Chatanda awatimua waandishi wahabari awatisha kuwapiga bastola | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chatanda awatimua waandishi wahabari awatisha kuwapiga bastola

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ng'wanza Madaso, Jan 11, 2011.

 1. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Na Joseph Ngilisho,Arusha
  MBUNGE wa Viti maalum Tanga ambaye pia ni Katibu wa CCM MKoa wa Arusha, Mary Chatanda, anazidi kuvuruga watu, sasa baada ya kuwavuruga Chadema na CCM, ameanza kuwashambulia waandishi wa habari na kuwaita wahuni, huku akiwatishia kuwapiga bastola.

  Hali hiyo ya kusikitisha imetokea , wakati Katibu huyo alipoitisha mkutano na waandishi wa habari, kwenye jengo la CCM Mkoa, ili kuelezea tamko la kamati ya siasa MKoa wa Arusha, kuhusina na vurugu zilizotokea januari 5 mwaka huu.

  Akitoa tamko hilo alianza kwa kusema, anaipongeza serikali kwa kutumia vyombo vya dola yaani Polisi, kudhibiti wahuni kwa kutumia jeshi la Polisi, kisha akawageukia waandishi wa habari na kuanza kuwafukuza.

  Waandishi waliofukuzwa na huku akiwatamkia maneno ya kashfa kuwa wameletwa sababu ya kufuata uchumi, ni mwandishi wa gazeti la Mtanzania, Fortunata Ringo, John Shija wa radio MJ, Rose JAkson wa radio Safina na Wankyo Ghati wa radio five na gazeti la Jamb oleo.

  Aidha baada ya kuwafukuza hao, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha naye alilazimika kuingilia kati na kumsihi Katibu huyo awaache kwa kuwa waandishi ni kazi yao kuchukua habari.

  Lakini Chatanda aliendelea kushikilia msimamo wake na kusema hapo siyo mahali pa kupata uchumi, watoke nje na waandishi hao walitoka nje ya jengo hilo.

  NAye Adamu Ihucha wa gazeti la East Africa, akielezea kwa masikitiko, alisema yeye ni mmojawapo, alipoingia ndani ya kikao hicho, alimuuliza swali Mary Chatanda, kuwa kwanini wanapingana na IGP, kwa sababu IGP alisema kuna askari walitumia nguvu kubwa kupita kiasi na wewe unasema unawapongeza?


  Mara baada ya swali hilo, Mary Chatanda aliingilia kati na kumkatisha huku akimkejeli mwandishi huyo kuwa, anamshangaa kuvamia mkutano ambao hakualikwa na alikuwa ametokea wapi.

  “Hivi wewe umetoka wapi? Maana hatukujuwi, sisi tunazungumzia mambo yetu na kunyanyuka kutoka nje ya kikao” alisema Ihucha.

  NAye Paul Sarwat wa gazeti la Raia Mwema, naye anasikitishw ana kauli za Katibu huyo na kusema awali, alishawahi kumfuata na kumtaka atoe ufafanuzi juu ya habari za CCM, lakini katibu huyo alimjibu kwa kejeli na kumwambia atamchapa makofi akiendelea kuandika habari za CCM.


  Alisema Chatanda alimwambia kuwa yeye haoni habari za kuandika sipokuwa habari ni cCM tu, akiendelea atamchapa makofi.

  Sarwat alisema kauli kama hizo zinazotolewa na kiongozi mkubwa wa ngazi ya juu ya Mkoa, zinasikitisha sana na zinapaswa kukemewa.

  Akizungumzia kuhusu kauli za Mary Chatanda na kuwaukuza waandishi wa habari, MAkamu Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari, APC, Charles Ngereza, alisema yeye amesikitishw ana udhalilishaji wa Mary Chatanda dhidi ya wanahabari.

  Alisema kuwa yeye kama kiongozi amekuwa akipata malalamiko ya mara kwa mara ya waandishi kutolewa vitisho na lugha chafu na Mary Chatanda, hivyo kama waandishi wanasikitika sana na hali hiyo ikiendelea italeta mvurugano mwingine kati ya CCM na waandishi wa habari.

  Ngereza alisema kuwa mbali ya kuleta mvurugano, pia itahalalisha viongozi na watu wengine kuwadhalilisha waandishi na hiyo tayari imetokea kwa Polisi kuwakamata baadhi ya waandishi kama Musa Juma wa MWananchi, ambaye alikamatw ana Polisi na kupigwa, kasha kunywang’anywa Kamera na kulazimishwa kufuta Picha.

  Alisema huo ni unyama na kuingilia kazi za waandhishi wa habari, ambao hawana mipaka na kazi zao, hivyo wanaomba serikali na viongozi wa juu, kuingilia kati na kuwakalisha viongozi wa Arusha, ili waheshimu uhuru wa wanahabari.
   
 2. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Si Bure kuna mkono wa mtu hapa,Huyu mama hawezi kuwa na nguvu namna hii, kipindi chanyuma nilijua kuwa Katibu mkuu ndo mwenye sauti katika kila lihusulo chama,nasikuweza hata kumfahamu katibu wa CCM wa wilaya yangu enzi hizo.
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Huyu MC ni samsingi ya nani? Kwanza tunaomba picha yake hapa.
   
 4. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Ukiona hivi ujue miti yote inateleza na tayari amechanganyikiwa hajui afanye nini. Unajua kuna watu wakishaua wanaweweseka kutokana na dhamira kuwashtaki na hivyo kukosa amani. Mary Chatanda anaweweseka kwa damu inayomlaani na laana ya maaskofu na amechanganyikiwa na kama CCM hawatamuwahi kumpatia counselling mapema anaweza kujitundika kwani nafsi ina mhukumu na hana amani moyoni. yaani akilala anasikia sauti za vilio vya aliowaua na anatafuta jinsi ya kuondoa frustration kwani anajua kila mtu hampendi wala msimshanga. CCM inaweza kumsaidia kwa kumpumzisha tu arudi home kwa mustakabali wa uhai wake
   
 5. K

  KERENG'ENDE JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Damu ya watu iliyo mwagika iko juu yake na vizazi vyake......
   
 6. W

  We can JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho. Walikuwepo kina Hitler....., sembusa chatandu.
   
 7. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Na hawa waandishi wa habari hawana mtu ama chama chao cha kuwasemea? Kwa nini wasiwazirie kuandika habari za CCM mkoa mpaka Taifa hadi pale watakapo toa tamko la kuwaomba msamaha? kwanini wanawabembeleza?

   
 8. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #8
  Jan 11, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli kuna haja ya kumfahamu vizuri huyu mama, mwenye details zake anaweza kuweka jamii ikamfahamu! Haiwezekani awe na nguvu kubwa hivyo! Kwanini kuna makatibu wangapi wa CCM wa mikoa na hawafahamiki kabisa? Lazima huyu mama ni chakula ya JK, Makamba, Lowassa au boss mwingine wa juu wa CCM! Haiwezekani avuruge uchaguzi wa Meya na mauwaji ya raia wema, awa kashifu maaskofu, wananchi, awatukane na kuwatishia waandishi wa habari na aendelea kupeta tu! Huyu mama ameichafua sana CCM na kuiongezea umaarufu CHADEMA kama Makamba na JK!
   
 9. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #9
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wasira amesema vyema kuwa serikali ikemewe na maaskofu kazi zao siku zote ni kukemea maovu. Huyu mama anahitaji kutiwa moyo aombe msamaha kwa maaskofu.
   
 10. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mambo haya yana sababishwa na utamu wa sketi vs suruali!
   
 11. C

  Choveki JF-Expert Member

  #11
  Jan 11, 2011
  Joined: Apr 16, 2006
  Messages: 448
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Mkuu nani kakwambia kuwa Tanzania kuna waandishi wa habari? Kama wapo basi wengi wao wana utapiamlo, wakioneshwa chakula tu macho yanawatoka pima! na wanasahau fani yao! ukweli na haki inabidi waviweke pembeni.
   
