CHAPTER ONE: Ewe Mwanadamu amka.! Acha Kushupaza Shingo,Mungu yupo,na Siku ya hukumu ipo.!

Heart Wood.

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
972
1,150
CHAPTER ONE: EWE MWANADAMU AMKA.! ACHA KUSHUPAZA SHINGO, MUNGU YUPO NA SIKU YA HUKUMU IPO.

UTANGULIZI: UWEPO WA MUNGU.!

Hatma ya Mwanadamu imefanywa kuwa siri kubwa, isipo kuwa kwa wachache wenye Imani juu ya Uwepo wa Mungu. Wenye kumjua na kumwamini Mungu tunaifahamu hatma ya Maisha yetu, tunafahamu kwa nini tupo Duniani, tunafahamu chanzo cha Ulimwengu na tunakoelekea. Tunafahamu na kuamii kuwa Maisha ya hapa Duniani si mwisho wa Masha halisi ya Mwanadamu,bali kuna Maisha mengine katika ulimwengu wa Roho yataendelea. Tunaamini kuwa katika maisha ya Ulimwengu wa Roho huko Mbinguni, watakaopata nafasi ya kushiriki Maisha hayo ni wale waliofanikiwa kuwa watiifu na kuwa Wacha Mungu hapa Duniani. Kisha wale wasiomjua na kumtii Mungu mwisho wao ni kwenye ziwa la Moto, yaani ule Moto wa Milele usiozimika.

Kama nilivyogusia hapo mwanzo kuwa, kuna Watu wachache wasioamini habari za uwepo wa Mungu, wengi wao ni Watu waliosoma sana na kuelimika katika masuala ya Elimu ya Ulimwengu/ Dunia hii tuliyopo. Watu hao ni Wasomi wakubwa hasa katika nyanja za Sayansi na Historia. Kwakweli, watu hao wamefikia hatua ya kusema kuwa ni Mwanadamu ndiye aliyemuumba Mungu katika Fikra zake na wala hakuna Mungu aliyemuumba Mwanadamu. Ofcourse, licha ya udhihirisho wa kazi za Mungu kupitia Watumishi wake yaani Wanadamu, kwa kuwa Mungu hawezi kuonekana kwa hali ya macho yetu, bali Mungu hudhihirika kupitia kwa Wnadamu kama ilivyo tangu hapo mwanzo enzi za akina Adam, Nuhu, Ibrahimu, Isaka, yakobo, Musa, Yoshua n.k, bado watu hao hawaamini lolote katika hayo yanayofanyika. Husema kuwa hayo ni maigizo na Sayansi ya Sanaa, ambayo Mtu yeyote anaweza kuifanya. Husema kuwa yote yanayofanyika ni masuala tu ya Kisaikolojia na mauza uza ya Ulimwengu huu.

Licha ya kuwepo ushahidi mpaka sasa wa mahali ambako Biblia imetaja kuwako Wanadamu wa Awali hapo Mwanzo, mahali ambako babu zetu katika Imani mfano akina Abrahamu,Isaka na Yakobo walikuwako,kama vile baadhi ya sehemu za Mashariki ya Kati (Middle East) Yaani kama vile Yerusalemu, Jordani,Lebanon,Damascus, n.k pamoja na sehemu za Ulaya kama Greece na Italy ambako Mtume Paulo alifika kuhubiri INJILI, pamoja na sehemu mojawapo Africa yaani Misri ambako YESU alitajwa kufika wakati Yusufu na Maria walitorokea ili kuepusha kifo cha YESU na ambako wana wa Israel walikombolewa kutoka utumwani mikononi mwa Farao, lakini bado Wanadamu hawa wanaopinga uwepo wa Mungu huishia kusema sisi tunaosema Mungu yupo tulete Ushahidi wa Kisayansi kuthibitisha kama kweli Mungu yupo. Ndio maana Mungu huwaita watu hawa ni VIPOFU, wana macho lakini hawawezi kutazama.

ULIMWENGU WA ROHO.

Siku ya Leo, ntajikita katika kuelezea maana ya Ulimwengu wa Roho kwa kutumia mifano rahisi ya Kidunia. Sitatumia references nyingi za Biblia na endapo itabidii iwe hivyo, basi sitakuwa na namna nyingine kwa maaana naamini kuwa ni Roho Mtakatifu ndiye anayeniwezesha kuandika mtiririko huu wa Mawazo na ndiye atakayekuwa amekusudia iwe hivyo.

KUHUSU MAZINGAOMBWE.!

Bila shaka huko nyuma, hata sasa japokuwa mambo haya yamepungua kiasi chake maana si kama ilivyokuwa zamani, kulikuwa na hawa watu walio julikana kama Wana Mazingaombwe, Waliruhusiwa kuonesha sanaa zao hasa Mashuleni kwa kile kinachoaminika kuwa kazi zao ni sehemu moja wapo ya kuendeleza Sanaa Mashuleni. Hakika walijitahidi kutuonesha kila aina ya mambo kwa Ubunifu wao kadiri walivyojaaliwa na roho wao.

Swali la Msingi hapa la kujiuliza ni kuwa, kulikuwa na ubunifu gani katika hali ya kawaida ya Kibinadamu ilyiokuwa inapelekea mara pesa inabadilika na kuwa karatasi, mara Mtu anameza kijiti na kubadilika kuwa kalamu, mara Mtu analazwa Usingizi fofofo bila ya kujitambua ili hali dakika mbili zilizopita alikuwa katika hali ya kawaida tu. Mara soda inakuwa maji au kinyume chake, mara kokoto zinakuwa pipi n.k Hakika tulishuhudia mambo mengi tu ila hapa nimetaja kwa uchache kama mifano.

Bila kupepesa macho na kupindisha pindisha mambo, ule ulikuwa ni Ulimwengu wa Rohoni, yaani mojawapo ya Uchawi. Mimi naamini kabisa kuwa yale Mazingaombwe ilikuwa ni sehemu ya Uchawi kama uchawi mwingine wa kuruka na ungo, kuroga n.k. Ila tu ule ulitafutiwa jina zuri na kuitwa sanaa.

Sasa basi, kama utakuwa nami na kuamini kuwa mambo hayo yalitokea kwa mgongo wa sanaa, bila shaka utakubaliana nami kuwa kuna mambo mengine huweza kufanyika sirini na yasionekane katika Ulimwengu wa macho haya ya kawaida. Ndiyo,upo Ulimwengu unaitwa Ulimwengu wa Roho. Hapa Duniani/Ulimwenguni, kuna maisha ya kawaida yanayoendelea katika macho yetu haya ya kawaida na kuitwa Ulimwengu wa Mwili, hali kadhalika, kuna Masiha mengine zaidi yanaendelea katika Ulimwengu mwingine ambao hauonekani yaani ulimwengu wa Rohoni.

Katika Ulimwengu wa Mwili ndio kuna Mwanadamu, Viumbe hai wanaoonekana, Magari, Nyumba, Barabara,Mito, Maziwa, Bahari, mifumo ya Utawala ya Wanadamu, Nchi n.k. Katika Ulimwengu wa Roho, yupo Mungu na Ufalme wake, yaani Malaika, vilevile yupo Shetani na Ufalme wake ukihusisha Majini,Mapepo, Vimbwengo, Wachawi wa kila namna n.k.

Ukweli ni kwamba, japokuwa Ulimwengu wa Roho umepewa kisogo na Mwanadamu na kutokupewa kipaumbele kwa kile tu jkuwa eti ni masuala yasioonekana, hivyo kumfanya Mwanadamu kuwa busy zaidi na masula yanayoonekana katika Ulimwengu wa Mwili katika hii Dunia kwa zaidi, lakini ukweli halisi ni kwamba, Maisha katika Ulimwengu wa Roho, ndiyo maisha ya kipekee tena yenye uwezo mkubwa zaidi ya ule Ulimwengu wa Roho. Kila kinachofanyika katika Ulimwengu wa Roho kina Impact kubwa katika Ulimwengu wa Mwili. Maisha katika Ulimwengu wa Mwili kwa kiasi kikubwa au kwa utoshelevu wake yanakuwa coordinated zaidi na kuongozwa na Maisha katika Ulimwengu wa Roho. Kama hujui hili basi ni kwa sababu tu ya ufahamu wako kutokuwa well informed kuhusu Elimu hii ya Ulimwengu wa Roho kwa Utoshelevu wake.

Labda tuwaulize hawa waliosoma na kuelimika sana katika maairifa ya Maisha ya hapa Duniani na kusema kuwa hakuna Mungu. Je, hamuoni kuwa mlipokuwa wadogo mlikuwa watupu kichwani, na Elimu iliyowafanya muone hakuna Mungu ni Elimu ya Upande mmoja pekee? Je, mna kiwango gani/ mmefanya bidii gani kupata Ufahamu wa Maisha katika upande mwingine yaani Ulimwengu wa Roho ? Mbona kuna watu wengine wasomi kama ninyi lakini wanamuamini Mungu.? Ni dhahiri kuwa hata Wasomi wanapopata elimu ya Ulimwengu wa Roho, huamini kuwa Mungu yupo. Ni vigumu sana na mara chache sana kukuta Mtu aliyekwisha pata elimu kuhusu Mungu baadae apinge uwepo wa Mungu.

UCHAWI NA UGANGA.
Mfano mwinghine ulio rahisi kuweza kuyathibitisha Maisha ya Ulimwengu wa Roho ni masuala ya Uchawi na Uganga. Kwa bahati mbaya pia kuna Watu wachache husema hakuna Uchawi, lakini hili si tatizo lao wenyewe, bali ni kutokana na sababu ya Ufahamu wao kutokuwa na taarifa za kutosha kuhusu masula haya.

UTHIBITISHO;
Mara nyingi Mwanadamu hawezi kufanya kitu bila ya kuwa na ufahamu wa jambo fulani. Bila shaka umewahi kuona hata Waigizaji wa Filamu huigiza namna Shughuli za Kichawi na Waganga zinavyofanyika. Kama Uchawi na Uganga usingelikuwepo basi isingelikuwa rahisi kwa Waigizaji kubuni jambo la Kichawi na Uganga bila ya kuwa na tone la Ufahamu wa uwepo wa mambo hayo. Kuigiza kwao vile ni ushahidi mwingine juu ya uwepo wa shughuli za Kichawi na Kiganga. Kule kupandisha kwa Waganga ni Majini yanakuwa yamemuingia Mganga na kuyaruhusu kusema masuala kadha wa kadha, Kabla sijamjua Mungu sawa sawa, niliwahi kupelekwa kwa Mganga mmoja kutokana na matatizo yaliyokuwa yakinisibu, kwa kweli nilishangaa sana jinsi ambavyo Mganga yule aliweza kuzungumzia kuhusu maisha yangu na kuzungumzia mambo yaliyofanyika Nyumbani kwetu wakati sikumsimulia chochote na wala hatukuwahi kufahamiana hapo awali, Leo hii baada ya kumjua Mungu, nimebaini kuwa yale yalikuwa ni Majini katika Ulimwengu wa Roho, Majini ni sehemu ya Ufalme wa Ulimwengu wa Roho. Shetani ana uwezo wa kufahamu chochote kuhusu Mwanadamu. Mambo yote yanayo fanyika katika Uganga na Uchawi ni masula ya Ulimwengu wa Roho. Hivyo huu pia ni ushahidi kuwa kuna maisha ya Ulimwengu wa Roho.

Mifano mingine ni ile ambayo umewahi kusikia kuwa Mchawi fulani alianguka kwa kuishiwa nguvu akiwa katika harakati zake za Kichawi. Je, umewahi kusikia juu ya kupigwa marufuku kuhusu Ramli chonganishi? Ile ni kazi mojawapo ya Kiganga/ Kichawi ila imetafutiwa jina zuri na kuitwa Ramli chonganishi. Ilitakiwa tu kuitwa kazi za Kichawi. Katika Mifumo yetu ya Sheria, suala la Kichawi halitambuliki kwa kile tu kuwa hauwezi kuthibitisha juu ya uwepo wa Uchawi kwa macho. Lakini masula haya yapo. Kwa msingi huo, huo ni ushahidi mwingine wa kuthibitisha masula yanayofanyika katika Ulimwengu ule usioweza kuonekana kwa macho, yaani Ulimwengu wa Roho.

KUTOLEWA/ KUFUKUZWA KWA MAJINI/ MAPEPO KATIKA MIKUTANO YA INJILI.
Mfano mwinginme ni huu, Je, umewahi kuona Katika Mikutano ya Injili namna ambavyo mapepo hukemewa na watu kuanguka na wengine kuanza kutamka maneno yanayoashiria kupagawa? Ile ni hali ambayo hudhihirisha Ulimwengu wa Roho pia. Kwa bahati mbaya sana Watu wengine husema yale ni maigizo au kupagawa Kisaikolojia. Sasa kama ni maigizo, iweje Ulaya, Marekani, Asia, South Afrika, Nigeria na kwingineko kote Waigize na matendo yote hufanana? Yaani uigizaji au matatizo ya Kisaikolojia yafanane Duniani kote.? Ni Chuo gani au mtu gani ambaye huwafundisha watu kufanya maigizo kiasi kile Duniani kote.? Hali ile ni halisi.Hii hutokea Makanisani na kwenye Mikutano ya Injili. Mie wakati nasoma Sekondari, wakati bado nilikuwa pia nina mashaka juu ya ukweli wa jambo hili, kulikuwa na kikundi cha Maombezi cha Wanafunzi wenzetu, basi siku moja kukafanyika Maombi ya pamoja wakaalikwa Wanafunzi wenzetu kutoka Shule moja ya Wasichana, Maombi yalipoanza tu, kuna Wanafunzi wadada wakaanza kupagawa na Mapepo na kuanza kujirusha rusha na kisha kuanguka chini kisha kuombewa na Mapepo yakafukuzwa na kuwaachia. Waliokuwa wakiendesha Maombi yale walikuwa ni Wanafunzi wenzetu, ingekuiwa ni Watu nisio wajua ningeendelea kuamini kuwa ni maigizo tu yaliyopangwa kama wasemavyo Watu wengine leo hii.

UHUSIANO WA UMISIONARI ENZI ZA UKOLONI NA UENEZI WA INJILI.

Fact nyigine ambayo baadhi ya watu husema kuwa hizi Dini tulizonazo yaani Uislamu na Ukristo ni Dini za Kiarabu na Kizungu, yaani zililetwa kwa mantiki ya kututawala enzi za Ukoloni, eti zilikuja ili kutupumbaza tu ili wakoloni wajichukulie Mali zetu Waafrika. Swali la kujiuliza, kama kweli Dini hizi ni Uongo na zilikuja ili kututawala,iweje na wao huko Ulaya, Asia, Amerika na kwingineko waendelee kushiriiki mpaka leo hii katika Imani hizo hizo tulizonazo huku Afrika. Nikupe tu taarifa kuwa, kwa sasa hata huko Ulaya, Marekani na Asia kuna Waafrika na wengine ni Watanzania wanashiriki kueneza habari za Mungu. Wengine hudiriki kusema kuwa Ukristo ni wa Wazungu. Huku ni kutojua Historia ya Ukristo. Ukristio haukuanzia Ulaya. Ukristo ulianzia Mashariki ya Kati yaani Israel, huko ndiko Chimbuko la Ukristo baada ya YESU KRISTO kuwako Duniani katika hali ya Kimwili yapata miaka 2017 sasa iliyopita.Yawezekana kweli baadhi ya Wamisionari waliitumia Dini kama sehemu ya kujitwalia mali za Waafrika, lakini Injili ya Mungu inaweza kuenezwa either katika hali ya Ubaya au Wema.

UHUSIANO WA ALAMA ZA TAIFA NA UDHIHIRISHO WA UWEPO WA MUNGU.
Tazama Wimbo wetu wa Taifa, maudhui yake ni kuomba rehema kwa Mungu, tazama Dua ya kuliombea Bunge, maudhui yake ni kumtaja Mungu aweze kuibariki Nchi na Viongozi wake. Tazama viapo vya Viongozi kuanzia Rais hadi Viongozi wengine. Viapo vyote vile hufanyika kwa kumuomba Mungu huku muhusika akiwa ameshika kitabu Kitakatifu kulingana na Imani yake. Yote hiyo ni kudhihirisha kuwa hata Nchi yenyewe inatambua uwepo wa Mungu. Sasa kama ndugu yangu wewe umezaliwa na kuikuta hata Nchi yenyewe inatambua uwepo wa Mungu, iweje wewe unayejiita msomi mwenye umri sijui wa mika 40 au 50 ukatae kuwa Mungu hayupo.? Wakristo tunaamini kuwa YESU alikuwapo miaka 2017 sasa iliyopita. Tangu hapo watu wamekuwa wakiamini kuwa YESUalikuwapo,ila wewe ndugu mwenye miaka 40, 50 au 60 unapinga mambo haya uliyoyakuta na kuwepo zaidi ya Miaka 2000 iliyopita. Bila shaka watu kama ninyi mnaopinga hamuwezi kukosekana, maana hata Israel aliko zaliwa Yesu mpaka sasa kuna Watu bado hawaamini kama YESU alishakuja na kwamba ndiye aliyetabiriwa tangu enzi za mababu zetu wa Imani kuwa atakuja Mwokozi wa Ulimwengu.

Mifano ipo mingi ila kueleza kwa uchache, kwa leo naomba kuhitimishia hapo. Lengo kubwa la andiko hili ni kuweka msingi mzuri wa wewe kuelewa na kuamini kuwa Yote yasemwayo kuhusu Mungu ni kweli na dhahiri. Baada ya andiko hili la Msingi, itafuatia maandiko mengine ya namna bora na sahihi ya kuweza kufahamu kwa nini tupo Duniani na ni nini Mungu amekusudia kuhusu Maisha ya Mwanadamu.

Kama andiko hili litakuwa sehemu ya Mwanzo wako mpya wa Maisha hasa katika kumuamini Mungu, basi tuungane pamoja kisha nitaandaa Ujumbe mwingine kwa ajili yako ili kukuongoza katika ile kweli kadiri Roho wa Mungu atakavyonijalia. Mungu akubariki sana na karibu tuendelee kujifunza kuhusu Mahusiano yetu na Mungu aliye muumba wetu.
 
Yesu sio Mungu
Hiyo ni mada nyingine tofauti, andiko hili siyo lengo lake. Hili andiko lengo lake ni kutengeneza foundation kwa ajili ya Mtu kupata ufahamu wa uwepo wa Ilimwengu wa Roho, maisha baada ya Kifo au Maisha zaidi ya haya tuyaonayo. Baadae itafuatiwa na mengine mengi na hilo lako likiwamo. Naona unachokisema ni kikubwa zaidi kuliko lengo la mada hii kwa leo.
 
Unaamini Mungu yupo?
Unahisi Mungu yupo?
Au unajua Mungu yupo?

Unaamini Uchawi ni zao la ulimwengu wa roho ama ni nguvu ya asili[natural force] ambayo binadam bado hajajua jinsi inavyofanya kazi ila yumkini siku moja Sayansi ikampa jibu?

Maaigizo ya kichawi ni ushahidi kuwa Uchawi upo

Je maigizo yanayohusu Aliens ni ushaidi kuwa aliens wapo au ni ubunifu tu wa watunzi?
 
Umeandika ujinga lakini nimejitahidi kuusoma wote. Kwa hizi taka mnazojaza kwenye vichwa vyenu, hata kama Mungu angekuwepo kwa bahati mbaya naye angekuwa Atheist.

Kwenye uzi wako nilitegemea kuona yafuatayo:

1.Sababu ya Mungu kumuumba Shetani.

2.Sababu za kuwepo kwa dini zaidi ya moja, je kama dini zote ni za Mungu mbona zinatofautiana sana?

3.Ushahidi wa uwepo wa Mungu pamoja na ulimwengu wa roho.

4.Kwanini unatumia Bible kama ushahidi wa uwepo wa Mungu ilihali bible inajikanganya na kujipinga yenyewe? pia kwanini Bible imehamasisha maovu mengi mno kama kweli yenyewe ni neno la Mungu mwenye upendo wote?

5.Umesema kwa kuwa waigizaji wanaigiza juu ya uchawi na uganga, basi uchawi na uganga ni kweli na vina exist. Je huoni kwakuwa watu wanatafiti, jinfunza, na kuigiza juu ya evolution inamaanisha kuwa evolution inayopingana na creationism ni kweli?

6.Mleta mada umenishangaza sana ulipouliza iweje matatizo ya kisaikolojia yaathiri watu wa mabara tofauti. Hujiulizi kwanini watu wa America, Ulaya, Africa, na Asia wanaugua UKIMWI na kuonesha dalili zinazofanana? kama unashangaa jinsi matatizo ya kisaikolojia yanavyoathiri watu wa mabara tofauti, jiulize pia kwanini risasi inaweza kuua watu wa mabara tofauti.

7.Halafu unasema injili itaenezwa kwa ubaya ama wema, hii ndio sababu ya mapadre wanajeshi wa crusade waliotumia kuiba mali za watu, kuua na kubaka wanawake na kufanya kila aina ya uovu kisa tu kueneza injili.Huyo Mungu anayesema ni wa amani, mbona haenezi amani? kwanini anatumia mabavu kulazimisha watu wampende? huoni kwamba huo ni udikteta?

8.Nilitegemea pia kuona ukitoa sababu za kwanini mabaki ya watu wa kale zaidi yanapatikana Africa na siyo M.East ambako dini zenu zinasema ndiko mtu wa kwanza yaani Adam alikoishi.

9.Kwanini unahusisha elimu na atheism? unataka kuniambia kuwa watu ambao hawakwenda shule wote ni waumini wa dini? mbona baadhi yetu huu ushirikina mnaouita dini tulishtukia ni uongo tangu utotoni?

10.Kwa kuwa ukristo ulienezwa kwa vita vya crusade, huoni ni haki kwa Boko haram na Al shabab kutumia mauaji, vita, na ubakaji kama njia ya kueneza dini yao ya kiislam? je kama ni hivyo huoni kuwa uwepo wa dini zote ndio vyanzo vya maovu na ukatili kwa watu?
Human being have naturally born with willing, and God creates us in this way so as to be able to control all the things on the earth including the devil.
Binadamu huyuhuyu alitokea alitumia vibaya utashi huo na kujikuta akiwekewa mipaka katika utashi na uhuru wa kutawala kila kitu, soma MWANZO 1:28, Binadamu wakapewa mamlaka juu ya kila kitu.

Kuhusu kuwa chini ya mamlaka ya shetani ni pale tu binadamu unapokuwa mtiifu kwa shetani ukaacha Mungu, matumizi mabaya ya utashi/willingness. Shetani haukuubwa kwa makusudi ya kutuadhibu sisi bali sisi tumejiadhibu na kwa kujiweka chini ya shetani kwa kukosa utiifu kwa muumba wetu (Mungu).

Kuna swali umeuliza kuwepo kwa dini nyingi; Jibu lako ni kuwa ubishi kama wako leo hii na ubinafsi wetu sisi wanadamu hauondoi uhalali wa kuwepo Mungu, rudi nyuma kidogo soma habari za historia ya kuhusu Mungu ni, ukisoma agano la kale lote hutakuta dini nyingi bali walikuwepo watu wenye imani tofauti, ukichunguza kwa umakini utakuta kila imani ilikuwa na muungu ulio mkubwa ambao huo muungu ulikuwa na nguvu kuliko zote na hawakuweza kumwelezea huyo muungu na ndiyo Mungu.

Ubishi na kushupaza shingo kwa mwanadamu kumetufanya watu wengi kushindwa kuelewa logic nyingi juu ya uwepo wa Mungu.

SWALI LA KUJIFIKIRISHA:-
Mnao bisha uwepo wa Mungu mnatumia sayansi je, unaweza nitajia sayansi ambayo ni siyo limited less??

Unaweza kunitajia asili nguvu zote hapa duniani (natural forces).

Have you ever gone to trace the origin&ends of lives??
 
God is A Spirit, you can't justify Him by Scientific evidences, Can you Justify Love, care, Joy, and Happiness Scientifically.?
We can prove scientifically the effects of love, hate, happiness joy etc but not GOD. We do not see gravity ( a scientific phenomenon) as we do not see GOD, but we can see the consequences/ effects and prove them scientifically of denying gravity! With God, you can not, you ill end up in IMANI..... and associatinf unproved phenomenon as due to God.
 
U r right to say we can't prove Love, happiness, Joy etc on their own Scientifically, rather, their effects. On the same sense, We are able to prove the presence of God by the Effects of his power. Through him, demons do manifest and detach themselves from the Human Spirits under the presence of God.
 
Perpetuaion of revelations, demon can not be proved either! scientifically
 
God is A Spirit, you can't justify Him by Scientific evidences, Can you Justify Love, care, Joy, and Happiness Scientifically.?
First you begin with false analogy between God[Spirit] and Love[Emotion]

We can detect the Presence of unseen force by examining its objective effects which ought to be the same to all viewers[not revelation]

The very concept of God is fallacy from Philosophical analysis to scientific scrutiny
 
Umeandika ujinga lakini nimejitahidi kuusoma wote. Kwa hizi taka mnazojaza kwenye vichwa vyenu, hata kama Mungu angekuwepo kwa bahati mbaya naye angekuwa Atheist.

Kwenye uzi wako nilitegemea kuona yafuatayo:

1.Sababu ya Mungu kumuumba Shetani.

Mungu hakumuumba Shetani kama alivyo leo, Mungu aliwaumba Malaika, Shetani kabla ya uasi alikuwa Malaika vilevile, wote wakiwa wema. Baadae huyo Shetani akamuasi na kujitenga na Mungu. Baada ya kuasi akapoteza ushirika na Mungu(Devil lost his fellowship with God). Baada ya kupoteza ushirika na Mungu, akajitenga na Mungu na kuondolewa kwenye Ufalme wa Mungu. Shetani akaandikiwa adhabu ya Milele, lakini Shetani hakuondoka peke yake ktk Ufalme wa Mungu, isipokuwa aliondoka na baadhi ya Malaika waasi tunaowaita Mapepo na Majini ambao anashirikiana nao hata sasa.

2.Sababu za kuwepo kwa dini zaidi ya moja, je kama dini zote ni za Mungu mbona zinatofautiana sana?

Mungu hana dini, isipokuwa Wanadamu tumetengeneza utamaduni wetu wa kumwabudu na kumfuata Mungu kwa kitu kinachoitwa Dini. Mungu si wa Dini yoyote ile hapa Duniani. Wala hakuleta Dini hapa Duniani, isipokuwa Wanadamu wenyewe wamejiwekea utaratibu wao kupitia Dini zao.

3.Ushahidi wa uwepo wa Mungu pamoja na ulimwengu wa roho.

Miongoni mwa Ushahidi ndio kama huo nilioeleza hapo juu. Soma kwa makini na taratibu ukiwa free minded. Ondoa kwanza negativity kwenye akili yako. Ruhusu akili yako iwe huru kupokea mambo mapya. Using'ang'anie tu hayo uliyonayo. Ubongo wa Mwanadamu umeumbwa kwa kujifunza mambo, huwezi kujua jambo bila kujifunza. Labda nikuulize, Je, una ufahamu kwa kiwango gani kuhusu BIBLIA ?

4.Kwanini unatumia Bible kama ushahidi wa uwepo wa Mungu ilihali bible inajikanganya na kujipinga yenyewe? pia kwanini Bible imehamasisha maovu mengi mno kama kweli yenyewe ni neno la Mungu mwenye upendo wote?

BIBLIA haijichanganyi, isipokuwa msomaji wake ndiye anaweza kujichanganya. BIBLIA siyo kitabu cha kawaida kama VITABU vingine. Ukisoma BIBLIA kama unavyosoma Novels lazima utachanganyikiwa tu.

5.Umesema kwa kuwa waigizaji wanaigiza juu ya uchawi na uganga, basi uchawi na uganga ni kweli na vina exist. Je huoni kwakuwa watu wanatafiti, jinfunza, na kuigiza juu ya evolution inamaanisha kuwa evolution inayopingana na creationism ni kweli?

Shetani naye anafanya mambo yanayoweza kufanana na Mungu. BIBLIA inamtaja Shetani kama mungu wa Dunia hii. Kwahiyo, si jambo la kushangaza kuwa naye anaweza kuwawezesha watu wake kutimiza lengo lake.

6.Mleta mada umenishangaza sana ulipouliza iweje matatizo ya kisaikolojia yaathiri watu wa mabara tofauti. Hujiulizi kwanini watu wa America, Ulaya, Africa, na Asia wanaugua UKIMWI na kuonesha dalili zinazofanana? kama unashangaa jinsi matatizo ya kisaikolojia yanavyoathiri watu wa mabara tofauti, jiulize pia kwanini risasi inaweza kuua watu wa mabara tofauti.

Ili mtu awe na UKIMWI kuna njia zake za maambukizi. UKIMWI hauwezi kuruka tu hewani na kumpata mtu. Hali kadhaklika kwa risasi uanzosema, haziwezi kumpata mtu bila kusababishwa na msababishaji anayezisababisha. Unaweza kuthibitisha namna ya hichpo unachosema ni matatizo ya Kisaikolojia yanaweza kuhama kutoka kwa mtu aliyo nayo na kwenda kwa Mtu mwingine.? Kwa mfano, mie naweza tu kusoma BIBLIA ndani kwangu kisha nikaanza ku practice kilichoandikwa na jambo kutendeka kama vile kumuombea mtu mwenye mapepo na kupagawa kisha mtu huyo kuwa vizuri baada ya maombezi bila hata kuambukizwa hiyo hali kutoka kwa Mtu mwingine kama unavyosema.

7.Halafu unasema injili itaenezwa kwa ubaya ama wema, hii ndio sababu ya mapadre wanajeshi wa crusade waliotumia kuiba mali za watu, kuua na kubaka wanawake na kufanya kila aina ya uovu kisa tu kueneza injili.Huyo Mungu anayesema ni wa amani, mbona haenezi amani? kwanini anatumia mabavu kulazimisha watu wampende? huoni kwamba huo ni udikteta?

Hukuelewa, nilimaanisha kuwa Mtu anaweza kutumia INJILI kwa manufaa yake mwenyewe japokuwa si kwa kusudi la kueneza INJILI Watu wapate WOKOVU, ila ajinufaishe mwenyewe. Unapoeneza INJILI kwa manufaa yako mwenyewe na si kwa dhamira ya kusukumwa na Roho wa Mungu basi ni kufanya HILA, ni sawa na mtu kukuchekea, usoni ataonekana mwenye furaha japokuwa moyoni amejaa HUSUDA na kadhalika. Ile furaha inayoonekana usoni itaendelea kuwa FURAHA japokuwa MOYONI hauna furaha.

8.Nilitegemea pia kuona ukitoa sababu za kwanini mabaki ya watu wa kale zaidi yanapatikana Africa na siyo M.East ambako dini zenu zinasema ndiko mtu wa kwanza yaani Adam alikoishi.
Hayo mabaki si yamegunduliwa na Wnadamu wenye damu na Nyama kama wewe na Mimi.?

Tangu lini kazi ya Mwanadamu ikawa kwa ukamilifu 100% ? Hujawahi kusikia bado kuna Ugunduzi unaendelea ambao haukuwahi kugundulika hapo awali.?

9.Kwanini unahusisha elimu na atheism? unataka kuniambia kuwa watu ambao hawakwenda shule wote ni waumini wa dini? mbona baadhi yetu huu ushirikina mnaouita dini tulishtukia ni uongo tangu utotoni?

Sikumaanisha kuwa ni wenye Elimu pekee ndio wanapinga uwepo wa Mungu, nimesema kuwa wengi wao ni watu wenye Elimu..!

10.Kwa kuwa ukristo ulienezwa kwa vita vya crusade, huoni ni haki kwa Boko haram na Al shabab kutumia mauaji, vita, na ubakaji kama njia ya kueneza dini yao ya kiislam? je kama ni hivyo huoni kuwa uwepo wa dini zote ndio vyanzo vya maovu na ukatili kwa watu?

Nimekwisha jibu hapo juu.
 
