Charles Kimei: One of the most exposed and reputable banking top executives in East & Central Africa. Hakupaswa kujiingiza katika siasa hizi za vyama

Kura zenyewe hazikutimia - kasaidiwa sana huyu jamaa hadi aibu kwa mtu mwenye status kama yake.
 
Mambo vp JamiiForums.

Ninapoandika hoja hii, ninaomba ifahamike kuwa i have nothing personal with mzee Kimei na ninatambua kuwa yeye ni moja katika ya hazina kubwa ambazo taifa hili linazo katika masuala mazima ya uchumi na banking.

Watu walikuwa wanapenda sana kumshambulia kaka yangu Pascal Mayalla kuwa amejiingiza katika siasa kwa sababu ya njaa. Sasa huyu CEO mstaafu yeye ana njaa gani? Charles Kimei alipaswa kubaki kama mzee mshauri wa masuala ya uchumi/banking hapa Tanzania/Africa Mashariki na sio kujiingia katika siasa hizi za vyama.

He is one of the most exposed and reputable top executives in banking and finance industry kwa hapa Tanzania na East Africa. Hakupaswa kuonesha mlengo wa wazi wazi wa chama chochote cha kisiasa kiwe upinzani au tawala.

Siasa hizi za vyama angewaachia mzee Dr. Bashiru Ally na Mheshimiwa Mbowe. Kimei angebaki kuwa kama William B. Harrison Jr. CEO mstaafu wa bank kubwa kuliko zote ya Marekani ya JPMorgan Chase ambaye sasa ni mshauri mwandamizi katika umoja wa banks za nchini humo - The American Bankers Association - (ABA)

William B. Harrison Jr.
=====

View attachment 1694756

Hata kama asingekuwa mbunge wa CCM akaamua kujiunga na CHADEMA, CUF au ACT, kitendo cha kujiingiza katika siasa za vyama kunampotezea intergrity yake aliyotumia nguvu kubwa na miaka mingi sana katika kuijenga kwenye tasnia ya masuala ya uchumi/banking.

Watumishi wa CRDB wenye mlengo tofauti wa kisiasa (upinzani) waliokuwa wanamuona kama role model wao sasa wataanza kuzozana naye hata kama sio face to face hata kupitia mitandao. Alistaafu kwa heshima nzuuuuri mzee wa watu, sasa anajiharibia heshima alipojiingiza kwenye siasa.

Achilia mbali CRDB, wale watumishi wa banks zingine waliokuwa wanamuona kama kioo bora kwa maana aliitoa CRDB kutoka kuwa bank ya kitanzania mpaka kufungua matawi yake nchi jirani, sasa nao atakuwa anajibizana nao kwa sababu za kisiasa. Yeye CCM wao wapinzani. Ipo wapi tena heshima ya mzee Kimei katika industry ya banking?

Kimei kwa levels zake angepaswa awe anaendesha kampuni kubwa sana ya masuala ya ushauri wa kiuchumi/kibank Africa Mashariki na sio kwenda bungeni kurushiana vijembe na wanasiasa ambao wengi ni umri wa watoto wake wa kuzaa, tena anawazidi mpaka exposure.

Kuna mada ilianzishwa humu kuhusiana na kauli yake moja ya kisiasa ( Dkt. Kimei na Spika Ndugai, watoto wenu mliwasomesha ufundi simu? ) ambayo inaonekana imewakera wengi na watu wanamshambulia kweli kweli.

View attachment 1695012

Mzee Kimei kwa sasa ni mwanasiasa wa mlengo wa chama tawala (CCM), ina maana watu waliokuwa wanamuheshimu kama CEO bora kwenye banking/uchumi ambao wapo mlengo wa siasa za upinzani sasa wataanza kumtukana na kumrushia maneno ya kejeli jambo ambalo mzee hakuwa na ulazima wa kulifanya.

Wapo watu watahoji mbona kuna professors na PhD holders wapo katika siasa miaka nenda rudi, lakini ni nani kama Kimei katika taaluma ya banking? Mzee Kimei bado unaweza kuwa mzalendo kama mimi pasipo kuwa mwanasiasa.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Wengi wanajiingiza kwenye siasa kwasababu ya kuzuhia kutochunguzwa na vyombo vya dola si unajua uheshimiwa
 
Mzee Kimei aliongea fyongo alipompa taarifa Mh Halima Mdee. Na Mh Halima alimjibu kishkaji bila ya kutaka aonekane alichosema ilikuwa fyongo. Mshaurini Dr Kimei kukaa kimya kwenye vitu vigumu vya kutetea serikali. Serikali kweli imefilisi mifuko ya kijamii ya wafanyakazi na kwa muda mrefu anatoa utetezi usio na mashiko kabisa.
 
Back
Top Bottom