 12. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #12
  Jan 11, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Waandishi wa habari muwe na ushirikiano wa pamoja, kama mmoja wenu akifukuzwa mkutanoni, tokeni wooote bila kuona haya. Huyu Kitanda amewa dhalilisha kwa kusema mmefuata "uchumi" pale. Hata kama alikuwa anawapa "uchumi" mum-andike vizuri aoshe kwa mabosi wake, mtoseni tu si alitoa kwa hiari yake kwani mlimlazimisha! Wake up journalists!
   
 13. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #13
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  HAPA UMEMENENA NENO LA UHAKIKA.
  KAMA SIYO sababu hii basi itakuwa ni ile UGONJWA WA KINA MAMA WAKIKOSA "SHAFT'" kwa muda mrefu pia hupata dalili km hizi.

  Au yote yamechanganyikana KUWEWESEKA NA KUKOSA SHAFT YA KULAINISHA MTAMBO.
   
 14. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #14
  Jan 11, 2011
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Waandishi kuweni majasiri,unyonge wenu ndo kitanzi chenu,toeni tamko kali,pia msimwandike iwe kwa jema au kwa baya,mfungieni kifungo cha miezi mitatu
   
 15. C

  Choveki JF-Expert Member

  #15
  Jan 11, 2011
  Joined: Apr 16, 2006
  Messages: 448
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Hapana huyu mama ndivyo alivyo, na viongozi wetu ndivyo walivyo, jinsia yake haihusiani kabisa na maamuzi yake. Hao wanaume viongozi kwabni wao wakoje? si vivyo hivyo tu, na kwa sababu ya kuwa na viongozi wengi wa dizaini hii (wa kike na wa kiume) ndiyo maana nchi yetu inadidimia na kuporomoka kila leo, at miaka 50 (hamsini baada ya uhuru) bado magonjwa kama kipindupindu, typhod, malaria, TB nk bado yanaongeza kila mwaka watanzania wanaokufa!

  Hazipiti siku mbili bila kusikia ajali mbaya yaua 10, 20, 30, 40 50 au zaidi! katibu mkuu na waziri wa wizara husika wanatesa mjini, wala hawahangaiki kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa kupunguza watu wanaopoteza maisha yao kwenye barabara zetu!

  Leo hii umeme wa mgao umepiga kambi nchini! waziri husika bado anatesa tu barabarani, ukimwona anamereta kwa kupendeza na suti alizovaa, wala hana hili wala lile!

  Bado unasikia ati watoto bado wanafeli darasa la saba! waziri wa elimu ye anatesa tu wala huruma hawaonei hao watoto wanaoishia la saba, kwani anajua ndiyo atakaowaajiri nyumbani kwake kwa mshahari wa tonge!

  Hiyo ndo mifano halisi ya viongozi wetu na ipo mingi sana, (kila kona) je, na hao viongozi (wengi wao wanaume) ni chakula ya nani?
   
 16. K

  Karandanya Member

  #16
  Jan 11, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duu,kweli tanzanzania ipo mikononi mwa watu, INAWEZEKANA NCHI HII CCM Wamejisahau sana sas a basi tutawaonesha kama nchi hii ni yawatanznia wote kuanzia sasa.
   
 17. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #17
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  she z a devil...................
   
 18. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #18
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Nilisema watu hawakunielewa,NDIVYO ALIVYO,weka pembeni hayo ya kutumwa.hakupelekwa Arusha hivi hivi,waliompeleka walijua wanapeleka mtu wa namna gani na kwa kazi gani.......Kwa namna alivyomtengeneza Batilda pamoja na nguvu yote ya Lowassa sijui ni nani huyu mama anamheshimu ndani na nje ya Chama.
   
 19. M

  Major JF-Expert Member

  #19
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 20, 2007
  Messages: 1,425
  Likes Received: 1,143
  Trophy Points: 280
  Hata Machinga hawezi kudhalilishwa namna hii,ndiyo maana mara nyingi huwa wanapambana na Polisi, nawashangaa hawa waandishi wa habari wetu
   
 20. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #20
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Kwenye makampeni wanawatafuta sana hawa waandishi. Sahivi wanawatimua.
  Huyo mama kashajua madudu yake ila hajui kwa kufanya hivyo anazidi kujichafua.
   
Loading...