KHALFANI 86
Member
- May 16, 2020
- 14
- 24
Halmashauri ya Wilaya ya Chato kwa hiki kinachoendelea sasa ni unyanyasaji wa wazi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba. Hii kunyatia kulipora soko la Magarini kwa mazao ya Ziwani na kutaka soko hilo liende Muganza ni mabavu ambayo hayana maana kwa sasa. Sifa za kulipora soko hilo hakuna kwa Chato na wanaojaribu hawafikirii hata uwiano wa vyanzo katika maeneo hayo mawili.
Halmashauri ya Wilaya Muleba wanazo kata 5 majini na kata hizo ndio mtaji wa kuendesha soko hilo la Magarini na kuikuza Bandari hiyo ya Magarini. Lakini Chato wao wanayo kata moja tu nayo ni Rubondo iliyoko kwenye hifadhi ambako hawatakiwi kuvuna chochote. Sasa jeuri ya kulazimisha soko kuwa Muganza wanaipata wapi?
Ipo haja ya kukataa hizi mambo waziwazi .hatuwezi kukubali huu uporaji wa Soko la kibiashara hasa kuporwa na watu ambao hawana sifa za kuwa na soko hilo. Muleba ina kila sababu kutokana na kuwa inazo kata tano majini na visiwa visivyo pungua 30.
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba wanatakiwa kuamka na kupambana vilivyo ili kuhakikisha walio na hila na Soko hilo la Magarini wanashindwa mapema sana na hila zao. Hili Soko la Magarini ndio chanzo kikubwa kwa sasa cha Halmashauri ya Wilaya ya Muleba. Chato watulie kwanza
Kata ambazo zinaibeba Muleba iendelee kuwa imara na kuendesha Bandari ya Magarini ni 5 nazo ni
1.Kata Ikuza
2.Kata Mazinga
3.Kata Bumbile
4.Kata Kerebe
5.Kata Goziba .