Chato: Wananchi walilipia umeme wa REA tangia mwezi wa tisa lakini hadi sasa hajapewa umeme

Kimla

JF-Expert Member
Jun 8, 2008
3,337
5,571
Wananjamvi-Mbunge Kalemani aliahamaisha sana watu kufanya wiring tayari kwa kuvuta umeme, Vijiji vya Bikaka na Nyakakarango tukafanya hivyo hadi tukaletewa Control namba ya kulipia umeme mnano mwezi wa tisa lakini hadi hivi sasa haujapata umeme.

Je, huu waziri wa Nishati na Pia Mbuge sijui kwanini hataki kusikiliza matatizo ya wananchi wake na kuyafanyia kazi. Mwananchi kauza kuku, Ngombe na kufanya wiring,, bado serikali ikaleta control namba tukalipa lakini hatuunganishiwi umeme.

Je, kuna nini nyuma ya pazia au ndo pesa zimeliwa na wananchi kutapeliwa na mbunge wao na serikali yao?

Nini wananchi tufanye kupata haki yetu ya umeme?
 
Inasikitsha sana. REA tunawalipa pesa kwa ajili ya kusambaza umeme kwa elfu 27 kwenye vijiji, why wanadelay? Wameshindwa kazi? Ni upuuzi wanachukua mabilioni yetu ambayo tunachangia halafu wanashindwa kuwapa wananchi umeme.
 
Hii iko kote

Mathalan pale zingiziwa chanika, ukilipa 27k utasubiri sanaa, ila lipa ile ya 321k.

Ndani ya siku 3 wanaunga umeme fasta
 
Na nyie mtulie sasa chato chato mambo yote mliofanyiwa bado hamna shukrani kuna vijiji vingi hali mbaya wala hawalalamiki watulize mshono serikali ina mambo mengi ya kufanya
 
REA ni kwa ajili ya vijiji, sio miji. Kama waliunganishwa chini ya mpango wa REA, basi hawastahili kupewa mkoa wa Chato, waendelee kuwa wilaya
 
Na nyie mtulie sasa chato chato mambo yote mliofanyiwa bado hamna shukrani kuna vijiji vingi hali mbaya wala hawalalamiki watulize mshono serikali ina mambo mengi ya kufanya
Kwa sasa Chato ni sehemu ya Tanzania, ni vema wahusika wakawasikiliza kama wananchi wengine. Wakati ikiwa nchi inayohitegemea haya hayakuwepo.

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom