Cheka, simulia, lakini usiombe yakukute

Umesoma hadithi hii mwanzo hadi mwisho?

  • Ndio

    Votes: 3 50.0%
  • Hapana

    Votes: 3 50.0%

  • Total voters
    6
Long time no see Bishop. Mupo? Silioni lile gazeti letu pendwa. Afisi bado iko palepale Migomigo? Nataka nije kumiisalimuni.
Gazeti lipo ila limebadilishwa style, hivi sasa halitolewi kama zamani kibiashara bali ni kama NGO magazine fulani kwa ajili ya uhamasishaji wa mambo fulani fulani. Ofisi ilihama MIgomigo tangu 2007, siku hizi ipo jirani na viwanja vya Leaders Club, inatazamana na Ubalozi wa Kenya. Kwa sasa kampuni imekua sana kwani wana-produce mpaka TV Magazines, documentaries na feature films, pia inamiliki chuo cha sanaa (Gaba Arts Centre)...
 
Cheka, Simulia, Lakini Usiombe Yakukute - 13

Viguu vya Grego vilitetemeka wakati muda wa maakuli ulipojiri. Majeraha yake, iwavyo vyovyote vile, itakuwa yalishakuwa yamepona kabisa. Hakujihisi mapungufu yoyote kuihusu. Hili lilimstaajabisha na kulitafakari, namna zaidi ya mwezi mmoja uliopita alijikata kidogo kidoleni kwa kisu na namna jeraha hilo lilivyokuwa likimuuma yaani mpaka hata juzi.

“Yaelekea hisia zitanipungua,” aliwaza, huku akifyonza jibini kwa pupa, ambayo ilimvutia bila kusita, zaidi ya vyakula vyote vengine.

Harakaharaka na huku macho yake kodo kwa kuridhika, alikula jibini moja baada ya nyingine, ilhali mbogamboga, mchuzi, ugali, hakuviona aslan kuwa na ladha. Hakuweza kustahimili harufu zake na hata ikambidi abebe vile alivyotaka kuvila mbali navyo kidogo.

Kufikia muda dada yake polepole anazungusha ufunguo kama alama ya kumuashiria aondoke, Grego zamani alikuwa ameshamaliza kula na sasa alilala kivivu palepale alipokuwapo. Sauti hiyo ilimchanganya Grego, licha ya ukweli kwamba usingizi ulikuwa karibu umeshampitia, na akaharakia kujificha chini ya kochi.

Lakini alijizuia sana kuweza kubakia mulemule chini ya kochi, japo kwa muda mfupi dada yake alipokuwa chumbani, kwa vile alikuwa sasa ameshiba mlo maridhawa aliokula punde, na nafasi ile finyu ilimbana kiasi cha kuvuta pumzi kwa taabu.

Wakati hali ya kukosa pumzi ikiendelea kumshambulia Grego, alimtazama dada yake macho kodo, wakati dada yake asiye na habari akiendelea kufagia chumbani kwa fagio, siyo tu makombo ya chakula, bali hata vile vyakula vingine ambavyo Grego hakuvigusa kabisa, kana kwamba navyo sasa havikuwa na matumizi, na kisha kutupa kila kitu kwa haraka kwenye ndoo, aliyoifunika kwa mfuniko wa mbao, na kuvipeleka vyote nje ya chumba.

Kabla hata dada hakufika mbali, Grego alikuwa tayari keshajikongoja kutoka chini ya kochi, akajinyoosha, na kuuachia mwili wake ukae vizuri.

Inaendelea Sehemu ya 14
 
Cheka, Simulia, Lakini Usiombe Yakukute - 14


Ni kwa namna hiyo Grego alijipatia mlo wake kila siku, mara moja asubuhi, wakati wazazi wake na msaidizi wa nyumbani wakiwa bado wamelala, na mara ya pili punde baada ya mlo wa mchana, kwani wazazi wake, kama ilivyokuwa kawaida yao, huwa wameuchapa usingizi wa mchana kwa muda kidogo, na dada wa kazi huwa ametumwa na dada kwenye majukumu yake mbalimbali.

Bila shaka hawakutaka Grego afe njaa, lakini pengine hawakupenda tafrani ya kufahamu ni nini alichokula kwa njia nyingine zaidi ya kupitia maneno ya kusikia.

Pengine dada yake alitaka kuwaepusha na kile ambacho pengine kilikuwa ni kausumbufu tu kadogo, kwani tayari walikuwa wameshateseka sana.

Ni visingizio vipi walivitumia asubuhi ile ya kwanza kuwaondosha daktari na fundi wa kitasa, Grego hakuweza kubaini kwa hakika. Na kwa vile alikuwa haeleweki anachokiongea, hakuwepo yoyote, hata dada yake, aliyewaza kwamba huenda Grego akawa na uwezo wa kuelewa mazungumzo yao.

Hivyo, wakati dada yake akiwa chumbani, Grego ilimbidi atosheke na kusikiliza mara hii au ile, dada yake akigumia na kusali kwa watakatifu wa kale.

Ni pale tu baadae, wakati alipoanza kuzoea kila kitu kiaina (kwa kweli hapawezi kuwepo kwa mazungumzo ya dada kuzoea kabisa hali ile)


Wakati mwingine Grego alibamba neno la kumzungumzia, lililokusudiwa kuwa jema au ambalo linaweza kutafsiriwa hivyo.

“Mh, leo kakiona chakula ni kitamu,” alisema dada yake, kama Grego alifagia sahani ya mlo aliopewa; wakati ambapo, ikiwa ni kinyume chake, ambayo polepole ilizidi kujirudia mara kwa mara, dada alizoea kusema kwa huzuni, “sasa kila kitu kimesita tena.”

Japo Grego hakuweza kupata taarifa mpya moja kwa moja, alisikia mengi kutoka kwenye chumba jirani, kwani pindi asikiapo sauti, aliharakia kwenye mlango husika na kukandamiza mwili wake wote hapo.

Hasa kwa siku za mwanzoni, hapakuwa na maongezi ambayo hayakumhusu kwa namna moja au nyingine, ngaa kwa siri.

Kwa siku mbili wakati wa maakuli yote gumzo lilikuwa ni nini sasa kila mtu awe anafanya; lakini pia walizungumza pia hayohayo kwenye mida baina ya milo, kwani muda wote nyumbani palikuwa na walau watu wawili, kwa vile hakuwepo yoyote ambaye alikubali kubaki nyumbani peke yake na watu hawakuweza kuondoka nyumbani na kuacha nyumba bila mtu kwa sababu yoyote ile.


Na kana kwamba hiyo haitoshi, siku ileile ya kwanza, dada wa kazi (haijulikani ni nini na kwa kiasi gani alikuwa anafahamu yaliyokuwa yanaendelea), akiwa amepiga magoti alimbembeleza mama Grego amwachishe kazi mara moja, na alipokuwa akiaga takriban dakika kumi na tano baadaye, aliwashukuru kwa machozi kwa kumwachisha kazi, kana kwamba alikuwa akipokea hisani kubwa wenyeji waliyomfanyia, na aliapa kwa hofu kuu, pasipo kuambiwa na mtu, kiapo cha kutomsaliti yoyote, hata kwa kiasi kidogo.

Dada yake sasa ilimbidi aunganishe nguvu na mama yake katika masuala ya upishi, japo hilo halikuleta taabu kubwa kwa vile watu ni kama walikuwa hawali kitu.



Inaendelea Sehemu ya 15
 
Cheka, Simulia, Lakini Usiombe Yakukute - 15

Tena na tena Grego alisikiliza wakati mmoja wao akimkaribisha mwenzie chakula pasi na fanaka na asipokee jibu lolote zaidi ya “Asante. Nimeshiba” au maneno yanayokaribiana na hayo.

Na pengine walishasitisha hata kunywa, pia. Dada yake mara kwa mara alimuuliza baba iwapo angependa kupata bia na akijitolea kwenda kumchukulia yeye mwenyewe, dada alisema, na pale baba alipokuwa kimya, ili kuondoa pingamizi zozote ambazo angekuwa nazo, kwamba dada angeweza kumtuma mke wa kijana wa kazi aende kumchukulia. Lakini kisha baba alihitimisha mjadala kwa kusema “HAPANA” kubwa, na hakuna chochote tena kingeweza kuongelewa kuihusu.

Tayari siku ile ya kwanza baba yake aliweka bayana hali halisi ya kifedha na matarajio kwa mama Grego na kwa dada yake pia. Mara kwa mara aliinuka kutoka mezani na kuchopoa kibubu kidogo alichobakia nacho toka kwenye biashara yake, ambayo ilikufa miaka mitano iliyopita, dokumenti hii au ile au kijidaftari fulani.

Sauti yake ilikuwa ya kusikika kadiri alivyokuwa akifungua kufuli tata, na baada ya kuondosha alichokuwa akikitafuta, kukifunga tena.

Ndicho kitu cha kwanza cha kufurahisha ambacho Grego alipata nafasi ya kukisikia toka masaibu yake yamkute. Alikuwa anadhani kwamba hakuna kilichopona kutoka biashara ya baba yake; walau baba yake hakuwahi kumwambia chochote kinachokinzana na mawazo hayo, na Grego kwa upande wake hakuwahi kumuuliza. Wakati ule jambo moja tu alilolijali Grego lilikuwa ni kujitoa muhanga kwa kila kitu ili kuiwezesha familia kusahau mapema inavyowezekana masaibu ya kwenye biashara ambayo yaliwaletea wote hao kwenye hali ya ufukara.

Na hivyo kuanzia wakati huo alipoanza kufanya kazi kwa bidii na kutokea tarishi alipanda na kufikia afisa mauzo asafiriye, kama vile kwa kutwa moja, afisa mauzo asafiriye, ambaye ni wazi alikuwa na fursa kadhaa za kujiongezea kipato na ambaye mafanikio yake kazini yaligeuzwa kuwa pesa taslimu za kamisheni, ambazo zingeweza kuwekwa mezani nyumbani mbele ya wanafamilia waliostaajabishwa na kufurahishwa.

Hizo zilikuwa siku njema, na hazikujirudia kamwe baadaye, walau si kwa kiwango cha kusisimua kilekile, licha ya ukweli kwamba baadaye Grego alikuwa akipata pesa nyingi sana kiasi cha kuwa kwenye nafasi ya kubeba mzigo wa gharma za matumizi yote ya familia nzima, gharama ambazo, kwa hakika, alizibeba.

Na walifikia mahala pa kuzoea kabisa hali hiyo, pande zote mbili familia na Grego. Walichukua pesa hizo kwa shukrani, naye aliziachilia kwa furaha, lakini lile fukuto maalum halikuendelea tena kuwepo. Ni dada yake tu ndiye bado aliyebakia karibu na Grego, na ulikuwa ni mpango wa siri wa Grego kumpeleka (tofauti na Grego alivyo, dada alipenda sana muziki na alijua namna ya kupiga zumari maridhawa) mwakani chuoni, bila kujali gharama kubwa ambayo ingehitajika na ambayo ingeleta pengo ambalo lingehitaji kujaziwa kwa namna nyingine.
Mara hii au ile wakati wa muda mfupi Grego anakuwepo jijini, chuo cha muziki kilikuwa kinatajwa kwenye mazungumzo na dada yake, lakini mara zote kama vile tu ni njozi njema, ambayo kufikiwa kwake hakufikiriki, na wazazi wao hawakusikiza matarajio haya kwa furaha kamwe.

Lakini Grego aliyatafakari kwa kuyazingatia kwa makini na alikusudia kulielezea kwa mashamsham mkesha wa Krisimasi.

Katika hali yake ya sasa, fikra hizo zisizo na tija zilipita kichwani mwake, wakati akijisukumiza mlangoni na kusikiliza yanayojiri.

Wakati mwingine kutokana na kujichokea hakuweza kuendelea kusikiliza zaidi na aliachia kichwa chake kigonge mlango kizembezembe, lakini mara moja alijiweka sawa, kwani hata kasauti kadogo kalikotokana na kujongea kwake kalisikika huko sebuleni na kumnyamazisha kila mmoja.

ITAENDELEA
 
We naye unatuzingua tu hapa yan kimya chote hiki kimoja ndio umepost sasa s ungeacha tu
 
Cheka, Simulia, Lakini Usiombe Yakukute - 16

‘Keshaanza,’ alisema baba baada ya muda, wazi kabisa akiugeukia mlango, ni hapo tu ndipo mazungumzo yaliyokatishwa yalianza kurejea polepole.

Grego alitambua wazi kabisa (kwa vile baba yake alikuwa na hulka ya kurudiarudia maelezo, upande ni kwa vile ni muda mrefu ulikuwa umepita bila ya kujishughulisha na mambo ya nyumbani, na upande kwa vile mama yake hakuelewa kila kitu mara ileile yanaposikika mara ya kwanza) kwamba, licha ya masaibu yote, kiasi cha hela, japo kidogo sana, kilisalia kutokea zamani, na ambacho riba (ambayo haikuwa imeguswa) imekifanya kiongezeke ngaa kidogo katika muda uliokuwa umepita.

Kana kwamba hiyo haitoshi, pesa zile ambazo Grego alizileta kila mwezi (alijiwekea kajiakiba kadogo kwa ajili yake mwenyewe) hazikuwa zimetumika zote na zilikuwa zimekua na kugeuka kijimtaji kidogo.


Grego, akiwa nyuma ya mlango, alitikisa kichwa kwa hamasa, akifurahia maono haya na matumizi bora ya rasilmali ambayo hakuyategemea.

Ni kweli, kwa pesa hizi za ziada, angeweza kupunguza zaidi deni la baba kwa mwajiri wake na siku ambayo angeweza kujikomboa ingekuwa imesogea karibu zaidi sana, lakini sasa mambo yalikuwa pasi na shaka ni vema zaidi hivi yalivyo kama vile baba alivyoyapangilia.

Kwa wakati huo, hata hivyo, kiasi hiki cha pesa hakikukaribia aslan kutosha kuwezesha kaya kuishi kwa kutegemea malipo ya riba. Pengine yangeweza kuendesha familia kwa mwaka mmoja au zaidi sana miaka miwili, si zaidi.

Kwa hiyo kiasi hicho kilikuwa tu ni kama kiasi ambacho kilihitaji tu kutunzwa bila kutumiwa na kuachwa kiwe kwa ajili ya dharura. Lakini pesa za matumizi ya kila siku lazima zikatafutwe.

Kumbuka, baba yake alikuwa mtu mwenye siha njema, japokuwa alikuwa umri umeenda, na ambaye hakufanya kazi aslan kwa miaka mitano sasa na hivyo hangeweza kutegemewa sana.

Alikuwa katika miaka hii mitano, katika mapumziko yake ya kwanza kabisa katika maisha yake yaliyojaa taabu lakini pasi na fanaka, akaongezeka unene na kuwa mzito kweli.

Na ikishurutishwa mama yake mzee sasa afanye vibarua kutafuta hela, mwanamke aliyekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa pumu, ambaye hata kuzurura tu ndani ya nyumba kulikuwa ni taabu kubwa na ambaye alitumia siku moja katika kila siku mbili kwenye kochi lililo jirani na dirisha lililo wazi akitaabika kuvuta pumzi?

Ikiwa ni dada ndiye atakayetakiwa kuleta pesa za kuendesha familia, binti ambaye alikuwa bado umri mbichi wa miaka kumi na saba, ambaye maisha yake ya hapo kabla yalikuwa murua sana kiasi cha kuwa ni ya kuvalia nguo vizuri, kuchelewa kulala, kusaidia vijishughuli vya nyumbani, kushiriki furaha nyingine ndogondogo na, zaidi ya yote, kupiga zumari?