Unaamini Mungu yupo?
Ndiyo, Mungu yupo.
Unahisi Mungu yupo?
Au unajua Mungu yupo?
Sihisi, bali ninaamini na ni Uhalisia kuwa Mungu yupo.

Unaamini Uchawi ni zao la ulimwengu wa roho ama ni nguvu ya asili[natural force] ambayo binadam bado hajajua jinsi inavyofanya kazi ila yumkini siku moja Sayansi ikampa jibu?
Uchawi ni jambo halisi katika Ulimwengu wa Roho, yeyote anayemwamini Mungu, vilevile anakuwa na ufahamu kuhusu Uchawi maana umeelezwa dhahiri kupitia BIBLIA.

Maaigizo ya kichawi ni ushahidi kuwa Uchawi upo
Ndiyo, kule kuigiza ni ushahidi pia kuwa uchawi upo.
Je maigizo yanayohusu Aliens ni ushaidi kuwa aliens wapo au ni ubunifu tu wa watunzi?
Sina hakika zaidi kuhusu Ubunifu. Ila Shetani pia yupo na huweza kuwawezersha Watu wake kufanya jambo ili kutimiza mapenzi yake.
 
CHAPTER ONE: EWE MWANADAMU AMKA.! ACHA KUSHUPAZA SHINGO, MUNGU YUPO NA SIKU YA HUKUMU IPO.

UTANGULIZI: UWEPO WA MUNGU.!

Hatma ya Mwanadamu imefanywa kuwa siri kubwa, isipo kuwa kwa wachache wenye Imani juu ya Uwepo wa Mungu. Wenye kumjua na kumwamini Mungu tunaifahamu hatma ya Maisha yetu, tunafahamu kwa nini tupo Duniani, tunafahamu chanzo cha Ulimwengu na tunakoelekea. Tunafahamu na kuamii kuwa Maisha ya hapa Duniani si mwisho wa Masha halisi ya Mwanadamu,bali kuna Maisha mengine katika ulimwengu wa Roho yataendelea. Tunaamini kuwa katika maisha ya Ulimwengu wa Roho huko Mbinguni, watakaopata nafasi ya kushiriki Maisha hayo ni wale waliofanikiwa kuwa watiifu na kuwa Wacha Mungu hapa Duniani. Kisha wale wasiomjua na kumtii Mungu mwisho wao ni kwenye ziwa la Moto, yaani ule Moto wa Milele usiozimika.

Kama nilivyogusia hapo mwanzo kuwa, kuna Watu wachache wasioamini habari za uwepo wa Mungu, wengi wao ni Watu waliosoma sana na kuelimika katika masuala ya Elimu ya Ulimwengu/ Dunia hii tuliyopo. Watu hao ni Wasomi wakubwa hasa katika nyanja za Sayansi na Historia. Kwakweli, watu hao wamefikia hatua ya kusema kuwa ni Mwanadamu ndiye aliyemuumba Mungu katika Fikra zake na wala hakuna Mungu aliyemuumba Mwanadamu. Ofcourse, licha ya udhihirisho wa kazi za Mungu kupitia Watumishi wake yaani Wanadamu, kwa kuwa Mungu hawezi kuonekana kwa hali ya macho yetu, bali Mungu hudhihirika kupitia kwa Wnadamu kama ilivyo tangu hapo mwanzo enzi za akina Adam, Nuhu, Ibrahimu, Isaka, yakobo, Musa, Yoshua n.k, bado watu hao hawaamini lolote katika hayo yanayofanyika. Husema kuwa hayo ni maigizo na Sayansi ya Sanaa, ambayo Mtu yeyote anaweza kuifanya. Husema kuwa yote yanayofanyika ni masuala tu ya Kisaikolojia na mauza uza ya Ulimwengu huu.

Licha ya kuwepo ushahidi mpaka sasa wa mahali ambako Biblia imetaja kuwako Wanadamu wa Awali hapo Mwanzo, mahali ambako babu zetu katika Imani mfano akina Abrahamu,Isaka na Yakobo walikuwako,kama vile baadhi ya sehemu za Mashariki ya Kati (Middle East) Yaani kama vile Yerusalemu, Jordani,Lebanon,Damascus, n.k pamoja na sehemu za Ulaya kama Greece na Italy ambako Mtume Paulo alifika kuhubiri INJILI, pamoja na sehemu mojawapo Africa yaani Misri ambako YESU alitajwa kufika wakati Yusufu na Maria walitorokea ili kuepusha kifo cha YESU na ambako wana wa Israel walikombolewa kutoka utumwani mikononi mwa Farao, lakini bado Wanadamu hawa wanaopinga uwepo wa Mungu huishia kusema sisi tunaosema Mungu yupo tulete Ushahidi wa Kisayansi kuthibitisha kama kweli Mungu yupo. Ndio maana Mungu huwaita watu hawa ni VIPOFU, wana macho lakini hawawezi kutazama.

ULIMWENGU WA ROHO.

Siku ya Leo, ntajikita katika kuelezea maana ya Ulimwengu wa Roho kwa kutumia mifano rahisi ya Kidunia. Sitatumia references nyingi za Biblia na endapo itabidii iwe hivyo, basi sitakuwa na namna nyingine kwa maaana naamini kuwa ni Roho Mtakatifu ndiye anayeniwezesha kuandika mtiririko huu wa Mawazo na ndiye atakayekuwa amekusudia iwe hivyo.

KUHUSU MAZINGAOMBWE.!

Bila shaka huko nyuma, hata sasa japokuwa mambo haya yamepungua kiasi chake maana si kama ilivyokuwa zamani, kulikuwa na hawa watu walio julikana kama Wana Mazingaombwe, Waliruhusiwa kuonesha sanaa zao hasa Mashuleni kwa kile kinachoaminika kuwa kazi zao ni sehemu moja wapo ya kuendeleza Sanaa Mashuleni. Hakika walijitahidi kutuonesha kila aina ya mambo kwa Ubunifu wao kadiri walivyojaaliwa na roho wao.

Swali la Msingi hapa la kujiuliza ni kuwa, kulikuwa na ubunifu gani katika hali ya kawaida ya Kibinadamu ilyiokuwa inapelekea mara pesa inabadilika na kuwa karatasi, mara Mtu anameza kijiti na kubadilika kuwa kalamu, mara Mtu analazwa Usingizi fofofo bila ya kujitambua ili hali dakika mbili zilizopita alikuwa katika hali ya kawaida tu. Mara soda inakuwa maji au kinyume chake, mara kokoto zinakuwa pipi n.k Hakika tulishuhudia mambo mengi tu ila hapa nimetaja kwa uchache kama mifano.

Bila kupepesa macho na kupindisha pindisha mambo, ule ulikuwa ni Ulimwengu wa Rohoni, yaani mojawapo ya Uchawi. Mimi naamini kabisa kuwa yale Mazingaombwe ilikuwa ni sehemu ya Uchawi kama uchawi mwingine wa kuruka na ungo, kuroga n.k. Ila tu ule ulitafutiwa jina zuri na kuitwa sanaa.

Sasa basi, kama utakuwa nami na kuamini kuwa mambo hayo yalitokea kwa mgongo wa sanaa, bila shaka utakubaliana nami kuwa kuna mambo mengine huweza kufanyika sirini na yasionekane katika Ulimwengu wa macho haya ya kawaida. Ndiyo,upo Ulimwengu unaitwa Ulimwengu wa Roho. Hapa Duniani/Ulimwenguni, kuna maisha ya kawaida yanayoendelea katika macho yetu haya ya kawaida na kuitwa Ulimwengu wa Mwili, hali kadhalika, kuna Masiha mengine zaidi yanaendelea katika Ulimwengu mwingine ambao hauonekani yaani ulimwengu wa Rohoni.

Katika Ulimwengu wa Mwili ndio kuna Mwanadamu, Viumbe hai wanaoonekana, Magari, Nyumba, Barabara,Mito, Maziwa, Bahari, mifumo ya Utawala ya Wanadamu, Nchi n.k. Katika Ulimwengu wa Roho, yupo Mungu na Ufalme wake, yaani Malaika, vilevile yupo Shetani na Ufalme wake ukihusisha Majini,Mapepo, Vimbwengo, Wachawi wa kila namna n.k.

Ukweli ni kwamba, japokuwa Ulimwengu wa Roho umepewa kisogo na Mwanadamu na kutokupewa kipaumbele kwa kile tu jkuwa eti ni masuala yasioonekana, hivyo kumfanya Mwanadamu kuwa busy zaidi na masula yanayoonekana katika Ulimwengu wa Mwili katika hii Dunia kwa zaidi, lakini ukweli halisi ni kwamba, Maisha katika Ulimwengu wa Roho, ndiyo maisha ya kipekee tena yenye uwezo mkubwa zaidi ya ule Ulimwengu wa Roho. Kila kinachofanyika katika Ulimwengu wa Roho kina Impact kubwa katika Ulimwengu wa Mwili. Maisha katika Ulimwengu wa Mwili kwa kiasi kikubwa au kwa utoshelevu wake yanakuwa coordinated zaidi na kuongozwa na Maisha katika Ulimwengu wa Roho. Kama hujui hili basi ni kwa sababu tu ya ufahamu wako kutokuwa well informed kuhusu Elimu hii ya Ulimwengu wa Roho kwa Utoshelevu wake.

Labda tuwaulize hawa waliosoma na kuelimika sana katika maairifa ya Maisha ya hapa Duniani na kusema kuwa hakuna Mungu. Je, hamuoni kuwa mlipokuwa wadogo mlikuwa watupu kichwani, na Elimu iliyowafanya muone hakuna Mungu ni Elimu ya Upande mmoja pekee? Je, mna kiwango gani/ mmefanya bidii gani kupata Ufahamu wa Maisha katika upande mwingine yaani Ulimwengu wa Roho ? Mbona kuna watu wengine wasomi kama ninyi lakini wanamuamini Mungu.? Ni dhahiri kuwa hata Wasomi wanapopata elimu ya Ulimwengu wa Roho, huamini kuwa Mungu yupo. Ni vigumu sana na mara chache sana kukuta Mtu aliyekwisha pata elimu kuhusu Mungu baadae apinge uwepo wa Mungu.

UCHAWI NA UGANGA.
Mfano mwinghine ulio rahisi kuweza kuyathibitisha Maisha ya Ulimwengu wa Roho ni masuala ya Uchawi na Uganga. Kwa bahati mbaya pia kuna Watu wachache husema hakuna Uchawi, lakini hili si tatizo lao wenyewe, bali ni kutokana na sababu ya Ufahamu wao kutokuwa na taarifa za kutosha kuhusu masula haya.

UTHIBITISHO;
Mara nyingi Mwanadamu hawezi kufanya kitu bila ya kuwa na ufahamu wa jambo fulani. Bila shaka umewahi kuona hata Waigizaji wa Filamu huigiza namna Shughuli za Kichawi na Waganga zinavyofanyika. Kama Uchawi na Uganga usingelikuwepo basi isingelikuwa rahisi kwa Waigizaji kubuni jambo la Kichawi na Uganga bila ya kuwa na tone la Ufahamu wa uwepo wa mambo hayo. Kuigiza kwao vile ni ushahidi mwingine juu ya uwepo wa shughuli za Kichawi na Kiganga. Kule kupandisha kwa Waganga ni Majini yanakuwa yamemuingia Mganga na kuyaruhusu kusema masuala kadha wa kadha, Kabla sijamjua Mungu sawa sawa, niliwahi kupelekwa kwa Mganga mmoja kutokana na matatizo yaliyokuwa yakinisibu, kwa kweli nilishangaa sana jinsi ambavyo Mganga yule aliweza kuzungumzia kuhusu maisha yangu na kuzungumzia mambo yaliyofanyika Nyumbani kwetu wakati sikumsimulia chochote na wala hatukuwahi kufahamiana hapo awali, Leo hii baada ya kumjua Mungu, nimebaini kuwa yale yalikuwa ni Majini katika Ulimwengu wa Roho, Majini ni sehemu ya Ufalme wa Ulimwengu wa Roho. Shetani ana uwezo wa kufahamu chochote kuhusu Mwanadamu. Mambo yote yanayo fanyika katika Uganga na Uchawi ni masula ya Ulimwengu wa Roho. Hivyo huu pia ni ushahidi kuwa kuna maisha ya Ulimwengu wa Roho.

Mifano mingine ni ile ambayo umewahi kusikia kuwa Mchawi fulani alianguka kwa kuishiwa nguvu akiwa katika harakati zake za Kichawi. Je, umewahi kusikia juu ya kupigwa marufuku kuhusu Ramli chonganishi? Ile ni kazi mojawapo ya Kiganga/ Kichawi ila imetafutiwa jina zuri na kuitwa Ramli chonganishi. Ilitakiwa tu kuitwa kazi za Kichawi. Katika Mifumo yetu ya Sheria, suala la Kichawi halitambuliki kwa kile tu kuwa hauwezi kuthibitisha juu ya uwepo wa Uchawi kwa macho. Lakini masula haya yapo. Kwa msingi huo, huo ni ushahidi mwingine wa kuthibitisha masula yanayofanyika katika Ulimwengu ule usioweza kuonekana kwa macho, yaani Ulimwengu wa Roho.

