Chato: Baraza la Madiwani lawasimamisha kazi Watumishi 15 kwa ubadhirifu wa Tsh bilioni 3.6

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,504
2,000
Baraza la madiwani halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita limewasimamisha kazi watumishi 15 wa idara mbalimbali kutokana na ubadhirifu wa Sh3.9 bilioni za miradi ya maendeleo.

Miongoni mwa watumishi hao sita ni wa idara ya manunuzi ,wengine sita ni watendaji wa vijiji, wauguzi wawili na ofisa kilimo wa kata ya Inchwankima aliyeondoka kwenye kituo cha kazi kwa miezi mitatu bila taarifa huku akiwa ametoroka na Sh300,000 za wananchi.

Uamuzi huo umetangazwa leo Alhamisi Februari 18, 2021 mwenyekiti wa baraza la madiwani wa halmashauri hiyo, Batholomeo Manunga aliyebainisha kuwa wamemtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuunda tume ya uchunguzi itakayohusisha baadhi ya madiwani na viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo.

Ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuanza kuichunguza miradi yote iliyotengewa fedha lakini haijatekelezwa, kumtaka mkurugenzi kuwachukulia hatua zaidi watendaji wa vijiji ambao hawajasoma taarifa za mapato na matumizi tangu mwaka 2018.

Baraza hilo lililofanyika jana Jumatano Februari 17, 2021 lilianza na vuta nikuvute baada ya madiwani kugoma kuendelea na kikao kutokana na taarifa za miradi inayotekelezwa kutowekwa.

Mkuu wa Wilaya ya Chato, Charles Kabeho amesema hatamvumilia mtumishi yeyote anayerudisha nyuma maendeleo ya wilaya hiyo na kusema tayari ameanza kwa kuwakamata baadhi ya watumishi na kuwafikisha kwenye vyombo vya uchunguzi kwa hatua zaidi .

Chanzo: Mwananchi
 

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
2,177
2,000

Tsh bilioni 3.6 kuibiwa mkurugenzi wa Halmashauri ya chato alikuwa wapi muda wote huo,? Hii ni sawa na mke kuiba fedha za mume wake .au mume kuiba fedha za mke wake.​

 

marxlups

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
14,784
2,000
Miongoni mwa watumishi hao sita ni wa idara ya manunuzi ,wengine sita ni watendaji wa vijiji, wauguzi wawili na ofisa kilimo wa kata ya Inchwankima aliyeondoka kwenye kituo cha kazi kwa miezi mitatu bila taarifa huku akiwa ametoroka na Sh300,000 za wananchi.
Unamsimamisha mtu kazi wakati alishakuibia akaondoka haya ni matumizi mabaya ya lugha
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom