Chato: Chatu aliyezua gumzo aondolewa na kupelekwa hifadhini. Wananchi waja juu

Hawa wajinga wajinga hawakawii kupeleka hata binadamu ili kutoa kafara. Jamaa wa kule wanaendekeza sana mambo ya giza
 
Nasikia supu yake ni zaidi ya supu ya pweza.
1568212074656.png
1568212093550.png
 
Mi natamani hilo lijoka lingeonyesha advataizi moja tu,animezee kama watu watatu kwa mpigo,tuone kama wangeendelea kumsogelea

Naona watanzania bado somo la uwezo wa kutambua hatari bado halijatuingia vizuri vichwani mwetu
Umejua kunichekesha. Niliwaza hill, lkn niliwaza angeng'twa mtu ingekuwaje?
 
Serikali imewatafuta wataalanu wa miujiza ya kiasili.kumbeba .Wale mnaobeza Manabii Wakristo watenda miujiza pateni somo.Serikali inahitaji pia watenda miujiza.Mnaopiga Vita Manabii wa miujiza na msioamini mambo ya miujiza oneni Hilo.Wachawi wametumika kubeba chatu kumpeleka pori la serikali.Vinginevyo ngoma ilikuwa nzito
 
Naona maliasili wamemchukua na kumpelekea Magu apate baraka kwanza. Hii nauhakika itafanyika kisirisiri. Huyu jmaa kma alienda kwa babu kunywa kikombe, sasa kwa nyoka ataachaje?
 
Nyoka anakuwa vipi baraka waache ujinga hao.

Baraka ipo ndani ya matendo yao wenyewe, waache kuua vikongwe, Albino kwa imani za kishirikina, Wananchi wapendane...hizo ndio baraka.
 
Hahaaa sinema haziishi toka chato yani waje shambani kwangu simanjiro chatu wanaonekana kila siku.yani jiwe na wafuasi wake wanatuona watz wajinga...iko siku mtasikia mungu kaonekana chato anakunywa fanta orange
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini Tanzania (Tawa) imemchukua nyoka mkubwa aina ya chatu aliyeonekana katika kijiji cha Kasala kata ya Makurugusi wilayani Chato mkoani Geita.

Kwa mujibu wa ofisa habari wa halmashauri ya wilaya ya Chato, Richard Bagolele amesema nyoka huyo anapelekwa pori la akiba la Kigosi wilayani Kahama kuhifadhiwa.

Nyoka huyo anayeanza kuonekana siku saba zilizopita aligeuka kivutio kwa wananchi waliodai kuwa ni baraka, wengi kushinda porini wakimtazama huku wakiwa na mbuzi, maji na unga wakiamini endapo nyoka atakula watapata baraka ya mvua, kuongezeka kwa mavuno.

Akizungumza leo Jumatano Septemba 11, 2019 amesema Tawa iliwatafuta wataalam wa nyoka kutoka makumbusho ya Bujora waliofanikisha kumchukua nyoka huyo aliyekuwa katika kichuguu akiwa amelalia mayai 20.

Mmoja wa Wananchi wa kijiji hicho, Philipo Maduhu amesema nyoka huyo ni baraka kwao na halmashauri haikupaswa kumuondoa.

View attachment 1204482
 
Ndiyo maana wanaitwa WANYONGE.
Serikali imeleta mgogoro wa kidini bure ingewaacha wananchi wamalize ibada yao.Huyo nyoka ndie Mungu wao wamewaonea kuwakatizia ibada yao.Au wamewaonea sababu dini yao ya kuabudu nyoka haijasajiliwa? Mambo ya kuabudu yako nje ya serikali sababu serikali haina dini serikali hata siku Moja haisajili dini na Wala nguvu hiyo haina kuanzia kwenye katiba.Inachosajili Ni NGO zile zinazotaka zipewe hati kwa ajili ya mambo Kama kufungua akaunti benki,kuanzisha miradi kama Shule,hospitali na biashara mbalimbali zinazohitaji leseni ya biashara Kama Vituo vya radio,television nk,kupata fedha na misaada kwa wafadhili wa nje nk.Catholic lazima isajiliwe sababu ina miradi na biashara kibao .Hata Bila waziri kuwafuata wangeenda .Kuna NGO za namna hiyo hata hawahitaji waziri awaombe wanaenda wenyewe sababu Bila kujisajili mambo yao hayawezi kwenda sababu wao Kazi yao kubwa Sio kusali tu Wana makando kando mengi.Sasa wako ambao hawahitaji hayo wao lengo lao kuabudu tu Kama hao waabudu nyoka hao Huwezi sajili labda watake wenyewe kwa hiari yao.Makanisa mengi Yana Mashule,miradi,mahospitali nk wawe sabato,waislamu,waanglikana,walutheri nk na wanaenda kusajili kwa hiari Sio sababu waziri kasema au Sheria inataka.Wanaenda kutafuta hati ya kuwawezesha mambo yao hayo Mengine yaende.sababu wakienda kutafuta leseni ya biashara wataulizwa hati ya usajili nk.Serikali ndio maana Ina Sheria za kusajili NGO Sio dini!!!! Ndio maana napinga kitendo Cha waziri kumtoa nabii mahela akiwa kanisani kwa kisingizio Cha kusali Bila kusajiliwa.Mambo ya kuabudu yako nje ya mamlaka ya serikali na hayahitaji kusajiliwa.Mfano hao waabudu nyoka wako ibadani hawatakiwi kubughudhiwa na yeyote kuwa wamesajiliwa au la awe polisi au waziri Lugora.Ila wakiwa na malengo mengine labda kuanzisha Shule nk Wala hata waziri Hana haja hata ya kuwataka wajisajili wataenda wenyewe kwa hiari sababu wakienda wizara ya elimu kutaka kusajili Shule wataambiwa wakalete hati yao ya kusajiliwa Kama NGO.Waziri anatumia nguvu kubwa kwa kitu kisichohitaji nguvu nyingi.Kosa la kusema Hilo kanisa la huyo nabii halijasajiliwa aliondoe haraka serikali haisajili makanisa inasajili NGO.Ila Kama liko kosa lingine labda Lakini Hilo la kanisa kutosajiliwa Sio kweli.Hilo Ni issue ya kuabudu haina uhusiano na registration.Na waziri kamkuta nabii akiwa kwenye majukumu Yake ya kiibada ambayo Ni haki Yake kikatiba .Kama liko kosa lingine sawa ila Sio Hilo la kusema anaendesha ibada Bila kanisa lake kusajiliwa.Hilo No no no no.Ndio maana Sina shida na hao waabudu nyoka wako peacefully kwenye ibada yao hawahitaji mtu wa kuhoji usajili wao hawauhitaji Serikali imewaonea kuwachukulia Mungu wao nyoka waliyekuwa wakimsubiri apokee sadaka zao za mbuzi nk.Serikali haijawatendea Haki waumini wa huyo nyoka.Kazi ya serikali Sio kukatiza ibada za watu haina dini
 
Bora wangemnywa supu ona sasa kasepa huyooo wanabakia kulia lia. Kuna jamaa alitaka kuwapa shekeri wakagoma. Wamebaki na umaskini wao.
 
Bora wangemnywa supu ona sasa kasepa huyooo wanabakia kulia lia. Kuna jamaa alitaka kuwapa shekeri wakagoma. Wamebaki na umaskini wao.
Sio kasepa kabebwa kwa nguvu na Askari.Amenyimwa haki Yake ya kula sadaka alizopewa na waumini wake.Watetezi wa wanyama mko wapi?
Mnyama Hana haki ya kuabudiwa Kama mungu? Wanasheriaa mko wapi kumtetea huyo mungu nyoka ambaye kabebwa kanisani mbele ya sadaka na mbele ya waumini wake waliokuwa ibadani usiku na mchana kumsubiri apokee sadaka zao? Waumini wake wameingiliwa Uhuru wao wa kuabudu waliopewa na katiba kwa nguvu kwa kuporwa mungu wao tena kipindi Cha sadaka ibadani
 
Back
Top Bottom