Charles Kitwanga, amkabidhi Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba Ofisi Rasmi

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba akikabidhiwa rasmi ofisi leo na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga ambaye alitumbuliwa na Rais Magufuli kwa kwa kosa la kuingia bungeni na kujibu hoja huku akiwa amelewa..
C12.jpg

C61.jpg

Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwa May 20 na Rais John Magufuli baada ya kuingia bungeni na kujibu swali akiwa amelewa, alikabidhi ofisi jana kwa Mwigulu Nchemba ambaye amechukua nafasi yake.

Baada ya uteuzi wake kutenguliwa, Kitwanga alitoweka bungeni na baadaye ilielezwa kuwa alikwenda Israel kabla ya hivi karibuni kurejea nchini na kusema kuwa yote yaliyotokea anamwachia Mungu.

Hivi karibuni, Rais Magufuli alimhamishia Mwigulu katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi huku Dk Charles Tizeba akimrithi Mwigulu.

Akizungumza katika mahojiano baada ya kukabidhi ofisi, Kitwanga alisema kila Mtanzania anaweza kufanya kazi iwapo atapewa nafasi huku akinukuu kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’ na kwamba amefanya makabidhiano hayo kwa wema na upendo wa hali ya juu.

Alisema amekabidhi ofisi bila kinyongo kwa sababu Tanzania si nchi yake peke yake bali ni ya wananchi wote.

Ratiba jimboni
Akizungumzia ratiba jimboni mwake, Kitwanga alisema Agosti 6, atafanya ibada ya shukrani nyumbani kwake Misungwi kumshukuru Mungu akisema hiyo ni baada ya ziara yake ya wiki sita mfululizo kwa wapigakura wake.

Ziara hiyo itaanza keshokutwa atakapokutana na kamati ya mipango na fedha kabla ya kufanya kikao na madiwani wote wa jimbo hilo Jumamosi ijayo.

Alisema Jumatatu ijayo atakabidhi vifaa mbalimbali vikiwamo magodoro na vitanda kwa hospitali ya wilaya na zahanati, vyerahani na kompresa kwa vikundi za ujasiriamali katika hafla itakayofanyika kwenye Stendi ya Mabasi Misungwi: “Hapo nitatoa nafasi ya dakika 10 mpaka 20 kwa waandishi wa habari kuniuliza maswali... lakini nisingependa umbeya... kwangu mimi ni Tanzania kwanza, nawaambia kabisa.”

Baada ya shughuli hiyo, alisema siku inayofuata atakutana na wenyeviti wa vijiji vyote vya jimbo hilo kupanga namna atakavyofanikisha ziara yake katika maeneo yao, kazi ambayo alisema ataifanya kwa wiki sita mfululizo; “nitafanya ziara siku tano kwa kila wiki mfululizo, zamani nilikuwa nikigawa muda wa kutembelea jimbo na kurudi Dar kufanya kazi sasa nitakuwa huko muda wote. Dar nitakuwa nakuja mara chache tu.”
 
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba akikabidhiwa rasmi ofisi leo na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga ambaye alitumbuliwa na Rais Magufuli kwa kwa kosa la kuingia bungeni na kujibu hoja huku akiwa amelewa..

Tupia neno moja kwa Charles Kitwanga.
7f4283b2-55f2-4065-9b8a-6e01d6e24b03.jpg

Chanzo : EATV
 
Safi sana Kitwaga, pamoja na yote yaliyokupata kupitia our dear Larger bado unakabidhi ofisi kwa bashasha tele bila kinyongo chochote.
Ubarikiwe sana na uwe wa kupiwa mfano!!!!!!!!!!!!!
 
Anaekabidhi ofisi ana furaha tele kuriko anaekabidhiwa....safi kitwanga ndio uanaume mitihani sehemu ya maisha...
 
Mwigulu hizi kazi za mambo ya ndani alizokuwa anafanya alikuwa anatokea wapi? Kwenye korido au?
 
Fenicha za ofisi za serikali zinatakiwa siziwe za kutoka China. Magereza yetu ni mafundi sana wakutengeneza fenicha nzuri na imara kama zinavyoonekana kwenye ofisi hii ya waziri wa mambo ya ndani.
 
Kitwanga kwaheri ya kuonana, sasa kawafanyie kazi wananchi wako waliokuchagua... Uwaziri kwako haukufaa, hukuwa that much competent ktk UWAZIRI...!! For me ur the lowest performer...!!
 
Kitwanga kwaheri ya kuonana, sasa kawafanyie kazi wananchi wako waliokuchagua... Uwaziri kwako haukufaa, hukuwa that much competent ktk UWAZIRI...!! For me ur the lowest performer...!!

Sio kweli mkuu, competence haipimwi kwa kuangalia media inasema nin kuhusu wewe. Competence inapimwa kwa kuangalia achievement of targets basing on perfomance indicators, tena zaid kwa kuwianisha na resources ulizopewa.

Yaliyomkuta yamemkuta, yanaweza kumkuta mtu yeyote, hebu tuache kuwachukia watu bila sababu za msingi. Manake saiv kuna kamtindo mtu akisikia Lugumi, Lugumi naye akajiona mfukoni hana kitu anahamishia hasira zake kwa Lugumi, this is not fair. Jiweke neutral tu uone maisha yako yatakuwa safi sana.

Kwanza huyu jamaa ana mdomo wa heri sana, refer ile video alimwambia rais achukue fomu, kweli kachukua kafanikiwa. Hatuwez kuconclude hivyo sana, lakin ndo evidence iliyopo mpaka saiv.
 
Back
Top Bottom