Chato: Chatu aliyezua gumzo aondolewa na kupelekwa hifadhini. Wananchi waja juu

Hivi punde

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Messages
2,064
Points
2,000
Hivi punde

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined Apr 1, 2017
2,064 2,000
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini Tanzania (Tawa) imemchukua nyoka mkubwa aina ya chatu aliyeonekana katika kijiji cha Kasala kata ya Makurugusi wilayani Chato mkoani Geita.

Kwa mujibu wa ofisa habari wa halmashauri ya wilaya ya Chato, Richard Bagolele amesema nyoka huyo anapelekwa pori la akiba la Kigosi wilayani Kahama kuhifadhiwa.

Nyoka huyo anayeanza kuonekana siku saba zilizopita aligeuka kivutio kwa wananchi waliodai kuwa ni baraka, wengi kushinda porini wakimtazama huku wakiwa na mbuzi, maji na unga wakiamini endapo nyoka atakula watapata baraka ya mvua, kuongezeka kwa mavuno.

Akizungumza leo Jumatano Septemba 11, 2019 amesema Tawa iliwatafuta wataalam wa nyoka kutoka makumbusho ya Bujora waliofanikisha kumchukua nyoka huyo aliyekuwa katika kichuguu akiwa amelalia mayai 20.

Mmoja wa Wananchi wa kijiji hicho, Philipo Maduhu amesema nyoka huyo ni baraka kwao na halmashauri haikupaswa kumuondoa.

pic-2bnyoka-gif.1204482
 
carcinoma

carcinoma

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2017
Messages
3,914
Points
2,000
carcinoma

carcinoma

JF-Expert Member
Joined Mar 5, 2017
3,914 2,000
Dah hivi huu ujinga watu wanautoa wapi??
Tangu lini chatu akawa baraka?
Hata nyoka mwenyewe atakuwa anawashangaa watu kinoma kwa ujinga wao
 
Mhadzabe

Mhadzabe

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2009
Messages
2,622
Points
2,000
Mhadzabe

Mhadzabe

JF-Expert Member
Joined May 20, 2009
2,622 2,000
Hizo ndio tamaduni zetu za asili.

Tusijione wakisasa kwa sababu tunatumia simu mpapaso na tunaishi mjini.

Wengine mnaponda kuhusu hao waabudu nyoka, ila kila siku haziishi Mkuranga na Bagamoyo au Pemba kufata uchawi wa kufanikiwa au kulinda mali. Mnasahau mkiwa huko mnaongea na lichatu kama hili!🤣🤣🤣
 
Daudi Mchambuzi

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Messages
41,812
Points
2,000
Daudi Mchambuzi

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2010
41,812 2,000
Haya wampelekee hayo mandazi huko Burigi
 
sagaciR

sagaciR

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2017
Messages
628
Points
1,000
sagaciR

sagaciR

JF-Expert Member
Joined Jun 17, 2017
628 1,000
Ila kanda ya huku ni wapenda ushirikina. Hivyo hapo tayari wameamini kitu kuhusu huyo nyoka!!
"Imani na uchawi" ni vitu vinavyofanana??. Au unachuki tu na kanda ya huko, so whatever happen which is against you is wrong, even if you are the mischief.
 
cocochanel

cocochanel

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2007
Messages
24,190
Points
2,000
cocochanel

cocochanel

JF-Expert Member
Joined Oct 6, 2007
24,190 2,000
Hiyo ya kulalamika kuondolewa.. imeniacha mataa!!!!
Ila hayo ya baraka kweli yanatokea au?
 
Papi Chulo

Papi Chulo

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Messages
2,849
Points
2,000
Papi Chulo

Papi Chulo

JF-Expert Member
Joined Jun 8, 2018
2,849 2,000
Mi natamani hilo lijoka lingeonyesha advataizi moja tu,animezee kama watu watatu kwa mpigo,tuone kama wangeendelea kumsogelea 🐍🐍

Naona watanzania bado somo la uwezo wa kutambua hatari bado halijatuingia vizuri vichwani mwetu
 
T

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2019
Messages
1,780
Points
2,000
T

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2019
1,780 2,000
Nadhani kuna kaugumu fulani hivi ka kuwatenganisha baadhi ya ndugu zetu wa kanda ya ziwa na masuala ya ushirikina, imani potofu na USHAMBA!

Nilikuwa Ifakara siku chache zilizopita, nilishangaa sana na sikufurahishwa kabisa na namna wenyeji wa kule wanavyowachukulia hawa ndugu zetu wanaolima na kufuga! Wanawachukulia kama washamba kupitiliza! Sijajua ni kwa nini!
Kuna umuhimu wa kuwahisha ujenzi wa zile taa za solar aisee. Huu ni mtazamo tu lakini.
 

Forum statistics

Threads 1,334,886
Members 512,157
Posts 32,489,890
Top