UncleBen
JF-Expert Member
- Oct 27, 2014
- 9,616
- 12,074
Amani iwe kwenu nyote
Tarehe 20/03/2015 bunge letu tukufu
lilipitisha muswada wa sheria na udhibiti wa silaha.
Na kwenye sheria hiyo ilitaja sifa kadhaa za anayepaswa kumiliki silaha
Moja ya sifa hizo ni kuwa Mtanzania halisi ,
Sifa nyingine ni mwombaji kutokutumia kilevi chochote ,
Ndugu yetu Kitwanga alifukuzwa kwenye nafasi yake kama waziri wa mambo ya ndani kwa kosa la kuwa mlevi ,
Ikitokea mwombaji amekutwa na kosa hilo baada ya kumiliki silaha ni hatua gani zichukuliwe ? Sheria haijweka wazi
Sheria imetaja tu makosa ya matumizi mabaya ya silaha ama kumiliki silaha kinyume cha sheria na adhabu yake ni miaka mitano jela au faini ya shilingi milioni kumi..
Pengine ni muda muafaka kwa bunge letu kuangalia tena sheria hiyo ikiwa na mapungufu basi waweze kuirekebisha
Kwa kuwa haya yamemkuta aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani itakua ni busara kwa serikali hii ya hapa kazi tu kutolifumbia macho jambo hili ile iwe funzo pia kwa wale wanaoshi kama malaika na pengine wanapaswa kuishi kama mashetani .
Kufanya hivyo kutatuma ujumbe kwa wote wanao miliki silaha hizi kuwa makini kwani kwa kosa kama la ulevi linaweza kusababisha kufutiwa leseni ama uzembe wa baadhi ya watu kutoa silaha zao hadharani bila sababu ya msingi.