Charles Kimei ashukuru kukamilika usambazaji wa umeme katika Vijiji vyote 78 vilivyopo Jimbo la Vunjo

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
Na Mwandishi Wetu.
Vunjo, Moshi.

Mbunge wa Jimbo la Vunjo Mheshimiwa Dkt Charles Stephen Kimei ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kupitia wizara ya Nishati kwa kutekeleza ahadi yake ya kukamilisha usambazaji wa umeme katika Vijiji vyote 78 vilivyopo Jimbo la Vunjo.

"Jukumu langu ni kuendelea kuiomba na kuishawishi serikali kukamilisha usambazaji wa umeme katika vijiji vyetu vyote. Naomba kuwajulisha serikali hii ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia imetuhakikishia kukamilisha vijiji vyetu vyote 78 vilivyopo Vunjo. Kwa niaba yenu napenda kumshukuru sana Rais Samia, kwani ameonesha kutupenda kwa vitendo ndio maana tunapata fedha nyingi za miradi ya maendeleo, tuendelee kumuunga mkono."

Mbunge huyo ametembelea vijiji viwili-02 (Kijiji cha Soko na Kochakindo) kujionea kazi inayoendelea ya kusambaza umeme katika vijiji hivyo. Tayari Vijiji hivyo vimetengewa Bajeti 21/22 ili miundombinu ya umeme ifike kote. Kwasasa kazi hiyo imefikia hatua nzuri na muda wowote umeme utawaka katika makazi ya wananchi hao.

Wananchi wa Vijiji vya Soko na Kochakindo wameishukuru serikali kwa kuendelea kusikiliza na kutatua kero zao huku wakimpongeza Dkt Kimei kwa kuwa Mbunge anayewasemea na kuwatetea ndani na nje ya bunge.


Aidha wamempongeza kwa kazi nzuri katika jimbo hilo ikiwemo kurudi kufanya mikutano ya wananchi na kuwasikiliza kila wakati kabla na baada ya bunge. Wamemuahidi kuendelea kumpa ushirikiano kwa kuwa ameonesha kuwajali na kuwapenda.

Mwisho Dkt. Kimei ameipongeza Serikali kwa kuzindua rasmi mradi wa usambazaji wa umeme katika maeneo yenye umeme lakini baadhi ya wananchi hawajafikiwa mradi wa "DENSIFICATION" katika Jimbo la Vunjo ambapo kila Kitongoji kitafikiwa na huduma ya umeme. Uzinduzi wake ulifanyika tarehe 29/07/2021 katika Kijiji cha Nganjoni na aliyekuwa Waziri wa Nishati Mheshimiwa Dkt. Kalemani.

#VunjoKaziInaendelea
#TanzaniaKaziInaendelea
#TwendeNaSamia

IMG-20210918-WA0051.jpg
 
Duh, Kimei naye amekuwa kama mzee wa Kiraracha! Mimi nijuavyo ni REA inapeleka umeme vijijini kutokana na tozo za miaka na miaka tunazokatwa kwenye manunuzi ya umeme.
 
Nilikuwa nasikia eti migombani umeme na barabara za lami toka mkoloni...kumbe bado!

Naamini Mama Samia atawapelekea bila kubeba majani ya kuomba msamaha....ila wenyeji wa huko wanaoishi kwenye miji mingine waache kumtukana Mama Samia.
 
Yule rais wa kwenye mawe hataki kabisa kuliona hili jina.
Hii sredi inampa simanzi.
 
Ila siasa ina umarufu kuliko kitu chochote ..nakumbuka crdb ndiyo bank ya kwanza kuwa na ATM card tz
.ila jili limesahulika.
.
Leo
Tunashukuru kuwaka umeme vunjo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom