Chaso-udsm mnatuangusha

spade

Member
Oct 25, 2012
52
26
mwaka 2009/2010 nilipokuwa first year tulimkuta Mr Kiswaga (ccm) akiwa raisi wa DARUSO ingawa inasemekana alipitishwa na watawala kimizengwe. nilishtuka sana kuambiwa kuwa umma wa wanaudsm unaongozwa na kada wa ccm!! ifahamike kuwa inapotokea raisi wa DARUSO akawa ni kada wa ccm basi dhahiri kabisa hata kabineti nzima ya DARUSO itakuwa ni ccm pia. Mwaka iliofuatia yaani 2010/2011 Mr Kipara naye akapita kwa mbwembwe nyingi na shamrashamra za kutosha ilhali umma ukiamini kuwa tumepata kamanda wa kututetea na kulinda masilahi ya wana udsm na taifa kwa ujumla (masalia ya wapiganaji owawa na silinde). Lakini kwa mshangao mkubwa badaae tukaambiwa hapana jamaa in kada/gamba. Pia mwaka 2011/2012 tukapewa polisi Kilawa tena kwa lazima akipitishwa na chuo (Kinamkandala) ili wamfurahishe mkuu wa nchi. Nikajaribu kufuatilia baraza la mawaziri nikakuta karibia lote ni ccm ambalo lilikuwa likienjiniwa na bwana salum hap akisaidiana na mwangomwango. Mwaka 2012/213 pia yalitokea yale yale na kwa utafiti mdogo tu nilioufanya baraza limejaa ccm na kama kawaida ni dhaifu kama serikali ya mwenyekiti wao. Hoja yangu ni kwamba haya yote yanafanyika CHASO wakiwa wapi? ina maana wanaridhika na hii hali ama na wao njaa inawatisha? maana kuna vijana wengi sana walianza chuo wakiapa kuichukia ccm mpaka pumzi yao ya mwisho lakini leo hii wanaimba nyimbo na mapambio ya kuutukuza na kuusapoti wizi wa ccm na sera zao imfu. Kiukweli hii hali inanitia hofu sana juu ya hitimisho la mabadiliko tunayoyaitaji. Sijaelewa kama ni uoga ama njaa ndio inayowabadili vijana, na kwann wawe waoga wa kutetea ukweli na haki? Hapo ndipo naanza kuwa na wasiwasi na uongozi mzima wa CHASO? Hakuna sehemu CHADEMA ina mtaji mkubwa kama vyuoni? sasa kwann minority watawale majority? Hapo ndipo utaona hakuna haja ya kuwalaumu Lindi na Mtwara kuwa wanachelewesha mabadiliko ilhali wasomi bado wanalegalega!WITO WANGUCHADEMA lazima walitazame sana hili kwa jicho la tofauti ikiwa ni pamoja na kubadili mfumo wa upatikanaji wa viongozi vyuoni na kuhakikisha kinakuwa na semina kwa vijana za mara kwa mara kwaajili ya kujenga courage na moyo wa ushindi ndani yao maana hamasa kiukweli haitoshi.Ndio, system ya kuchagua viongozi wa DARUSO ni mbovu sana inayolenga kukibeba chama cha ccm lakini bado CHASO wanakitu cha kufanya kulirekebisha na kuiondoa hii cancer.
 
kwa udsm nijuavyo mm tangu nikiwa pale ilikuwa mgombea urais akijulikana ni GAMBA haki ya nani hapati kura... sasa jamaa walishajua akitaka kugombea anajifanya ni mpambanaji wa ukweli kumbe nia yake aukwae urais tu basi.

nakumbuka uchaguzi wa mwaka 2006/2007 ilikuwa agombee mtatiro akaundiwa zengwe na jina lake likapigwa chini kulikuwa na mgombea mmoja aliprint mabango mengi na yenye ubora wa hali ya juu.. basi raia wakavumisha kuwa amepata pesa kutoka kwa makamba katibu wa sisiem enzi hizo, mambo yalikuwa magumu sana kwa huyu jamaa maana alikuwa anazomewa kila kona aliyopita na kweli kwenye matokeo jamaa akawa wa mwisho

tokea hapo magamba wamekuwa wakigombea urais wa DARUSO kwa siri kubwa(bila kujulikana kama ni GAMBA) huku wakipata misaada ya kifedha kutoka ccm

ndio maana ukiangalia marais hawa Mwita mwikabe-ccm(sasa cdm), Mwita(civil Eng.)-ccm, deo mbasa-ccm, Mlowe-ccm, kiswaga-ccm, kipara simon-ccm
 
Tangu MACHIBYA andoke DARUS mpaka leo sijaona jembe jingine aiseee...... tuliokuwep mgom wa 2008 tunakumbuka mtiti wake...........
 
mwaka 2009/2010 nilipokuwa first year tulimkuta Mr Kiswaga (ccm) akiwa raisi wa DARUSO ingawa inasemekana alipitishwa na watawala kimizengwe. nilishtuka sana kuambiwa kuwa umma wa wanaudsm unaongozwa na kada wa ccm!! ifahamike kuwa inapotokea raisi wa DARUSO akawa ni kada wa ccm basi dhahiri kabisa hata kabineti nzima ya DARUSO itakuwa ni ccm pia. Mwaka iliofuatia yaani 2010/2011 Mr Kipara naye akapita kwa mbwembwe nyingi na shamrashamra za kutosha ilhali umma ukiamini kuwa tumepata kamanda wa kututetea na kulinda masilahi ya wana udsm na taifa kwa ujumla (masalia ya wapiganaji owawa na silinde). Lakini kwa mshangao mkubwa badaae tukaambiwa hapana jamaa in kada/gamba. Pia mwaka 2011/2012 tukapewa polisi Kilawa tena kwa lazima akipitishwa na chuo (Kinamkandala) ili wamfurahishe mkuu wa nchi. Nikajaribu kufuatilia baraza la mawaziri nikakuta karibia lote ni ccm ambalo lilikuwa likienjiniwa na bwana salum hap akisaidiana na mwangomwango. Mwaka 2012/213 pia yalitokea yale yale na kwa utafiti mdogo tu nilioufanya baraza limejaa ccm na kama kawaida ni dhaifu kama serikali ya mwenyekiti wao. Hoja yangu ni kwamba haya yote yanafanyika CHASO wakiwa wapi? ina maana wanaridhika na hii hali ama na wao njaa inawatisha? maana kuna vijana wengi sana walianza chuo wakiapa kuichukia ccm mpaka pumzi yao ya mwisho lakini leo hii wanaimba nyimbo na mapambio ya kuutukuza na kuusapoti wizi wa ccm na sera zao imfu. Kiukweli hii hali inanitia hofu sana juu ya hitimisho la mabadiliko tunayoyaitaji. Sijaelewa kama ni uoga ama njaa ndio inayowabadili vijana, na kwann wawe waoga wa kutetea ukweli na haki? Hapo ndipo naanza kuwa na wasiwasi na uongozi mzima wa CHASO? Hakuna sehemu CHADEMA ina mtaji mkubwa kama vyuoni? sasa kwann minority watawale majority? Hapo ndipo utaona hakuna haja ya kuwalaumu Lindi na Mtwara kuwa wanachelewesha mabadiliko ilhali wasomi bado wanalegalega!WITO WANGUCHADEMA lazima walitazame sana hili kwa jicho la tofauti ikiwa ni pamoja na kubadili mfumo wa upatikanaji wa viongozi vyuoni na kuhakikisha kinakuwa na semina kwa vijana za mara kwa mara kwaajili ya kujenga courage na moyo wa ushindi ndani yao maana hamasa kiukweli haitoshi.Ndio, system ya kuchagua viongozi wa DARUSO ni mbovu sana inayolenga kukibeba chama cha ccm lakini bado CHASO wanakitu cha kufanya kulirekebisha na kuiondoa hii cancer.

Comrade Spade,

Uliyoeleza ni ya msingi sana na kwa kweli CHADEMA inahitaji kuweka mikakati zaidi huko.Kwa hali ilivyo CCM hawastahili kuongota hata chuo kimoja
 
Mkuu unaelewa maana ya demokrasia?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Fine. Lakini umeeleza kana kwamba ni kazi ya akina fulani au ya fulani! Have played ure part kamanda?
 
Comrade Spade,

Uliyoeleza ni ya msingi sana na kwa kweli CHADEMA inahitaji kuweka mikakati zaidi huko.Kwa hali ilivyo CCM hawastahili kuongota hata chuo kimoja

Nilipendekeza hapa siku moja kuwa BAVICHA wanajukumu kubwa sana la kuisimamia hii org. sidhani hata ikiwa baraza linajua hata majina ya viongozi wao na hali zao na je wanapewa majukumu hususa? na ikiwa wanapewa je wanatoa feedback tulitegea CHASO katika vyuo vyote wangekuwa watumiaji sana wa social media katika kujitangaza lakini naona wamela.
 
Makamanda mmezungumza mambo ya msingi sana,pia mmetoa ushauri mzuri,CHASO UDSM, kwa sasa wako kwenye uongozi wa mpito hii inatokana kamanda ambaye pia ni mwenyekiti kuwa nje ya chuo kwa kusimamishwa masomo ila lazima tuongeze nguvu kuhakikisha tunakuwa na CHASO thabiti itakayotoa Rais wa DARUSO pia.
 
Back
Top Bottom