Chaso arusha watoa tamko kufuatia maamuzi ya kuwafutia nyadhifa zitto na kitila.

Moses James

Senior Member
Dec 13, 2012
131
21
Kufuatia maamuzi yaliyofanywa na kamati kuu kuwavua uongozi mh.zitto na Dr.kitila makundi na jumuiya mbalimbali za chama zimeeleza namna zilivyo lichukulia uzito suala hilo lililo dhihirisha utofauti kati ya Chadema na ccm.
Ilikuwa ni siku ya mwisho ya kufunga mafunzo ya Chadema ni msingi kwa Makamanda kutoka majimbo takribani manane viongozi wa CHASO mkoa waalikwa kuhudhulia mafunzo hayo ya siku mbili. Baada ya katibu wa jimbo na wilaya ya Arusha mjini kutoa salaam zake kama kiongozi mwenyeji alifuatiwa na mratibu/mwenyekiti wa CHASO mkoa wa Arusha Kamanda KITALIKA, TITHO.E kutoa hotuba fupi kama sehemu ya kufunga mafunzo hayo pamoja na mambo mengine kiongozi huyo kutoka chuo cha uhasibu Arusha aliwaomba msamaha wajumbe wa semina hiyo kwa kuchelewa kutoa msimamo wao kama shirikisho, lakini akasema haikuwa na ulazima huo kwani tayari CHASO mkoa wa Dar-es-salaam walikwishatoa tamko kwa niaba ya mikoa yote.
Kiongozi huyo anaeongoza shirikisho hilo la wasomi kutoka vyuo vya mkoa wa arusha alisisitiza kwamba, hawapo tayari kuona chama kikiwavumilia wasaliti na wasiopenda kufuata misingi na taratibu za chama kwa kisingizio chochote kile iwe ni dini,kabila, kanda ama chochote kingine. Aliongeza kuwa wanatambua uwepo wa vijana waliofukuzwa vyuo kwa ajili ya Chadema, watu waliofiwa wazazi, ndugu na jamaa kwa ajili ya kupigania haki, iwaje watu fulani ati kwa sababu ya kutaka madaraka wafifiishe juhudi hizi za ukombozi kwa watanzania wenye matumaini na Chadema? akimalizia hotuba yake hiyo iliyojaa hisia kali na ambayo iliwafanya wajumbe wapige makofi kila baada ya kuweka nukta alisisitiza kwamba watu wanaoota ndoto za kifo cha Chadema watakufa wao, wajukuu na vitukuu wao Chadema bado itakuwepo kwani ni mpango wa mungu.hata hivyo aliwaahidi wajumbe kutoka majimbo kwamba CHASO mkoa wa Arusha itashirikiana pamoja nae kuhahihisha Chadema ni msingi inafanikiwa kwa zaidi ya asilimia mia moja
source;mjumbe mmoja wa semina hiyo.
 
Hivi hawa si wameambiwa na Dr. Slaa kuwa mjadala umefungwa!

Dr. Slaa ndani ya chama haheshimiki kabisa. Ni sawa na Simba kibogoyo...
 
Hivi hawa si wameambiwa na Dr. Slaa kuwa mjadala umefungwa!

Dr. Slaa ndani ya chama haheshimiki kabisa. Ni sawa na Simba kibogoyo...


Kwi kwi kwiiiii! Hiyo ni njama ya mafisadi lakini imegonga mwamba.

Cc. nakuja
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom