mtembea kwa miguu
JF-Expert Member
- Mar 23, 2012
- 1,121
- 1,726
Kwenye hoja ya udikiteta wa rais Magufuli, kuna madikiteta wabaya na madikiteta wazuri au madikiteta wema.
Madikiteta wazuri ni wale ambao wanafanya vitendo vya udikiteta kwa nia njema, hata ikibidi kuivunja katiba, au kukiuka sheria, taratibu na kanuni, kwa nia njema, ni udikiteta unaokubalika, mfano katiba inaruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano, rais Magufuli anataka watu wafanye kazi na sio kuwa wazururaji kwa kisingizio cha kufanya maandamano, au kuwa ni watu wanaokaa bure tuu kwa kisingizio cha kuhudhuria mikutano ya siasa, watu wenye muda wa kuhudhuria mikutano ya siasa kila siku ni watu wasio na kazi, hivyo kama tangazo lake la kupiga marufuku mikutano ya siasa na maandamano ni ili watu wasizurure ovyo, na wasikae onyo bila kufanya kazi, then huu ni udikiteta mzuri. Dikiteta wa aina hii anaitwa a benevolent dictator.
Hata kuachiwa kwa Babu Seya, sheria hairuhusu wabakaji na wauwaji kuachiliwa kwa msamaha wa rais, kilichofanyika pia ni udikiteta, ila umefanywa kwa nia njema kuwa vipindi walivyotumikia gerezani, wamejirekebisa, na sasa ni watu wema, hivyo udikiteta is not necessarily ni udikiteta mbaya, udikiteta mwingine ni udikiteta mzuri.
Big up sana rais Magufuli.
Paskali
Vip mzee baba umeichungulia nisani nyeupe au noah nyeusi na sasa umeamua kuflipp maandishi yako? Hahahah
Any way tuendelee kushangilia ila ikifka zam yako keep on kushangilia