Charles Kimei: Serikali iwekeze kwenye Elimu ya ujuzi ambayo inaakisi maisha yetu ya kila siku

lulu za uru

JF-Expert Member
Aug 7, 2015
2,171
2,660
Salamu wakuu, nilipata nafasi ya kutizama Bunge Leo wakati wa majadiliano ya hotuba ya Raisi, kwa moyo mmoja kabisa nimpongeze mbunge Charles kimei kwa kufikiri na kutoa mawazo ya nje ya box.

Graduates kwa sasa ni wengi mtaani hakuna ajira za kutosha kila anayegraduate kuajiriwa, ni wakati wa meza kupinduliwa kazi za mikono ziwekewe kipaumbele kikubwa kwenye system ya elimu...mitaala itanduliwe tupone, hii mind set ya MTT akimaliza Chuo aajiriwe akashike kalamu tu kwenye kiyoyozi ife, vijana wapewe skills za maisha zinazotumika kila Siku.

Kuna skills zingine mie nilisoma sijui unaiapply VP kwenye maisha ya kawaida serious!. Mh. Kimei Ameishauri serikali kuwekeza zaidi kwenye skills ambazo ajira zake zinaakisi maisha yetu ya kila siku kina fundi simu ,magari na the likes VETA izidi kukua.
 
Kimei na Benno Ndulu ndo mababa zangu wa uchumi kwa hapa Tanzania..

Japo hawajanifundisha ila nimejifunza mengi kutoka kwao.

Kikubwa ni kwamba, wameelimika kiasi kwamba wanaweza kutambua na kutofautisha theory na practice vitu ambavyo bado vinawasumbua wasomi wengi nchini
 
Charles Kimei ni msomi aliyeelimika mwenye kujua jinsi ya kuitumia elimu yake kwa matumizi sahihi ya mazingira yaliyopo
Hongera kwake mbunge wa Vunjo
Kimei Huyo wa kusikilizwa alibadilisha benki ya kizawa ya CRDB hadi kuwa ya kimataifa yenye Matawi nje ya nchi

UShauri wangu syllabus zote za Veta zichukue syllabus ya China na ujerumani ziko vizuri sababu zinafunza mtu kuwa producer wa bidhaa za kupeleka sokoni sio tu fundi tu msubiri aitwe kufanya ufundi !!!! hii ya kuitwa mtu anakuwa na idle time muda mrefu bila kazi
 
Kimei Huyo wa kusikilizwa alibadilisha benki ya kizawa ya CRDB hadi kuwa ya kimataifa yenye Matawi nje ya nchi...
Curriculum ya elimu ya Tanzania na afrika kwa ujumla hazisadifu mahitaji ya nchi, imekazia kumuandaa mtoto kuajiriwa tuu.
Kwa kiasi kikubwa sana curriculum yetu imechangia kuua vipaji wanavyozaliwa navyo watoto, inakinzana pia na shughuli za uzalishaji zilizo katika jamii zetu kama nufugaji na kilimo na na hii inachangia sana kuwako kwa hii shida ya ajira Tanzania na Africa

Eti zaidi ya 70% ya ajira zipo kwenye kilimo halafu vijana wetu wapenda chipsi hawajui hata kama viazi vya chips vinachumwa kwenye mti kama maembe au vinachimbwa ardhini 😎😎
 
Kuna dogo mmoja mama yake kamlazimisha kusoma weee.
Form 4 kagonga 0.
Kumbe mwenzie akili ya darasani Hana.
Kampeleka ufundi
Curriculum ya elimu ya Tanzania na afrika kwa ujumla hazisadifu mahitaji ya nchi, imekazia kumuandaa mtoto kuajiriwa tuu.
Kwa kiasi kikubwa sana curriculum yetu imechangia kuua vipaji wanavyozaliwa navyo watoto, inakinzana pia na shughuli za uzalishaji zilizo katika jamii zetu kama nufugaji na kilimo na na hii inachangia sana kuwako kwa hii shida ya ajira Tanzania na Africa
 
Curriculum ya elimu ya Tanzania na afrika kwa ujumla hazisadifu mahitaji ya nchi, imekazia kumuandaa mtoto kuajiriwa tuu.
Kwa kiasi kikubwa sana curriculum yetu imechangia kuua vipaji wanavyozaliwa navyo watoto, inakinzana pia na shughuli za uzalishaji zilizo katika jamii zetu kama nufugaji na kilimo na na hii inachangia sana kuwako kwa hii shida ya ajira Tanzania na Africa
Shida mwingereza alipokuja lengo lake lilikuwa kuandaa makarani wa white color jobs tulipopata uhuru tuka adapt elimu ya muingereza!! ya kuzalisha white color jobs officials!! Tukabaki na mentality ya kikoloni hadi Leo

Niseme wazi tulipofikia white color jobs are not nuch needed kwenye makert na hazina future kubwa both in the public sector na private sector

Wanafunzi wasisome tu kama wehu waangalie soko linataka nini. NA WAZAZI tuwe serious tuangalie soko linataka nini vyuo pia waangalie soko lataka nini sababu wakisubiri wazazi na watoto waamke kugomea course zao sababu hazina ajira wala future watakuja jikuta vyuo vinafungwa kwa kukosa wanafunzi
 
Mtihani huyo hata veta huwezi mpeleka zero hawapokei course ndefu labda fupi kama udereva nk
Ataendesha gari za nani? Siku hizi private sectors ofice nyingi ukiajiriwa na unastahili kupewa gari ujue kujiendesha mwenyewe maana hamna atakayekulipia dereva, daladala wanapeana kazi kifamilia ili kupunguziana ukali wa maisha, kama ukoo wenu hauna daladala au malori ni ngumu kiasi.

Ukisema uje kwenye Taxi technology imeingia watu wengi ni madreva tax wa gari zao wenyewe kupitia uber. Hapo ukimpeleka udereva uwe na gari tayari sehemu
 
Mimi Sasa hivi Nina mipango ya kujifunza.
CCTV
Electric gates.
Na electric fence.
Najua ipo siku vitakuja kunisaidia
Mtaani wako kibao wanafanya tena darasa la saba sikukatishi tamaa lakini wahi soko bado Lipo ni ajabu darasa la saba wamekufa fast mover ndio wanafunga security systems ,mafundi simu na computer ,wauza vifaa vya simu na computer,wafunga sattelite dishes nk wasomi wamelala wanakoroma kusubiri ajira serikalini sijui shida nini ina maana darasa la saba ana more entreprenur skills kuliko graduate aliyesoma somo la entrepreneurship chuo?

UKo kwenye right track hongera
 
Halafu ni mbaya, unapeleka mtoto shule hadi form4 anapata0 na ukimpeleka shamba hawezi kulima pia..... na hapo keshakua mtu mzima 18, 19
Mpeleke attachment kwa mama ntilie atalipwa elfu tatu kwa siku kupika ku serve na kuosha vyombo ajifunze umama au ubaba nitilie halafu mpe mtaji baada ya mwaka afanye
 
Back
Top Bottom