Ilipofikia mazungumzo ya kutafuta rizk, awal Grego aliondoka mlangoni na kujitupa kwenye kochi poa la ngozi karibu na mlango, kwani alikuwa anajihisi joto kwa aibu na huzuni.

Mara nyingi alijilaza pale usiku wote. Masaa yalikatika pasipo kupata lepe la usingizi na wakati mwingine aliparura tu ngozi kwa masaa.

Alijipa jukumu gumu sana la kusukumiza kiti kisogee dirishani. Kisha alitambaa mpaka kwenye kijiukuta cha dirisha na, akisaidiwa na kiti alichojishikiza nacho, aliegemea dirisha ili kuangalia nje, bila shaka akiwa na kumbukumbu hii au ile ya raha aliyokuwa akiipata aangaliapo nje zama za zamani.

Kiuhalisia, aliweza kubainisha vitu avitazamavyo kwa uwezo unaozidi kupungua, hata yale yaliyokuwa umbali mfupi tu: hospitali iliyokuwa upande wa pili wa mtaa, kitu alichochukia sana kukiona, sasa hakikuweza kuonekana tena, na kama hangekuwa anajua kwamba anaishi kwenye mtaa wa Shalote ulio tulivu lakini wa mjini, angeweza kuamini kwamba kutokea dirishani mwake, alikuwa anatazama mbuga chovu, ambayo anga la kijivu na ardhi ya kijivu viliunganika, na visivyoweza kutofautishwa.

Dada yake msikivu lazima atakuwa alishabaini mara kadhaa kwamba kile kiti kilikuwa dirishani; kwani, baada ya kufanya usafi, kila mara alikisukuma kile kiti kurudi palepale chini ya dirisha na kuanzia hapo hata aliacha wazi kidroo kilichokuwa kikifungwa.

Laiti Grego angeweza japo tu kuzungumza na dada yake na kumshukuru kwa kila kitu alichomtendea, angeweza kustahimili kivyepesi huduma dada anazomsaidia. Hali ilivyokuwa Grego alikuwa akiteseka. Dada yake ni bayana alijitahidi kupotezea hali ya sintofahamu ya kila kitu kadiri alivyoweza, na, kadiri muda ulivyokuwa ukienda, aliweza kuwa nguli zaidi kwa hayo.
Lakini kadiri muda ulivyokuwa ukienda, Grego pia alianza kuelewa kila kitu vyema zaidi.

Hata namna dada alivyoingia chumbani ilikuwa ni hali mbaya kwa Grego. Pindi tu aingiapo, hukimbilia dirishani, bila kutumia muda wowote kufunga mlango (licha ya ukweli kwamba mara nyingine zote alikuwa makini sana kuwahurumia wengine wasije wakaona vilivyomo chumbani kwa Grego), na alifungua dirisha kwa nguvu ya mikono yenye hamasa, kana kwamba alikuwa ni akosaye hewa ya kuvuta, na alibakia dirishani kwa muda kiasi hali akivuta pumzi ndefu, hata pale ambapo ilikuwa bado ni baridi kali.

Kukimbia kwake huku kulikoambatana na kelele kulimhofisha Grego mara mbili kila siku. Muda wote alikuwa akitetemeka chini ya kochi, japokuwa alifahamu vema sana kwamba bila shaka dada yake angemvumilia bila shida iwapo ingekuwa ni jambo linalowezekana dada kubakia wakati dirisha limefungwa kwenye chumba ambacho Grego yupo.

Siku moja (kama mwezi mmoja hivi ulikuwa umepita tokea Grego abadilike, na sasa hakukuwa na sababu ya maana kwa dada yake kustushwa na muonekano wa Grego) dada alifika mapema kuliko ilivyokuwa kawaida na akamkuta Grego akiwa bado yuko palepale akiangalia nje ya dirisha, ametulia na amekaa vizuri tayari kumtishia mtu.


Inaendelea Sehemu ya 17
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom