Chato: Wafanya biashara wadogo wakana kumjua Steven Joseph Wandwi

Hii imekuwa kama ile ya jambazi kuvua viatu wakati anaingia kuiba
Huyu ni muuza chipsi aliyemfanyia maombo Rais Magufuli na baadaye alipewa laki moja na mh. Rais ili akuze mtaji wake wa chipsi.

Kijana huyu mwenye miaka 23 alijichanganya kwa kutoa taarifa zisizo endana ambazo zimezua maswali mengi kwa watanzania na kuona lile lilikuwa ni igizo lililopangwa ili kunasa fikra za watanzania na kukuza coverage ya serikali iliyopo madarakani.

Kijana Steven Joseph mwanzo alisema kuwa alitoka Mara na kwenda Chato kwa lengo la kwenda kumuona mh. Rais na kumpongeza kwa kazi anazozifanya mh. Rais za kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya nchi.

Akiwa amekisahau alichosema mwanzo, Steven Joseph akasema yeye ni mkazi wa Chato na anakibanda cha kuuza chipsi pale Chato. Inaonekana Kijana Steven hakusoma na kunakiri vizuri script ya movie mwisho wa siku akaharibu movie nzima. Pengine director wa movie hiyo hawakumpa kijana huyo muda wa kutosha wa kuifanyia mazoezi movie hiyo.

Sasa kuna wafanyabiasha wadogo wadogo wa maeneo ambayo Steven amesema anafanyia biashara zake za kukaangia chipsi wamesema hawamjui kabisa na ndiyo kwanza wengine wamesema wamemuona siku ile alipokuwa anafanya maombi mbele ya Rais.

Directors pangeni maigizo yenu vizuri mnatia aibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muuza chips mwongo mwongo.. Huenda akawauzia watu mishikaki ya mbwa akidai ni ya punda alivyomsaulifu
Kama katoka mkoa wa mara yaweza kuwa ni mtoto au mjukuu wa mzwee wandwi (sina hakika). Askari mstaafu na mwana CUF aliyelitafuta jimbo la msoma mjini mara kadhaa bila mafanikio kati ya 2000 hadi 2010. Sina hakika kama aligombea tena 2015 kwani sikuwa tena huko. Naukumbuka sana uchaguzi wa mwaka 2005 tulimfanyia figisu jimbo likaenda kwa Vedastus Mathayo Manyinyi.
 
Hata yule aliyemsajiria line rais mwishoni mbona hakumchaji hela ya line,nae huenda yakawa maigizo mengine
Mkuu ile Mh. raisi kwenda kusajili SIM Card ni symbolic tu, ukweli ni kwamba namba yake binafsi haipaswi kujulikana hata na yule msajili wa namba za simu.
Na lazima iwe maalum ktk huduma flani. Pale ni kampeni tu ya kuhamasisha usajili wa simu.
Kama vile raisi anavyoenda kupimwa HIV hadharani na daktari au muuguzi wa kawaida. Mtu asiye ktk mfumo wake maalum wa matibabu hapaswi kujuwa hali ya afya ya raisi duniani kote.
Lakini ulimuona Mh. Kikwete na mkewe walienda kupima HIV hadharani enzi zile yupo raisi wa JMTZ.
Sio ajabu alipomaliza kupima damu na vifaa vyote alivyotumia na damu yake vilichukuliwa na watu wa usalama wa raisi mara tu baada ya kuondoa kamera za wana habari.
 
Hata yule aliyemsajiria line rais mwishoni mbona hakumchaji hela ya line,nae huenda yakawa maigizo mengine
Nawe unajichanganya! Ajabu unapewa likes! Kusajili line kwa vidole unalipia? Kwani rais alinunua line mpya?
Elimu yetu ina matatizo, hakika!
 
Mleta mada kama huna cha kuandika ni bora kipindihiki cha mvua muda uliotumia kuandika uo upuuzi unge utumia kulima ata tuta moja la viazi familia yako ingekuona wa maana pindi utakapo vuna.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hilo tuta la viazi la mleta mada litatupatia viazi vingi sana na watu wengi sana watapata ufahamu.
 
Nawe unajichanganya! Ajabu unapewa likes! Kusajili line kwa vidole unalipia? Kwani rais alinunua line mpya?
Elimu yetu ina matatizo, hakika!
Huyo unaemuita rais aliomba achaguliwe line mpya kabisa ndo aisajili... Kusoma hamjui... Kuangalia picha hamjui...! Daah!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom