Chato, Geita: Rais Magufuli afungua jengo la Mahakama ya Wilaya na kuweka jiwe la msingi jengo la Zimamoto

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,891
141,824
leo Jumatano Desemba 18, 2019 Rais wa Tanzania, John Magufuli amehudhuria hafla ya uzinduzi wa jengo la Mahakama ya Wilaya ya Chato na uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa jengo la Zimamoto na Uokoaji la Wilaya ya Chato mkoani Geita.

Haya ni baadhi ya yaliojiri kwa ufupi.

Prof. Ibrahim Juma, Jaji Mkuu wa Tanzania amesema:

“Ujenzi na ukarabati wa mahakama mbalimbali nchini utakuwa na maana sana na utaleta tija iwapo watumishi wa mahakama kwa kada zote wataendelea kuzingatia bidii weledi na maadili wakati wa kuwahudumia wananchi”


Rais John Magufuli amesema:

“Kabla ya ujenzi wa mahakama hii wananchi wa Chato walilazimika kwenda hadi Biharamulo kufuata huduma za kimahakama. Hili lilikuwa gumu sana kwakuwa Mahakama ya Wilaya ilikuwa Biharamulo, gereza nalo lilikuwa Biharamulo.”

“Nampongeza Jaji Mkuu kwa ujenzi na marekebisho ya Mahakama mbalimbali nchini. Mahakama zilizojengwa katika kipindi cha Jaji Mkuu Ibrahim Juma, mahakama zimejengwa kwa viwango vizuri.”

Kuhusu kuongeza idadi ya watendaji wa Mahakama, Rais amesema:

“Napenda kuhakikishia Mahakama kuwa tutaendelea kushughulikia suala la upungufu wa watendaji wa mahakama kwa kadiri itakavyowezekana”

“…Jaji Mkuu utakumbuka katika kipindi cha miaka mine iliyopita, tumeteua majaji wa Mahakama ya Rufaa 11 na Majaji wa Mahakama Kuu 39 na hivyo jumla ya majaji kuwa 50”

“…serikali imeajiri mahakimu 396 na hivyo kuongeza idadi ya mahakimu kutoka 700 mwaka 2015 hadi kufikia mahakimu 938. Najua bado hawajatosha. Nakuahidi Mh. Jaji Mkuu, hili suala la watumishi wa mahakama tutalishughulikia kikamilifu.”

Wito kwa watumishi wa Mahakama

“…endeleeni kuchapa kazi kwa kuzingatia weledi na iuadilifu. Jiepusheni na vitendo vya rushwa.”

“…ujenzi wa mahakama hii na nyingine hautakuwa na maana endapo watumishi wataendeleza vitendo vya rushwa”
“Mh Jaji Mkuu, najua jitihada unazofanya kuwashuhghulikia watumishi wanaojihusisha na rushwa, endelea na jitihada za kuwachukulia hatua”

Ushirikiano wa vyombo vya haki

“Najua changamoto munazokumbana nazo. Mambo mengine hayasababishwi na majaji au mahakimu, yanasababishwa na vyombo vingine. Unakuta kesi inatakiwa kupelekwa mahakamani na haipelekwi haraka. Unakuta kesi inatakiwa kufanyiwa upelelezi lakini Jeshi la Polisi halipelelezi haraka.”

“…vyombo vyote vya kutoa haki lazima vishirikiane kwa pamoja kuhakikisha haki za Watanzania zinapatikana”

“...watu wanakaa mahabusu bila kupelekwa mahakamani, na wengine wana kesi ndogo tu.”

Pia Rais amesema kuwa katika mikoa mitatu ambayo Wizara ya Sheria imetembelea, tayari wamesamehe na kuwatoa watu 601, ambapo DPP Biswalo amethibitisha mbele ya Rais na kuongeza kuwa “Jana nimewafutia na kuwasamehe mahabusu 150 katika Gereza la Geita”, hivyo idadi ya waliosamehewa kufikia 751.

