Chato, Geita: RC awaweka ndani masaa 48 Afisa Elimu Wilaya na Mkuu wa shule ya Zakia Meghji kwa kukiuka maagizo

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,927
geita.jpg


Mheshimiwa RC baada ya kumaliza shughuli katika Kituo cha Afya Mganza, ametembelea Mradi wa pili wa Ujenzi wa Bweni la wanafunzi Shule ya Sekondari Zakia Meghji ambalo linajengwa kwa ufadhili wa pesa za P4R kwa gharama ya Tsh. 75,000,000.00 litakalotakiwa ku-accommodate wanafunzi 80 kwa mujibu Melekezo ya Wizara yenye dhamana juu ya utaratibu wa fedha hizo.

Itakumbukwa kuwa tarehe 31 Oktoba, 2017 Mhe. RC alipotembelea Ujenzi wa Bweni hilo alibaini ukiukwaji wa taratibu za fedha hizo za P4R, ambapo ujenzi wa Bweni uliofanyika katika Shule hiyo ya Zakia Meghji ulijengwa kwa kuweza kutosheleza wanafunzi 56 badala ya wanafunzi 80, RC alichukua hatua ya kuwaelimisha viongozi na watendaji wa Shule, Halmashauri na Wilaya kwa ujumla juu ya matumizi ya fedha hizo yanavyotakiwa kuzingatiwa, na alidiriki kuthibisha maelekezo hayo kwa kuwasiliana na Wizara husika na wote kwa pamoja waliokuwepo mahali hapo walijiridhisha.

Hivyo, RC aliagiza ujenzi huo usimamishwe na yafanyike marekebisho ya kuonngeza ukubwa wa Bweni hilo kwa maana ya kutosheleza idadi ya wanafunzi 80 badala ya wanafunzi 56 kama walivyojenga sasa.

(Ikumbukwe kuwa wakati huo Bweni hilo lilikuwa halijapauliwa bado). RC alielekeza Viongozi wenye dhamana na maslahi ya Mradi huo watekeleze maagizo hayo na kusimamia ipasavyo Mradi huo na kuhakikisha thamani ya fedha hiyo inaonekana.

Leo (jana) Mhe. RC alipotembelea Mahali hapo amekuta ukiukwaji wa Maelekezo aliyoyatoa hivyo amechukua hatua za kisheria kwa kumuagiza Kaimu OCD Chato awapeleke Polisi Afisa Elimu Sekondari Chato pamoja na Mkuu wa Shule ya Sekondari Zakia Meghji kwa muda wa masaa 48 kwa kukiuka Maagizo halali yaliyotolewa na Mamlaka.

Aidha, Mhe. RC amemuagiza DED achukue hatua za kinidhamu kwa watendaji hao kwa mujibu wa taratibu za Utumishi wa Umma.

CHANZO: Geita Info
 
Kuna uhusiano gani wa kuwekwa kizuizini kwa watumishi kwa masaa 48 na kukiuka amri ya RC?
 
Watu walijenga mahostel chuo kikuu dar kwa pesa ndogo mkuu tusubiri TBA wajenga ilo jengo kwa hiyo fedha
Pale yalitumika mabilioni mengi sana ila mzee wa mihemko mara ya kwanza alijinadi kwamba atatumia pesa ndogo kwa kuwaaminisha wananchi kuwa yeye ni mbana matumizi.
Watu kitambo tu walishazinaa profoma halisi na wakaona gharama zote
 
Unaweza kuwa mchawi bila kupenda, ningelikuwa mimi nikitoka lupango namuendea kwa kigagula anabeba mimba bila kupenda, nchi hii ilipofikia bora kuwa machinga kuliko mtumishi wa umma, sipendi dharau.
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom