Chato imekuzwa na kuwa Chatu, sasa inataka kuimeza Kagera na Geita?

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,127
35,138
Mwanzoni (wakati Magufuli akiwa bado hai) ilikuwa kama tetesi lakini sasa kila kitu kiko wazi kuwa Chato imejipanga kuhakikisha inakuwa mkoa, tena mkoa mkuu na imara kwa gharama za kuimega Kagera na Geita.

Kwa sasa ni vuta nikuvute, kila upande unavutia kwake, wezee wa mkoa wa Kagera wakisema; hawako tayari kuona historia, tamaduni na uchumi wa mkoa wa Kagera ukipotezwa kimakusudi chini ya mpango wa kuumega mkoa wa Kagera ili kuundwa mkoa mpya wa Chato. Na wakati huo huo, viongozi wa wilaya ya Chato wakijiapiza kuwa iwe isiwe, mkoa wa Chato lazima uundwe kwa gharama ya kumega wilaya muhimu za mkoa wa Kagera, Geita na Kigoma.

Chini ya sera za CCM za siku zote za kuwagawa watu kimaeneo na kitamaduni ili iwe rahisi kuwatawala (chini ya mwamvuli wa kuunda mikoa na wilaya mpya), mpango huu kwa sasa huenda ukaleta maafa, chuki na visasi visivyokwisha kwa karne kadhaa ikiwa busara haitatumika.
 
Hivi mikoa au wilaya inagawanywa kwa kufuata ukabila na utamaduni wa eneo husika..Yaani kama eneo linawanyarwada zaidi basi i aundwa wilaya ya kufuata utamaduni huo?

Mimi nimeshauri kwa kuwa Chato kuwa makao makuu ya mkoa ndo shida basi mkoa mpya uwe Nyakanazi na wilaya zake za chato..Biharamulo..Ngara..na Nyakanazi yenyewe..Naamini hili li akubalika kwani kwa kufabya hivi tutaukwa tu.ewakomesha watu wa chato
 
kusema ukweli mimi naona ni upuuzi kusema eti mkoa fulani usimegwe kwani ukimegwa unapelekwa Burundi ? si inabaki kuwa Tanzania
lakini pia siungi wala kupinga hoja ya chato kuwa mkoa, maoni yangu katika kutawala hii Tanzania ni kwamba,wakuu wa Mikoa ndio wawe wabunge hii itaokoa pesa sana kuliko kuwa na wabunge na wakuu wa mikoa
 
We mzanzibar ya bara yanakuhusu nn,kajadilini ya kwenu huko visiwani ambapo mkoa kwenu haufiki hata ukubwa wa kata ya buza
 
Mwanzoni (wakati Magufuli akiwa bado hai) ilikuwa kama tetesi lakini sasa kila kitu kiko wazi kuwa Chato imejipanga kuhakikisha inakuwa mkoa, tena mkoa mkuu na imara kwa gharama za kuimega Kagera na Geita...
Hiyo chato itahamia uganda au itabaki tanzania?
 
wezee wa mkoa wa Kagera wakisema; hawako tayari kuona historia, tamaduni na uchumi wa mkoa wa Kagera ukipotezwa kimakusudi
Kagera itamegwa tu. Kwa mujibu wa katiba hii rais ni kama Mungu. Akiamua atawaua wahaya wote na asishitakiwe popote.
 
Chatu :D:D:D😂

Mkuu una akili kubwa SANA.

Umenipa burudani Jpili ya leo. Nimesahau mpaka madeni yangu ya fedha.

Everyday is Saturday................................:cool:
 
Mwanzoni (wakati Magufuli akiwa bado hai) ilikuwa kama tetesi lakini sasa kila kitu kiko wazi kuwa Chato imejipanga kuhakikisha inakuwa mkoa, tena mkoa mkuu na imara kwa gharama za kuimega Kagera na Geita...
Kwahiyo mawazo yako ni kuwa soon chatu ataanza kumeza watu , au shida yangu ni stress zangu na njaa njaa zangu tuuu🤔.
 
Back
Top Bottom