Check mambo ma 5 USIYOYAJUA kuhusu Freddie Mercury

anonymousafrica

JF-Expert Member
Aug 24, 2016
611
639
1-freddie-mercury-melanie-d-transparent.png

Nimefanya video.... karibu



Ila kwa ufupi tu , kuna mtu alisema kuwa
Freddie Mercury alizaliwa King Stone Zanzibar na kukulia visiwani humo kabla ya Wazazi wake kuhamia India na baadaye Middlesex England Kwenye ulimwengu wa burudani jina lake linatambulika kama gwiji wa muziki, muimbaji, mzalishaji na mtunzi wa nyimbo. Freddie aliyezaliwa mnamo 05 mwezi Septemba mwaka 1946 alifariki akiwa na umri wa miaka 45 mnamo tarehe 24 mwezi Novemba mwaka 1991 Mwanamuziki huyu alibainika kuwa amepata maambukizi ya vurusi vya UKIMWI siku chache kabla ya kifo chake Enzi za uhai wake alijinyakulia tuzo lukuki za kimataifa pamoja na kutengeneza nyimbo nyingi zilizokonga nyoyo za wapenzi wa burudani ulimwenguni Taifa la Uingereza lilitengeneza alama maalumu ya kumuenzi iliyowekwa Feltham jijini London huku nchi ya Uswisi ikitengeneza sanamu maalumu iliyoko Jijini Geneva

Me nikaongezea mambo matano ambayo ni

5. Freddie Mercury alikuwa na uwezo
usio wa kawaida katika mpangilio wa sauti... yani uimbaji

Uongeaji
wake ulikua kwenye baritone, lakini uimbaji wake mwingi ulianguka katika kiwango
cha tenor. Mnamo mwaka 2016, timu ya wanasayansi iliamua kusoma sauti ya
Mercury. Miongoni mwa mambo waliyoyathibitisha ni kwamba kamba za sauti za Mercury zilisonga
haraka kuliko mtu wa kawaida. "Wakati vibrato ya kawaida hubadilika kati ya 5.4 Hz na 6.9 Hz, Mercury ilikuwa 7.04
Hz," Matokeo ya Sauti yaliripoti.
4. Freddie Mercury alipenda sana paka.
Alipenda sana
paka hadi aliwafuga paka kumi sehem moja. Aliwahi toa album inayoitwa (Mr.
Bad Guy
) ambamo ndani yake aliandika kibao alichomdediketia nyau wake
mpendwa Delila
Icheki kidogo

Delilah, Delilah, oh
my, oh my, oh my - you're irresistible

You make me smile when I'm just about to cry

You bring me hope, you make me laugh - you like it

You get away with murder, so innocent

But when you throw a moody you're all claws and you bite -

That's alright !

Delilah, Delilah, oh my, oh my, oh my - you're unpredictable

You make me so very happy

When you cuddle up and go to sleep beside me

And then you make me slightly mad

When you pee all over my Chippendale Suite​
3.
Inaripotiwa ya kwamba Freddie Mercury alikua na aibu iliyopitiliza.

Licha ya kutambulika kuwa ni mtu mwenye fujo nyingi
jukwaani, watu wengi waliomtambua kwa maisha ya kawaida wanasema alikua ni mtu
mwenye aibu nyingi nah ii ndio sababu ya yeye kutoonekana kwenye interview
nyingi kama walivyokua ma star wengine. Katika maisha ya kawaida hakuna
anayemfaham Freddie (mshirika
mwenzake wa kwenye band Roger Taylor aliwahi kusema) Alikua mwenye aibu
na mstaarabu. Hajawahi kuwa Yule anayeonekana stejini.
2. Microphone isiyoishia chini (iliyo nusu almaarufu kama
"bottomless mic" ilikua ndo bidhaa yake kubwa nahii ilipelekea kupata
wateja wengi pia wa aina hii ya mike.
Mwanzoni kabisa
mwa kundi la queens, Freddie na wenzake wakiwa stejini. Stand ya mike ya
Freddie ilichomoka na kubaki kipande lakini chaajabu hakubadilisha microphone
na ukawa ndio mwanzo way eye kuanza kutumia microphone fupi.
1. Freddie Mercury aliwahi kuwa mpakiaji na mbeba mizigo
katika kiwanja cha ndege cha Heathrow.
Mwanzoni kabla
hajawa msanii maarufu Mercury aliwahi kuwa kwenye kitengo cha mizigo katika Heathrow
Airport. Katika kusherehekea miaka 72 toka azaliwe Freddie, Baadhi ya
wafanyakazi wa British Airways kitengo cha mizigo waliwaburudisha abiria kwa
kuvaa na kujiweka kimwonekano wa Freddie huku wakiimba na kucheza kwa
kumkumbuka mfanyakazi mwenzao.

Mambo Ma 5 Usiyoyajua Kuhusu Freddie Mercury
 
Kuna movie yake inaitwa Bohemian Rhapsody ameigiza rami malek (yuke star wa tv series ya mr robot) na hiyo movie ambayo rami kaigiza kama freddie imepata tuzo 5 za Oscar na nyingine 32 duniani kote.. Kupitia hii movie ndo ikanifumbua macho maisha ya huyu jamaa kumbe ni reality kabisa..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna movie yake inaitwa Bohemian Rhapsody ameigiza rami malek (yuke star wa tv series ya mr robot) na hiyo movie ambayo rami kaigiza kama freddie imepata tuzo 5 za Oscar na nyingine 32 duniani kote.. Kupitia hii movie ndo ikanifumbua macho maisha ya huyu jamaa kumbe ni reality kabisa..

Sent using Jamii Forums mobile app
AHSANTE SANA, ni kweli na nlikua mtu wa mwanzo kuandika hiki kitu kwenye thrd flani hivi
 
Kati ya mambo matano ambayo wengi pia hawayajui ni kuwa Freddie Mercury pia alikuwa ni shoga!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi ndivyo nilivyosema! Sijasema kuhusu HIV yake. Ukiandika kitu uwe na kumbukumbu! Unaposema kila mtu unamaanisha watu wote!
SIJASEMA KITU KAMA HIKO...... mchangiaje amesema, lingine lisilojulikana ni kwamba alikua na HIV, nikamjibu hilo kila mtu analijua. Sikumaanisha kila mtu anamjua Freddie, na haiwezekani tumjue kila mtu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom