Chato: Rais Magufuli atoa salamu za maadhimisho ya miaka 56 ya Muungano. Asamehe wafungwa 3,973

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,813
4,546
Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania ametoa salamu za maadhimisho ya miaka 56 ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibari yanayotarajia kuadhimishwa siku ya kesho tarehe 26/04/ 2020.

Katika salamu hizo Mh. Rais amewataka Watanzania wote kutumia maadhimisho hayo kutafakari Muungano huo ambao uliasisiwa na viongozi wakuu Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pamoja na Hyati Sheikh Abeid Aman Karume pamoja na kumuomba Mungu dhidi ya janga la Corona.

Sambamba na hilo, Katika maadhimisho hayo Rais Magufuli ametoa msamaha kwa jumla ya wafungwa 3973 ambapo kati yao wafungwa 3717 wamesamehewa vifungo vyao wakati wengine 256 waliokuwa wakikabiliwa na adhabu ya kunyongwa wamebadilishiwa adhabu hiyo.

Mwisho, Rais ameendeleza kutoa msisitizo kwa Watanzania wote kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona kwa kuhakiksha kuwa wanaepuka mikusanyiko na safari zisizo za lazima.

1587818939465.png
 
Ndio kusema wanachama na wafuasi wa Chadema wanachukia sababu anafanya kazi akiwa Chato?
 
RAIS MAGUFULI ATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 3,973

Rais Dkt John Magufuli ametoa msamaha kwa jumla ya wafungwa 3,973 ambapo kati yake wafungwa 3,717 wamesamehewa vifungo vyao na wafungwa 256 waliokuwa wanakabiliwa na adhabu ya kunyongwa hadi kufa wamebadilishiwa adhabu hiyo.

Msamaha huo umetolewa ikiwa kesho Jumapili, April 26 ni maadhimisho ya miaka 56 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

FB_IMG_1587821029446.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani mimi huwa nakasirika nikisikia jitu linamtaja Mungu utafikri licha Mungu kweli! Bure kabisaaa!
 
Angeanza na wale wa ushahidi haujakamilika wako ndani zaidi ya 5yrs wakisubiria ushahidi wakakamilishe ushahidi kwanza.Waafrika twatendeana mabaya kuliko hata mkoloni aliyomtendea mwafrika yaani easy tu tunacheza na maisha ya wengine eti upelelezi haujakamilika and then ikifika wakati wa ibada tumejaa kwenye nyumba za ibada hii mizigo yote ya nn kuwafurahisha wanadamu nasi tuonekane misikitini au makanisani?
 
Back
Top Bottom