CHASO,Tanga wakana Uasi: Waunga mkono Zitto kutimuliwa CHADEMA

Ni jambo wazi kabisa, kwa nini kutimuliwa kwa akina Zitto CCM hawalali? Kama wanamuona anafaa si wamchukue akawe asset kwao? Wamtumie kama wanavowatumia akina Shonza? Mtela?

Hahahaaaaa....hawa watu wawili wanatumika kama ving'amuzi mwehhhhh..... Ye kalanda wee....
 
Tamko lenyewe limetolewa na kina john,masawe na waoza meno? Hakuna jipya hapo.
 
msaliti huwa na tabia ya nyoka hafi haraka, hivyo CDM endeleni kuponda kichwa cha hawa nyoka mpaka wafeee
 
TANGA WAKANA UASI
Kwa upande wake, Chadema Mkoa wa Tanga kimekemea viongozi waliyoibuka kupinga maamuzi ya Kamati kuu ya kuwavua nyadhifa Zitto na wenzake na kwamba kitendo hicho ni kinyume cha Katiba ya chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa Chadema Mkoa wa Tanga, Jonathan Bahweje, alikemea viongozi hao kuwa wanakiuka katiba kifungu cha saba ibara ya saba na 16 (V) inayoipa mamlaka na uwezo Kamati Kuu ya kuteua na kumuondoa mtu yeyote atakaebainika kwenda kinyume cha katiba.

Bahweje alieleza kuwa viongozi hao wanatenda kosa la kikatiba na kwamba hawana haki ya kuhoji wala kukosoa kilichotendeka kwa kuwa wao ni ngazi za chini, hivyo hawawezi kutengua maamuzi ya chombo kilichopo juu yao.

CHASO YAONYA
Shirikisho la Wanachama wa Chadema Vyuo Vikuu (Chaso) Mkoa wa Dar es Salaam, limesema watu wanaojitokeza hivi sasa na kutoa matamko yanayopinga uamuzi wa kumvua Zitto na wenzake nafasi za uongozi wanatumiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mratibu Mkuu wa Chaso, Elihuruma Jackson Himida, alisema hayo jana alipozungumza na NIPASHE na kusema katika kutekeleza mbinu zao alizoziita ‘chafu’, watu hao wamekuwa wakijitambulisha kuwa ni wanachama wa Chadema wakati siyo kweli.

Alisema Chaso itatoa majibu leo kuhusiana na matamko yanayoendelea kutolewa na watu hao ili Watanzania wajue ukweli halisi wa kile kinachoendelea juu yao.

Alisema uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha Sekretarieti ya Chaso, kilichofanyika jana kujadili watu hao, ambao alisema hawamo hata kwenye kumbukumbu za Chadema kuwa ni wanachama wake, lakini wanashangazwa kuona waandishi wa habari wakiwashabikia.

Kauli hiyo ya Elihuruma imetolewa siku moja baada ya juzi watu waliojitambulisha kuwa ni wanachama wa Chadema, wakiwamo wanafunzi wa vyuo vikuu kuitisha mkutano na waandishi wa habari na kutangaza kile walichokiita mgogoro wa kiutawala kati ya wapigania demokrasia na wahafidhina ndani ya chama hicho.

IRINGA WANENA
Katika hatua nyingine, Chadema katika mikoa ya Iringa na Tanga kimeunga mkono hatua ya Kamati Kuu kuwavua nafasi za uongozi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Zitto na wenzake.

Zitto alivuliwa uongozi Ijumaa iliyopita sambamba na aliyekuwa mjumbe wa Kamati Kuu, Dk. Kitila Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba, kwa tuhuma za kukisaliti chama.

Wote wanatuhumiwa kuandaa waraka ambao ulikuwa na tuhuma dhidi ya chama na viongozi wake ngazi ya taifa.

Chadema mkoa wa Iringa kimesema hatua zilizochukuliwa na Kamati Kuu dhidi ya viongozi hao ni sahihi.

Mjumbe wa Kamati ya Uendaji wa Chadema Nyanda za Juu Kusini, Abdu Changawe, aliwaambia waandishi wa habari mjini Iringa jana kuwa chama hicho kinaongozwa na katiba na kama mtu yeyote atakayehusika kutoiheshimu katiba hiyo, lazima katiba itamshughulikia kikamilifu.

“Kutokana na tabia zao za usaliti ndani ya chama sisi kama wanachama wa Chadema Iringa tunapongeza maamuzi yote na pia tunatoa msimamo wetu kuwa yeyote aliye na tabia kama hiyo ajirekebishe haraka kabla sheria haijachukua mkondo wake,”alisema Changawe.

Aidha, alisema kuwa chama hicho kimejipanga kuhakikisha kuwa haki inatendeka sehemu zote na pia wamejipanga kuwa tayari kutokumbatia uovu wa aina yoyote kwani mafanikio ya chama mpaka sasa yamegarimu damu za watu, mali za watu na hata wengine kufungwa magerezani.

Source:Nipashe Ijumaa
Mimi ni miongoni mwa watu mwanzo kuunga mkono KAMATI KUU kwa maamuzi yake dhidi ya Zitto. Ila mara baada ya kutangazwa tarehe na ratiba ya uchaguzi siku chache mara baada zitto kuvuliwa nyadhifa zake,,,kuna maswali mengi sana nimejiuliza.

Pamoja na kuunga mkono kamati kuu,,,lakini watu lazima tuende mbali zaidi kwa kuhoji, iweje siku chache mara baada ya zitto kuvuliwa uongozi chama kitangaze tarehe na ratiba ya uchaguzi? Kwanini siku zote isitangaze ikiwa kamati kuu iliazimia hadi mwezi ujao uchaguzi ungekuwa umekamilika? Kuchelewa huku kulisubiria Zitto kukosa sifa za kugombea?

Kwanini MKAKATI WA KUTAKA ushindi uonekane usaliti na hujuma kwa chama? hivi yupo mwenye kwenda kwenye uchaguzi bila mkakati? hivi tangu lini mkakati huwa si siri? Je, ina maana mikakati yetu ya kuing'oa CCM ni haramu na uhaini?

Hivi tukisema kuchafuliwa na kuundiwa tuhuma Zitto ni sehemu ya MKAKATI mwingine wa ushindi au wa kubaki madarakani tutakosea? Hivi tukisema MAAMUZI ya kamati ni sehemu ya utekelezaji wa MKAKATI wa kuhakikisha Mbowe anagombea bila kupingwa au hata kama akipingwa basi hapingwi na Zitto tutakosea? Kama ni kweli, Hivi harakati zote hizi za kumchafua Zitto na kuhakikisha hagombei uchaguzi ujao si kiashiria cha udhaifu wa Mbowe?

Nafikiri ifike mahala wanachama tusimamie demokrasia, na chama kisimamie demokrasia na kikubali gharama za demokrasia, Mh.Mbowe asitengeneze mazingira ya kugombea uenyekiti bila kupingwa kama alivyofanya mwa 2009, kama Zitto hatogombea basi wapambe na wapenzi wa Mbowe humu kwenye mitandao wajiepushe kumchamfua mwanaCHAMA yeyote atakayegombea na Mbowe, kinyume chake watatulazimisha tuamini Mbowe ni dhaifu ili hali si kweli.

Halafu jambo lingine sidhani hili ni afya kwa demokrasia endapo mbowe akigombea tena, hata kama chama chetu kinatoa fursa kwa yeye kuweza kugombea tena, lakini nafikiri si jambo jema kwa Mbowe kugombea nyadhifa hiyo. Nafikiri sasa Dr.Slaa ni lazima afikirie kuachana na ukatibu mkuu na badala yake agombee nafasi hiyo, si hivyo tu, ili kutii matakwa ya demokrasia ni vema Mh. Lissu, Frof Safari, Baregu, na Suzan Kiwanga wangejitosa kugombea nafasi hii.

Mbowe hafai hata kidogo kugombea nafasi hiyo kwasababu kwa siasa zinazoendelea ndani ya CHADEMA Mbowe na Zitto wamechafuka. Kwa hivyo ili kulinda taswira ya chama na kukuza demokrasia Zitto kama hili likiisha na akawa bado ni mwanachama basi nashauri asigombee nafasi hiyo,,alikadhalika naye Mbowe asigombee.

Mbowe asigombee kwasababu mbili, mosi hichi kitakuwa ni kipindi chake cha tatu, lakini pili MAAMUZI YA KAMATI KUU, kutangzwa kwa tarehe ya uchaguzi mara baada ya maamuzi hayo na siasa za kumchafua Zitto zilizokuwa zinafanyika ndani na nje ya chama zinapelekea Mbowe kuchafuka kwani inahisiwa yote hayo ni SEHEMU ya utekelezaji wa MKAKATI wa Mbowe wa kugombea bila kupingwa. Kwa kutunza heshima yake na kwa kututhibitishia yote haya si SEHEMU ya utekelezaji wa huo mkakati ni vema asigombee na awaache wanaCHADEMA wengine wagombee.

Sema ukweli na kubali ukweli, hata kama huo ukweli ni pakanga. Pia ukweli na urongo ni watoto pacha waliofanana kupita kiasi, na katika ulimwengu wa kichamchunga ukweli huwa ni urongo hata mbele ya jambia lilofutwa. Katika ulimwengu wa "hisia" urongo wa leo kesho huenda ukawa ukweli, kwa hivyo urongo kukuza kama mbuyu lakini ipo siku utakushusha ghafla hata uwe kama mchicha. La kuzingatia hakuna mwenye kushindana na ukweli kisha akashinda.

Siasa hizi naziona kama siasa za mchwa ndani ya chuguu. Kitendo cha kung'ang'ania madaraka kwa kutumia hila chafu au cha kutaka madaraka pia kwa kutumia hila chafu ni sawa na kitatange cha mchwa cha kutaka mbawa ili apae kama ndege. Tamaa ikawa mbele nyuma ikawa mauti. Mchwa kupanda mbawa akajibatiza jina la kumbikumbi na akaanza kutamalaki kwenye anga kama Mfalme Juha. Huko angani akakutana ndege na alipotua ardhini akakutana na nyoka na vyura; wote hawa wakafanya kumbikumbi ni kivuno. Kifo cha kumbikumbi ndio kifo cha mimba ya chuguu tarajiwa. Tutafika?

Njano5.
0655345394.
 
chanzo gazeti la mjomba mengi. unatarajia nini.
haina tofauti na habari utakayoiona uhuru mzalendo au tanzania daima. ukweli ni kwamba demokrasia imekatwa kidizaini fulani. kila mtu anaona. wapinzani mnatuangusha kwa sisi tunaotaka mabadiliko.
Kwa sababu hatufurahishwi na ujumbe tunaanza kumlaani mjumbe. Nawaelewa sasa.
 
Kwahiyo ulitaka Ratiba iarishwe kwasababu Kavuliwa Uongozi wake! Ratiba lazima zienelee kama kawaida!
 
Back
Top Bottom