Mahabusu na wafungwa katika magereza ya Tanzania

Kwa mujibu wa Phaustine Martin Kasike, Kamishna Jenerali wa Magereza
  • Wamebaki wafungwa 12,000 kutoka 17,000, ukitoa zaidi ya 5,000 waliosamehewa na Rais mwaka huu.
  • Mahabusu wapo 17,000

Rais apongeza Jeshi la Zimamoto


“Jeshi la Zimamoto ni moja ya taasisi zinazoongoza kwa kulaumiwa zaidi, ingawa wakati mwingine linalaumiwa kimakosa. Unaweza kukuta jeshi linalaumiwa lakini kumbe taarifa zimechelewa kuwafikia au ni kwasababu ya ugumu wa kufika kwenye maeneo husika kutokana na watu kujenga kiholela”

“..nalipongeza Jeshi kwa kukusanya mapato. Katika kipindi cha miaka mine Jeshi limekusanya zaidi ya bilioni 73.”

“…serikali itaendelea kuwaonga mkono ili kuboresha utendaji”


Vyeo kwa maofisa na askari 683


Serikali imawapandisha vyeo maofisa na askari 683 ikiwa ni pamoja na:
  • Makoplo 109
  • Masajini 128
  • Stesheni Sajini 134
  • Wakaguzi Wasaidizi 151
  • Wakaguzi 95
  • Warakibu Wasaidizi 61
  • Mrakibu 1
  • Warakibu Waandamizi 2
  • Makamishna Wasaidizi 2

Wito kwa Jeshi la Zimamoto

“…endeleeni kuchapa kazi ili malalamiko ya wananchi dhidi yenu yapungue au kuisha kabisa.”

“Kuna matatizo yanayo sababishwa na nyinyi wenyewe. Unaenda kuzima moto, unakuta gari halina maji. Sasa kwanini ulienda? Si ungepaki tu?”


 
Rusha picha ya jengo letu hilo, japo nimeona kule twita, lakini najisikia kuona tena kwenye thread yako
 
Ujenzi wa mahakama ya Chato unaweza kuwa a blessing in disguise.

Akimaliza muda na kwenda kuishi Chato anaweza kushitakiwa baada kuondolewa kinga kwa ma milioni ya madudu aliyofanya akiwa Ikulu.

Anaweza kujikuta ndani ya mahakama hiyo ya Chato.
 
Tuache kwanza, tupo Mlimani city sasa hivi kwenye mambo ya kitaifa.
 
Hongera JPM, wanachato hawatasahau mchango wako ni neema kwa kwenda mbele. Hotel zote Chato zimejaa,watoa huduma bar migahawa, vituo mafuta kote neema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Mhe. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULU inaendelea na utekelezaji wa mradi mkubwa wa ujenzi wa majengo ya kisasa ya mahakama za wilaya na kanda katika maeneo ya Singida, Ruangwa, Kasulu,Bukombe, Musoma na Kigoma.

Utekelezaji wa mradi huo ni ishara tosha kuwa Mhe Rais ana nia ya dhati ya kuhakikisha utoaji haki za wanyonge zinapatikana kwa wakati pamoja na kusogeza karibu huduma huyo kwa wananchi.
 
Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Mhe. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULU inaendelea na utekelezaji wa mradi mkubwa wa ujenzi wa majengo ya kisasa ya mahakama za wilaya na kanda katika maeneo ya Singida, Ruangwa, Kasulu,Bukombe, Musoma na Kigoma.

Utekelezaji wa mradi huo ni ishara tosha kuwa Mhe Rais ana nia ya dhati ya kuhakikisha utoaji haki za wanyonge zinapatikana kwa wakati pamoja na kusogeza karibu huduma huyo kwa wananchi.
Kwenye ujenzi kuna madili. Ujenzi na haki vitu viwili tofauti. Tuanze na mchakato wa kupata mkandarasi je sheria za tender zilifuatwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom