Chato yazidi kuneemeka; Serikali kujenga Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Ziwa

iHistoria haijampa somo vizuri, kama kule kijijini kwao Mobutu na kwao Humphouet Boigny
 
... Ummy naye kashindwa kujenga hoja vizuri. Kama Kanda ya Ziwa ina "wagonjwa" wengi kuliko maeneo mengine kwanini Chato? Au Chato ni center ya kanda ile? Kwanini sio Kahama, au miji mingine mikubwa kama Shinyanga?

Mkuu ndiyo maana wahenga walisema "njia ya mwongo fupi." Hana hoja ya maana ya kutetea huo uamuzi.
 
iHistoria haijampa somo vizuri, kama kule kijijini kwao Mobutu na kwao Humphouet Boigny
Chato siyo kijijini. Chato ni mji mdogo toka enzi za ukoloni. Ni bandari na ina ginnery ya kuchambua pamba toka mwanzoni mwa miaka ya sitini. Iko kwenye barabara kuu ya Bukoba - Muleba - Bwanga. Usilinganishe kijiji ch Mobutu na Chato ambayo.tayari ni makao makuu ya wilaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu unataka kila kitu kiwe dar hapana aisee dar kumejaa huduma nyingine tuziweke mkoani badala ya kwenda india
Shida iko hapa.kwanini kilakitu chato .hatukusikia kila kitu msoga,msoga msoga
 
Baada ya Waziri Ummy kueleza hayo, baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CCM), Peter Serukamba walicheka.

Miaka ile ya kusikiliza Bunge kwenye radio Marehemu Phares Kabuye, alipata kuuliza kama kuna mtu amepata kumuona mtu mzima anakula ugali kwa mikono miwili! Haijapata kutokea lakini ndiyo haya yanayoendelea Chato; watu wazima wanakula kwa mikono miwili! Ajabu na kweli.
 
Hakuna cha ubaba! Taifa umaskini chanzo ni yeye. Magufuli ndiyo ananyoosha hii sasa.

Pwani ipi? Au hujui viwanda takribani 73 vimejengwa enzi za Kikwete?! Mloganzila kwanini haikupelekwa Iringa?!

Tuwe wakweli zama za Umwinyi na Umangi kwisha habari yake. U-Daslam utapotea ili taifa lisonge.

Haiwezekani mtu Kigoma na Kagera yupo mahtuti mpaka afike Daslam kwa tiba! Haiwezekani, Daslam ni kipande kidogo sana kwa Tanzania.

Maendeleo endelevu ya Tanzania
Hoja yako afifu,Hospital za Mikoa zingeboreshwa kwa kiwango cha kuwa za rufaa na kikanda .
 
Pembezoni ipi unayoisemea?! Daslam?, Zama hizo zimeisha.

Kwa takribani miaka 60 sasa wakazi wa Kigoma na Kagera wamekuwa wakifuata huduma za kijamii Daslam, Elimu ya juu, Hospitali, Usafiri wa Kimataifa na mengineyo. Haiwezekani hii lazima ifike ukomo kwa maendeleo ya taifa hili! U-Daslam lazima ufe.
Suluhisho ni kuboresha hospital za Kagera au Kigoma kufikia uwezo wa hospital za kikanda.
 
Serikali ya Tanzania itajenga Hospitali ya Rufaa wilayani Chato Mkoa wa Geita.
Akiwasilisha taarifa yake kwa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii leo Jumatatu Januari 20, 2020, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu amesema Serikali inatarajia kujenga hospitali hiyo kutokana na idadi kubwa ya watu kuwa eneo hilo.

“Tumefanya utafiti na kugundua kuna wagonjwa wengi Kanda ya Ziwa kwa hiyo tunajenga Zonal Hospital (hospitali ya Kanda) Chato,” amesema.

Amesema kuwa sababu ya kujenga hospitali hiyo Chato ni Mikoa ya kanda ya ziwa kuwa na watu zaidi milioni 15.

Baada ya Waziri Ummy kueleza hayo, baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CCM), Peter Serukamba walicheka.

Baadaye wajumbe wa kamati hiyo watapata fursa ya kuichangia na kama kutakuwa na maswali, mapendekezo watayatoa.

Chanzo: Mwananchi

Pia soma Serikali kujenga hospitali ya kikanda ya kitalii Geita

"Baadaye wajumbe wa kamati hiyo watapata fursa ya kuichangia na kama kutakuwa na maswali, mapendekezo watayatoa".
Pole serukamba ulishindwa kuwa mnafiq
 
Serikali imesema ina dhamiria kujenga hospital ya kanda ya Ziwa huko Chato mkoani Geita

Waziri wa Afya jinsia na watoto amebainisha hilo leo

My take: kwa nini ijengwe Chato na si Mwanza kitovu cha kanda ya Ziwa au Geita makao makuu ya mkoa?

Source Mwananchi

Sent using Jamii Forums mobile app
Baadaye wajumbe wa kamati hiyo watapata fursa ya kuichangia na kama kutakuwa na maswali, mapendekezo watayatoa.
 
Mobutu wa Chato tumemchoka. Mwaka huu hatoboi URAIS. Tuone Kama hata hiyo international airport pale Chato itatumika.
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom