Chato kuna nini na ufaulu wa NECTA? Takwimu zinaonesha wanaongoza darasa la nne, Saba na kidato cha 4 wote wanatoka Chato

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Mwaka 2018 Mwanafunzi Aliyeongoza Kitaifa Kwenye Matokeo Ya Darasa La 7 Alitokea Chato, Pia Mwanafunzi Aliyeongoza Darasa La 4 Kitaifa Alitokea Chato, Mwaka Huu Mvulana Wa Kwanza Kitaifa Darasa La Saba Katokea Chato Tena. Coincidence? Wamepanga?Au NECTA Nao Wanaunga Mkono Juhudi?

qw.PNG
 
Matokeo yao yanatosheshwa! Na kwa vile NECTA bado wanapenda kazi zao basi wanaunga mkono juhudi....Mwakani au 2025 rais akitoka Tanga Basi watoto wa Bumbuli watakuwa wanatuongoza inshaallah
 
Alipangiwa special school?
Hivi mpaka uwe wa kwanza kitaifa wanachukua vigezo gani? Maana mimi mwanangu wa kike mwaka jana 2018 kapata A masomo yote yaani hakuna cha B wala nini..lakini hata kwenye mkoa sijasikia hizo habari au A clean sheets zitakuwa zipo nyingi?
 
Mbona naskiaga wahaya ndiyo wenye akili Afrika nzima au Chato ndiyo kwa wahaya?
 
Huu ni uboya Sana na unakuta jitu mtoto ana ufaulu wa kawaida linaenda pale school mfano shule yeyote ya kipaji Kama tabora girls anafanya yake mtoto anasoma pale
Huyu ndio mwanangu wa mwisho kusoma Tanzania *****...upumbavu ndo nilishakataaga kitambo sana
 
Back
Top Bottom