Chato yazidi 'kujimwambafai', Serikali kujenga Chuo cha VETA kwa TZS 10.7 bilioni. Dr. Kalemani aomba Chuo Kikuu

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,060
4,044
Mbunge wa Chato (CCM), Dk Merdard Kalemani ameiomba Wizara ya Elimu kujenga chuo kikuu wilayani Chato Mkoa wa Geita ili wanafunzi wanaomaliza elimu ya sekondari waweze kujiunga na chuo hicho.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Oktoba 2, 2019 katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika chuo cha mafunzo ya ufundi cha wilaya ya Chato, akibainisha kuwa tayari wilaya imetenga eneo kwa ajili ya ujenzi wa chuo kikuu.

Akizungumzia chuo cha Veta, Dk Kalemani ambaye ni Waziri wa Nishati ameomba chuo hicho kinachojengwa kwa Sh10.7 bilioni kufundisha lugha za kimataifa ili vijana wa Chato waweze kujifunza na kupata ujuzi wa kuwahudumia watalii watakao tembelea Hifadhi ya Burigi Chato.

Mkuu wa mkoa wa Geita, Robert Gabriel amesema ni muhimu Chato kuwa na chuo kikuu cha afya kwa kuwa hospitali ya kanda inajengwa katika wilaya hiyo, “ni jambo zuri chuo kikajengwa kwa ajili ya wanafunzi wa wa afya.”

Chuo cha wilaya ya Chato kinatarajia kudahili wanafunzi 480 wa muda mrefu na 800 wa muda mfupi na hadi sasa kimekamilika kwa asilimia 78 na kinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Novemba, 2019.

Chanzo: Mwananchi
 
Aisee! Ikulu Ndogo,International Airport, MSD ya mkoa, CRDB bank, Jengo La TRA, Jengo La Tanesco, Bandari, Hospital Ya Rufaa Ya Kanda, Chuo Cha Veta Na sasa wanataka chuo kikuu. Aya mambo yanafanyika kwenye population ya watu ambao hawafiki hata Laki 4. Wakati Kuna Mikoa Ina Watu Zaidi Ya Mil 2 Hawana Hizi Huduma.

Izi Pesa Ukijumlisha Ni Kama Bil 500 Ndani Ya Miaka 5 Ya Kwanza Maana Yake Jamaa Anaweza Tumia Trion 1 Kuwekeza Kwao Kabla Ya 2025
 
Ule uchea wa sadeki angeutumia kama anavyotumia nafasi yake kwa jimbo lake Tizi tutakuwa mbali ndani ya mwaka huu moja
 
Nawapongeza, ni jukumu lao kuwapa vijana elimu inayoendana na mazingira ya nchi hasa katika kipindi hiki ambacho ajira ni ngumu.
Wajitahidi wavieneze vyuo hizi kila kanda kwa idadi inayokidhi mahitaji na warahisishe vigezo na ada za kujiunga navyo.
 

Katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, VETA inasimamia Ujenzi wa Chuo cha VETA cha Mkoa wa Geita wenye thamani ya Sh. 9.9 na fedha zinazogharamia mradi huo zinatokana na mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB); ujenzi wa Chuo cha VETA cha Wilaya ya Chato wenye thamani ya Sh. bilioni 10.7 ambazo ni fedha za ndani; ujenzi wa chuo cha VETA cha Mkoa wa Kagera wenye thamani ya Sh. bilioni 20 ambao unagharamiwa na Serikali ya China na ukarabati wa Chuo cha Ufundi Stadi Karagwe wenye thamani ya Sh. bilioni 4.6 fedha za ndani.
 
Watu wa Chato endeleeni kujimwambafai tu.Ni awamu yenu hii. Maana hakuna wa kupinga hayo maendeleo yenu. Nahisi kuna maagizo na maelekezo toka juu.
 
Aisee! Ikulu Ndogo,International Airport, MSD ya mkoa, CRDB bank, Jengo La TRA, Jengo La Tanesco, Bandari, Hospital Ya Rufaa Ya Kanda, Chuo Cha Veta Na sasa wanataka chuo kikuu. Aya mambo yanafanyika kwenye population ya watu ambao hawafiki hata Laki 4. Wakati Kuna Mikoa Ina Watu Zaidi Ya Mil 2 Hawana Hizi Huduma.

Izi Pesa Ukijumlisha Ni Kama Bil 500 Ndani Ya Miaka 5 Ya Kwanza Maana Yake Jamaa Anaweza Tumia Trion 1 Kuwekeza Kwao Kabla Ya 2025
Chato hakuna Ikulu ndogo, kuna nyumba ya Magufuli hivyo akiwa likizo wakati mwingine anaitumia kama ofisi.
 
Ndio maana shule kumi bora za msingi zimetoka kanda ya ziwa,huu ni mkakati-vyuo yva veta na sasa chuo kikuu vyote ni sehemu ya mkakati,vipi sisi wa kanda ya kusini??
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom