Chatu ammeza dreva, aacha gari porini! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chatu ammeza dreva, aacha gari porini!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nyange, Aug 18, 2010.

 1. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,186
  Likes Received: 231
  Trophy Points: 160
  Wakuu nimeona niwashirikishe kisa cha kweli kilichotokea hivi karibuni, ili kisaidie kufanya maamuzi sahihi wakati wote.

  Dreva wa magari yanayo safirishwa nje ya nchi kupitia bandari ya Dar es salaam yenye namba 'IT' amekumbwa na kifo baada ya kumezwa na chatu, pale alipo patwa na haja kubwa na kuamua kuacha gari (silensa) na kuingia porini ili achimbe dawa. Kumbe Chatu mkubwa akiwa na njaa yuko mawindoni akafanikiwa kumkamata na kummeza!.

  Madreva wenzie, walio kuwa na magari ya aina hiyo wakisafiri kwa pamoja, walishangaa baada ya kuona kuwa yeye na gari yake hawaonekani, wakati wanampigia simu inaita mpaka inakata bila kupokelewa. Mwanzo walidhani kuwa kuchimba dawa ni starehe hivo, akimaliza kuchimba dawa, atajibu simu zao. Mara wanaona kimya! hapo ilikuwa kama saa 2 usiku na walikuwa wanakaribia kufika mpakani Zambia.

  Baadhi yao (Madreva wenzake) wakaamua kurudi nyuma kuona kulikoni. haikuwachukua muda, mara wakarikaribia gari na bado liko( on) yaani limepack na liko kwenye 'silensa' wakaangalia huku na huku, na kuna giza, pia wakiita, bila mafanikio.

  Iliwalazimu kwenda kuwaambia wenzao walio kuwa wametangulia mbele. Kwakuwa usiku ulikuwa unazidi, wakaamua kuelekea karibu na mpakani mwa TZ na Zambia kutoa taarifa Polisi. Kilicho fanyika, Polisi na baadhi ya madreva hao, walirudi kwenye eneo la tukio na kuamua kuchukua gari hilo mpaka kituoni, ili kesho waanze zoezi la kumtafuta huyo dreva.

  Asubuhi na mapema waliondoka na polisi wawili wakiwa na silaha kwenda kweye eneo la tukio. wakaanza kuzungukia maeneo hayo, ghafla kama hatua kumi kutoka kwenye tukio wakamwona Chatu mkubwa akiwa amejilaza na asiweze hata kusogea.! Mmoja wao akapiga yowe na kusema Jamani ni chatu ndiye aliye leta balaa! Askari ammoja aliye kuwa karibu, akatoa msaada wa kumuua chatu kwa risasi.

  Baada ya kumuua Chatu huyo wakapasua tumbo wakamkuta maskini dreva kesha kufa, na simu yake iikakutwa na missed call walizokuwa wakimpigia!

  USHAURI' TUNZA MAZINGIRA NA ACHA UBAHILI WA SH. 200 UOKOE MAISHA. - KISA HIKI NI CHA KWELI KABISA.
   
 2. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  mhhh...sasa njiani kama barabara za vjj napo kuna toilets za kulipia?
   
 3. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #3
  Aug 18, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,830
  Likes Received: 10,142
  Trophy Points: 280
  Ina maana simu ilikuwa ikiita ndani ya tumbo la chatu, sijaelewa hapo mpwa.....au ndo zile hadithi za sungura na fisi???
  asante kwa somo lako zuri stay blessed
   
 4. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #4
  Aug 18, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,186
  Likes Received: 231
  Trophy Points: 160
  Inabidi halimashauri zijipange. Majanga yako mengi, yale yanayo zuilika yadhibitiwe tupambane na yale yasiyozuilika.:confused2:
   
 5. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #5
  Aug 18, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  simu ilikuwa inaita tumboni mwa chatu? anyway; RIP
   
 6. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #6
  Aug 18, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,186
  Likes Received: 231
  Trophy Points: 160
  Mkuu, simu ilikuwa ikiita wakati kesha mezwa! Mungu ameumba bwana hayo ni maajabu ya Mungu.
   
 7. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #7
  Aug 18, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  mhh nyange bwana...nchi ina matatizo kibao kibao, shule hadimu, umeme wa mawazo, hosp zenyewe ovyo yaani hakuna kinachoelkeweka, sasa wewe umeona hilo ndio waanze nalo kujipanga?
   
 8. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #8
  Aug 18, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,186
  Likes Received: 231
  Trophy Points: 160
  Mkuu huamini ??????? Keshaonekana Musa matatizo mbona yatakwisha tu? Washikaji miaka kibao wameshindwa hata kuboresha shule za akina kayumba! Tunasubiri kutawazwa kwa uongozi mpya.
   
 9. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #9
  Aug 18, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,830
  Likes Received: 10,142
  Trophy Points: 280
  Hakuna HADIMU kuna ADIMU by the way hili nalo neno, Nyange anajaribu kueleza miongoni mwa matatizo yetu, Asante Nyange, hili jina lako linanikumbusha kwa wakwe zangu Tanga
   
 10. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #10
  Aug 18, 2010
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Is this possible? Chatu kummeza mtu mzima wandugu?
   
 11. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #11
  Aug 18, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,830
  Likes Received: 10,142
  Trophy Points: 280
  Yes, it is...ulidhania anakufuata na kukuomba akumeze??? Hapana, MUNGU wa ajbu, nao pia wana namna zao za uwindaji atii
   
 12. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #12
  Aug 18, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Hehehehe huyo chatu naona anamdomo mkubwa size ya pipa la debe 8
   
 13. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #13
  Aug 18, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  duuh maskini
   
 14. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #14
  Aug 18, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,186
  Likes Received: 231
  Trophy Points: 160
  Hebu jaribu kusoma hurka za wanyama. Mwanangu hata kama una silaha, chatu akiwa mawindoni mwanangu huchomoki!
   
 15. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #15
  Aug 18, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Nyie hamuamini? ni mkoa gani vile mkuu?.....................MBY! teh teh, msifikirie mbali.
   
 16. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #16
  Aug 18, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,186
  Likes Received: 231
  Trophy Points: 160
  Ndugu yangu mbona unasahau maajabu ya Mungu! Kama mama anaweza kujifungua mtoto wa kilo 6 kwa njia ya kawaida, tena ile tunayoijua, sembuse Chatu kummeza mtu!, Nyati ni chakula chake cha kawaida mbona!
   
 17. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #17
  Aug 18, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  nyati gani unayemzungumzia wewe, ndama?
   
 18. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #18
  Aug 18, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Ni ngumu sana unless mtu mwenyewe awe diminutive na chatu mwenyewe awe mkubwa kwelikweli. Nimeshaangalia sana vipindi vya hawa wanyama kwenye National Geographic na mpaka sasa hakuna documented cases zozote zile za chatu au Anaconda kumeza watu wazima.
   
 19. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #19
  Aug 18, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Nilishashuhudia Chatu akipasuliwa na kutolewa ng'ombe mkubwa sana(zaidi ya mtu),kilichokuwa kimevunjika ni miguu tu.tangu siku hiyo nikiambiwa chatu kameza chochote sishangai
   
 20. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #20
  Aug 18, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,186
  Likes Received: 231
  Trophy Points: 160
  Hebu contact na game keepers about nature and characteristics za huyo mnyama. In short it is dangerous animal
   
Loading...