Chato inafaa kujengwa Ikulu kubwa baada ya Dar es Salaam

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
Chato ni eneo zuri ki ulinzi kwa kiongozi ikibidi zaidi ya Dar es salaam na Dodoma

1. Kiusalama imezungukwa na ziwa Lina visiwa zaidi ya 60; Ni rahisi kuondoshwa kupitia njia ya Maji

2. Ulinzi : Kuna vikosi vikubwa vinne . Biharamulo,Ngara, Rwamishenye,Kaboya na Kwa Mbali Mwanza . Kiulinzi kiongozi yupo salama.

3. Kuna Poli nene lenye Giza na kubwa . Linenda Uganda ,Rwanda,Kigoma mpk Katavi Lina mbuga za Burigi Chato,Rumanyika ,Kimisi ,Akagera na Rwenzori.

4. Chato ikifingwa ni rahisi kupitia Biharamulo na kuendelea bila kuathiri usafirishaji.

5. Ni Katikati ya nchi 5. Rwanda km 179 km ,Burundi 200km ,Uganda 300km. Kenya 60 Km. South Sudan ,Congo. . Kuendesha mikutano ya Viongozi wa EAC ni Rahisi kuliko Sehemu yoyote.

6 Robo tatu ya watanzania milioni 35 wanapakana na Chato . Mikoa ya Mwanza,Geita,Musoma,Simiyu,Shinyanga,Kigoma, Tabora na Kwa mbali Arusha na Singida

7. Kuna mandhari nzuri ya Kiongozi Mkubwa kupumzika mf. Kuvua Samaki ziwani,Kuwinda,Kutembelea mbuga ,kutembelea visiwa vya Rubondo na saa nane nk anapoitaji mapumziko

8 Kiongozi (Rais) ana muingiliano wa Wageni km yupo busy . Na hakuna pollution. Km majiji ya Dsm na Dodoma.

9. Kiongozi amezungukwa na viwanja vya ndege vikubwa vitatu. Bukoba, Chato na Mwanza. Na viwanja vikubwa vya jeshi viwili Biharamulo na Ngara

Ni wakati umefika tuwe na Ikulu kubwa nne nchini na Chato ikiwemo
 
Hii nchi basi ikifika miaka mia tangu uhuru wake tutakuwa na ikulu nyingi sana. Sioni kama kuna umuhimu wa kuwa na ikulu nyingi kama kipaumbele.

Kipaumbele kwa sasa angalau iwe viwanda. Tutanue zaidi kilimo, watu wasaidiwe walime kisasa, mali ghafi zipatikane ziuzwe viwandani tukuze uchumi wetu.

Haya ndo mawazo natamani watu waje nayo hapa. Hii ndo namna ya kuwasaidia viongozi waliopo madarakani kukuuza uchumi wetu.

Taifa letu bado ni changa sana kuwaza mambo ya luxury namna hiyo.
 
Mwambieni akirudi tu atakiona kwani covid 19 tumemfuga tayari yumo ndani ya vifuko vifuko vya plastic tunamlisha unga uliochanganywa na maji betri ya bajaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukipenda kichekesho hiki toka Lumumba,
Bonyeza #slow×2 Tz# kitawezeshwa kwenye masikio yako ,Ahsante
 
Baada ya miaka kumi akaja Raisi kutoka jimbo la Luangwa huko Lindi ,akajenga Ikulu Luangwa
Miaka 20 ijayo akaja Rais kutoka Pemba akajenga huko Ikulu.
Miaka 30 ijayo akaja Rais kuoka Kalenga Iringa akajenga Ikulu Kalenga.
Miaka 40 ijayo akaja Rais kutoka Hai Kilimanjaro akajenga Ikulu Hai.
Tutunge sheria iingizwe kwenye katiba ya nchi yetu kuwa Dar-es-salaam ni mji mkuu wa serikali ya Muungano.Haitabadirishwa na mtu yeyote hadi dunia ifutike.
Mikoa ya bara ipunguzwe hadi ya mwaka 1985.
 
naaona idadi ya wachawi Tanzania inaongezeka na huyu atakuwa ni mwenyekiti wao. Kwa akili za kawaida huwezi kuwaza kwa kutumia kijambio
 
Back
Top Bottom