Chato na Ruangwa Inaweza Kuwa Mikoa Mipya?

Ilipokuwa kila kitu kinapelekwa Moshi ilikuwa sahihi tu,ila sasa wanapelekewa wengine imekuwa shida si ndio ........ Kila mtu kashtuka kwa sasa,kama kila kitu kilipelekwa kwa viongozi wa juu basi wacha na wao wapeleke makwao.
 
Hata hii mikoa inayojiona imeendelea ni kutokana na kutoa viongozi wengi toka uhuru, hivyo keki ya Taifa kuliwa upande.

Naamini Utawala wa Magufuli utajali sana ile mikoa maskini.
Umeelewa swali kweli ?
 
Ilipokuwa kila kitu kinapelekwa Moshi ilikuwa sahihi tu,ila sasa wanapelekewa wengine imekuwa shida si ndio ........ Kila mtu kashtuka kwa sasa,kama kila kitu kilipelekwa kwa viongozi wa juu basi wacha na wao wapeleke makwao.
Nyerere , Kawawa Mwinyi , Mkapa , Kikwete na Malecela walitokea Moshi ?
 
Nyerere , Kawawa Mwinyi , Mkapa , Kikwete na Malecela walitokea Moshi ?
Wakati wa Nyerere nchi haikuwa na pesa,Kawawa ni wa hapa hapa Dar,Mwinyi kwake ZNZ ile ni nchi,Mkapa ye mkewe ni wa huko Moshi,Kikwete wizara nyingi zilishikwa na wao.Una swali jingine bi dada ...??
 
Hii miradi ya Chato ni masurufu ya kuuza nyumba za serikali jamaa alipiga hela ndefu alikuwa anasubiri fursa tu afanye vitu vyake!
 
Ilipokuwa kila kitu kinapelekwa Moshi ilikuwa sahihi tu,ila sasa wanapelekewa wengine imekuwa shida si ndio ........ Kila mtu kashtuka kwa sasa,kama kila kitu kilipelekwa kwa viongozi wa juu basi wacha na wao wapeleke makwao.
Pelekeni na Iramba basi maana na sisi sio wa moshi. Ila ungeelewa point moja tu, nayo ni mgawanyo wa mapato ili kuijunga nchi na si kujenga sehemu alotoka kiongozi wa nchi. Je, miradi hii inapangwa na kuidhinishwa lini na wapi kama si mkuu mmoja anasema tu leta pesa huku.
 
We hakuna unachokielewa,mtoa mada anazungumzia UPENDELEO,sio kwamba sehemu zingine hakuna kinachofanyika. Sasa wewe unaongea kama vile sehemu zingine hakuna kinachofanyika.
 
Wewe mtuma post ni mbinafsi sana. Pia lazima ujue mikoa kama Kilimanjaro, Arusha na Kagera ilipata maendeleo muda mrefu sana. Mikoa hii ya kusini iliminywa sana kimaendeleo, tena kwa makusudi mazima. Ili kwa sababu waliopewa dhamana kipindi hicho mikoa yao haswa hii mitatu niliyoitaja

Kitu ambacho unapaswa kujua ni kwamba hii keki ya taifa ni kwa ajili ya watanzania wote wala sio kwa ajili mikoa hiya mitatu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Chato haiko kusini. Maendeleo yanategemea aina ya watu waliopo mahali penye kutaka maendeleo sio kaskazini wala kusini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ruangwa naombea Sana Iwe Mkoa, Katika wilaya ambazo zilisahaulika ni pamoja na Ruangwa, Ahsante Mh Majaliwa Mimi Siyo CCM Ila jitihada zako Katika Jimbo lako tunaziona.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ruangwa ikiwa Mkoa je itakua na wilaya zipi?Jimbo lilisahaulika ila si kwa kusema iwe Mkoa,sema waboreshe na kuongeza miundombinu.
Toka Nanganga to Ruangwa waweke lami,toka Nachingwea to Ruangwa waweke lami,waweke umeme wa uhakika(Mgao wa umeme Ruangwa ni pie),waweke maji ya uhakika.maana hawana maji wale,waboreshe miundombinu ya stendi,Kutafunguka tu,now si kuna machimbo ya madini kule Chunyu

May Allah bless Me and You
 
Back
Top Bottom