Nawaomba mliopewa viwanda, mniepushe na kikombe hiki. Msiniponze, kazi yangu naipenda na mwenzenu nina watoto - Waziri Mwijage
kijasho chembamba kinamtoka, analeta utani na kujiajiri huyu...
huyu waziri aliwahi sema vijana wana waza sana kuajiriwa
naona leo na yeye anang'an'ania ajira yake alo ajiriwa
Nawaomba mliopewa viwanda, mniepushe na kikombe hiki. Msiniponze, kazi yangu naipenda na mwenzenu nina watoto - Waziri Mwijage.
Waziri anaonekana amepaniki sana. Rais Magufuli alipotembelea Pwani, alimuagiza kuhakikisha wote walipewa Viwanda lakini hawaviendeshi wanyang'anywe. Leo alitembelea Kwanda cha Bora. Alipoongea na wanahabari akawambia "Wambie watu wote, waniepushe na kikombe hiki, Wote mliopewa Viwanda kwa bei ya kutupwa, nmepewa amri tarehe 22 mwezi wa Sita kwaka 2017, na leo mheshimiwa Mavurunde amejibu swali kwa niaba yangu.
Msiniponze nina watoto na hii kazi naipenda. Aliyepewa kiwanda kama hujui utakifanyia nini uje unione nikwambie uje umuone msajili wa Hazina. Mimi ni mtaalam wa shughuli hizi, uje unione nikueleze kama nlivyomfanya mheshimiwa Bora, Bora walikuwa wanafanya Magodauni nikawambia don't do that. Wameanza na ntahakikisha bidhaa yote ya bora inauzwa.
Taasisi za Serikali lazima muiconside Bora, Vatu vyote vitanunuliwa bora.
Hakuna viatu vitapita bandarini kama havina TBS. Unakuta binti anatembea halafu miguu inalemaa Sendoff inaharibuka. Kwahiyo Viatu vya wakina Mama lazima Viwe na TBS.
Ikibidi nitawawekea na TFDA, Ntawawekea na NEMC kule bandarini kusudi vitu vinavyokuja viwe vya Ubora“. Amesema Mwijage.
Nmemuonea huruma sana. Anaongea hadi machozi yanataka kumtoka. Pole sana Waziri Mwijage