

Member
Feb 8, 2012
99
27
Chuo maalum kwa ajili ya kutoa ajira za chapchap kimefunguliwa hapa Kiborloni. Chuo Kimesajiliwa na VETA na kina waalimu waliobobea katika nyanja zote.

Chuo kinapokea maombi kwa wanafunzi waliomaliza darasa la saba au waliofeli Form IV kwa ajili ya kozi zifuatazo:-

1.** **Ulevi Mwezi mmoja

2.** **Ujambazi miezi sita

3.** **Kuchoma mtu kisu wiki moja

4.** **Kuchoma nyama kwenye baa miezi miwili

5.**** Kung'arisha viatu wiki tatu (Maalum kwa vijana wa Rombo)

6.** **Kuuza duka miezi mitatu

7.** **Kurekebisha mipaka ya kiwanja cha jirani miezi minne

8.** **Kupata mume msomi na mwenye wadhifa mkubwa miaka miwili

9.** **Kufuga ng'ombe mwaka mmoja

10.** **Kuendesha pick-up miezi minne

11.** **Kugombea udiwani miaka miwili

12.** **Kuendesha pikipiki za bodaboda na bajaji wiki sita

13.** **Kuchakachua mafuta mwaka mmoja

14.** **Kupata kazi TRA miezi mitatu

15.** **Kukwepa kodi wiki nane

16.** **Jinsi ya kuishi eneo la Kimara, Dar es salaam; na

17.** **Kukatisha tiketi kwenye magari ya Moshi, Dar na Arusha ni bure

Mwanafunzi lazima awe Mchaga wa kuzaliwa pia baba na mama yake wawe Wachaga, mwenye elimu ya msingi au kidato cha nne na asizidi miaka 21

Mwisho wa kupokea maombi ni kabla ya Pasaka ya mwaka huu wa 2012 saa 10.00 jioni. Maombi haya yasitumwe siku ya Ijumaa Kuu.

Nafasi za malazi zipo. Utapata nafasi ya kufanya mazoezi ya ziada ya kimasomo usiku na week end kulingana na kozi uliyoichagua. Watakaojiandikisha mapema watafundishwa bila malipo. Kipaumbele kitapewa kwa kina Manka na Meku.

Maommbi yatumwe:
Mkuu wa Chuo,
Chuo cha Waliobobea katika Kusaka
Fedha, PO Box 2,
Kiborloni, Moshi.
 
Back
Top Bottom