Chato: Mtoto Yohana Bahati (Albino) atekwa, akatwa viungo vya mwili, Azikwa kwa ulinzi mkali

Wanatoa pesa za nini wakati mauaji ya albino ni biashara ya CCM? Au wanatoa shukrani kwa kukamilisha mradi wao vizuri?
 
Naibu waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba ametoa kiasi cha shilingi milioni moja ili kumsaidia mama huyo alielazwa katika hospitali ya Bugando mkoani Mwanza baada ya kujeruhiwa wakati akijaribu kumnusura mwanae ambae hivi sasa ni marehemu.

Kwa taarifa tu,hata Magufuli akiwa kama mbunge wa eneo analotoka mama huyo,jana nae alitoa kiasi kama hicho kumsaidia mama huyo.

Chanzo: ITV

kwa nini wasinge tumia mamlaka walio nayo kuzuia mauaji ya albino,hivi kutoa pesa wakati janga lilishatokea ndo ishara ya kuwanibika?kinga ni bora kuliko tiba
 
wamefanya juhudi gani kuzuia mauaji...au wanasubiri kutoa rambirambi tu!!!
Mkuu kama ulikua mawazoni mwangu najiuliza mauaji haya ni mara ya kwanza kutokea. Kwa sasa huyu mama pesa si kitu kwake kuna mahala kuna makosa kama viongozi wanatakiwa kuliona hili. Hii nchi yenye intelijensia ya hali ya juu kweli tushindwe kukabiliana na hawa maharamia wanaotumia sijui boda boda. Kiukweli inauma sana hasa siku zinavyokwenda na mauaji yanavyozidi kana kwamba hakuna cha kuwafanya.

Pesa si jibu litakalomsaidia mhanga wa hii kitu tunahitaji uwajibikaji . Hawa wauaji wakimaliza albino ni wazi watahamia kwenye watu wa aina flani je tutakaa kimya mpaka lini. Iko wapi ile boldness ya kupambana na uovu si kila kitu siasa wawajibike wafanye kazi.
 
Mtatoa sana ila kura ni ukawa tu. Mtakoma. Nyie kama serikali hathtaji mtupe hela ila muwakamate wauaji. Sio mnatuua ili msaidie familia zetu. Pumbfuuu
 
Ina sound kama wanampongeza kiaina yaani naibu waziri wa fedha na usalama wa raia wapi na wapi, hana cheo chochote kinachohusu usalama, nilitegemea waziri wa mambo ya ndani ndiye ange sympathize na mapungufu hayo ya kiusalama wa raia.
Mwigulu amefanya jambo zuri kwa lengo maalumu la kisiasa.
 
Last edited by a moderator:
Wilaya ya Chato na Mkoa wa Geita kwa ujumla ni maeneo hatari sana kwa ndugu zetu Albino kuishi. Hii inatokana na takwimu zinazotolewa kila siku juu mauaji na mashambulizi yanayofanywa na idadi ya kesi zinazohusiana.

Bahati njema ni kuwa eneo hilo limepata mmoja wa wagombe Urais, tena advantage aliyo nayo ni kuwa anatoka chama kinachotawala na alikuwa Mbunge wa eneo hilo kwa miaka takribani 20.

Kinachoshangaza ni kuwa pamoja na yeye kuwakilisha wananchi wanaoishi kwa hofu ya maisha yao, bado kwa muda wote huo hajawahi kuonyesha msimamo wake wa kupiga vita kwa nguvu vitendo hivyo vilivyokuwa vimeweka makazi jimboni mwake. Ushiriki pekee ambao ameonyesha kushiriki kwa mujibu wa kumbukumbu zangu ni pale mtoto Yohana alipotekwa toka kwa mama yake na kwenda kuuwawa na mama kujeruhiwa vibaya.

Alichofanya mheshimiwa huyo Mbunge ni kuita wapiga picha wa TV na magazeti ili wamuonyeshe akitoa msaada wa shs millioni moja na vijimaneno vichache.

Kama mwakilishi wa wananchi kwa miaka 20 ameshindwa kuwasemea kuhusu maisha yao jee kweli katika nafasi kubwa kama hii anayo omba ataweza kweli kusimamia hatma ya maisha ya watu wengi zaidi? Anafaa kuaminiwa katika hilo au nako atakuwa anakuja kupiga picha za kutoa misaada bila utatuzi?

ImageUploadedByJamiiForums1436867875.997450.jpg
 
Subirini za mgongo tu kamwe hamtasalimika hata iweje magufuli atawanyoosha tu.
 
Subirini za mgongo tu kamwe hamtasalimika hata iweje magufuli atawanyoosha tu.

Atawanyoosha wakina nani? Sii ameshasema SITAWAANGUSHA ?? Kwa hiyo ni business as usual. Anyway back to topic, kwa nini mauaji ya Albino yalikuwa ndani ya eneo lake na hata siku moja hajaonekana akishirikiana na wakina Vick Ntetema kupiga vita?
 
Atawanyoosha wakina nani? Sii ameshasema SITAWAANGUSHA ?? Kwa hiyo ni business as usual. Anyway back to topic, kwa nini mauaji ya Albino yalikuwa ndani ya eneo lake na hata siku moja hajaonekana akishirikiana na wakina Vick Ntetema kupiga vita?

Hoja ngumu pana shaka magamba kama wataijibu kwa usahihi
 
Hoja ngumu pana shaka magamba kama wataijibu kwa usahihi

Mkuu ni jambo la kushangaza sana. Kama ule ukali aliokuwa anawafanyia wakandarasi angefanya hivyo kwa wananchi/ waganga wa jadi kule Chato wallah nakuambia mauaji ya Albino yangekoma na kuisha kabisa katika eneo lake.
Au mikwala ile kwa Wakandarasi ilikuwa na namna? Maana isije kuwa kama yale ya Mrema "nifate Kiraracha haraka"
 
Back
Top Bottom