KUTOLEWA/ KUFUKUZWA KWA MAJINI/ MAPEPO KATIKA MIKUTANO YA INJILI.
Mfano mwinginme ni huu, Je, umewahi kuona Katika Mikutano ya Injili namna ambavyo mapepo hukemewa na watu kuanguka na wengine kuanza kutamka maneno yanayoashiria kupagawa? Ile ni hali ambayo hudhihirisha Ulimwengu wa Roho pia. Kwa bahati mbaya sana Watu wengine husema yale ni maigizo au kupagawa Kisaikolojia. Sasa kama ni maigizo, iweje Ulaya, Marekani, Asia, South Afrika, Nigeria na kwingineko kote Waigize na matendo yote hufanana? Yaani uigizaji au matatizo ya Kisaikolojia yafanane Duniani kote.? Ni Chuo gani au mtu gani ambaye huwafundisha watu kufanya maigizo kiasi kile Duniani kote.? Hali ile ni halisi.Hii hutokea Makanisani na kwenye Mikutano ya Injili. Mie wakati nasoma Sekondari, wakati bado nilikuwa pia nina mashaka juu ya ukweli wa jambo hili, kulikuwa na kikundi cha Maombezi cha Wanafunzi wenzetu, basi siku moja kukafanyika Maombi ya pamoja wakaalikwa Wanafunzi wenzetu kutoka Shule moja ya Wasichana, Maombi yalipoanza tu, kuna Wanafunzi wadada wakaanza kupagawa na Mapepo na kuanza kujirusha rusha na kisha kuanguka chini kisha kuombewa na Mapepo yakafukuzwa na kuwaachia. Waliokuwa wakiendesha Maombi yale walikuwa ni Wanafunzi wenzetu, ingekuiwa ni Watu nisio wajua ningeendelea kuamini kuwa ni maigizo tu yaliyopangwa kama wasemavyo Watu wengine leo hii.

UHUSIANO WA UMISIONARI ENZI ZA UKOLONI NA UENEZI WA INJILI.

Fact nyigine ambayo baadhi ya watu husema kuwa hizi Dini tulizonazo yaani Uislamu na Ukristo ni Dini za Kiarabu na Kizungu, yaani zililetwa kwa mantiki ya kututawala enzi za Ukoloni, eti zilikuja ili kutupumbaza tu ili wakoloni wajichukulie Mali zetu Waafrika. Swali la kujiuliza, kama kweli Dini hizi ni Uongo na zilikuja ili kututawala,iweje na wao huko Ulaya, Asia, Amerika na kwingineko waendelee kushiriiki mpaka leo hii katika Imani hizo hizo tulizonazo huku Afrika. Nikupe tu taarifa kuwa, kwa sasa hata huko Ulaya, Marekani na Asia kuna Waafrika na wengine ni Watanzania wanashiriki kueneza habari za Mungu. Wengine hudiriki kusema kuwa Ukristo ni wa Wazungu. Huku ni kutojua Historia ya Ukristo. Ukristio haukuanzia Ulaya. Ukristo ulianzia Mashariki ya Kati yaani Israel, huko ndiko Chimbuko la Ukristo baada ya YESU KRISTO kuwako Duniani katika hali ya Kimwili yapata miaka 2017 sasa iliyopita.Yawezekana kweli baadhi ya Wamisionari waliitumia Dini kama sehemu ya kujitwalia mali za Waafrika, lakini Injili ya Mungu inaweza kuenezwa either katika hali ya Ubaya au Wema.

UHUSIANO WA ALAMA ZA TAIFA NA UDHIHIRISHO WA UWEPO WA MUNGU.
Tazama Wimbo wetu wa Taifa, maudhui yake ni kuomba rehema kwa Mungu, tazama Dua ya kuliombea Bunge, maudhui yake ni kumtaja Mungu aweze kuibariki Nchi na Viongozi wake. Tazama viapo vya Viongozi kuanzia Rais hadi Viongozi wengine. Viapo vyote vile hufanyika kwa kumuomba Mungu huku muhusika akiwa ameshika kitabu Kitakatifu kulingana na Imani yake. Yote hiyo ni kudhihirisha kuwa hata Nchi yenyewe inatambua uwepo wa Mungu. Sasa kama ndugu yangu wewe umezaliwa na kuikuta hata Nchi yenyewe inatambua uwepo wa Mungu, iweje wewe unayejiita msomi mwenye umri sijui wa mika 40 au 50 ukatae kuwa Mungu hayupo.? Wakristo tunaamini kuwa YESU alikuwapo miaka 2017 sasa iliyopita. Tangu hapo watu wamekuwa wakiamini kuwa YESUalikuwapo,ila wewe ndugu mwenye miaka 40, 50 au 60 unapinga mambo haya uliyoyakuta na kuwepo zaidi ya Miaka 2000 iliyopita. Bila shaka watu kama ninyi mnaopinga hamuwezi kukosekana, maana hata Israel aliko zaliwa Yesu mpaka sasa kuna Watu bado hawaamini kama YESU alishakuja na kwamba ndiye aliyetabiriwa tangu enzi za mababu zetu wa Imani kuwa atakuja Mwokozi wa Ulimwengu.

Mifano ipo mingi ila kueleza kwa uchache, kwa leo naomba kuhitimishia hapo. Lengo kubwa la andiko hili ni kuweka msingi mzuri wa wewe kuelewa na kuamini kuwa Yote yasemwayo kuhusu Mungu ni kweli na dhahiri. Baada ya andiko hili la Msingi, itafuatia maandiko mengine ya namna bora na sahihi ya kuweza kufahamu kwa nini tupo Duniani na ni nini Mungu amekusudia kuhusu Maisha ya Mwanadamu.

Kama andiko hili litakuwa sehemu ya Mwanzo wako mpya wa Maisha hasa katika kumuamini Mungu, basi tuungane pamoja kisha nitaandaa Ujumbe mwingine kwa ajili yako ili kukuongoza katika ile kweli kadiri Roho wa Mungu atakavyonijalia. Mungu akubariki sana na karibu tuendelee kujifunza kuhusu Mahusiano yetu na Mungu aliye muumba wetu.

Kuna maswali ma chache want to ask ,Sir !

1.hemu let's say kuwa unapozaliwa tu ,hatukufundishi dini yoyote mpaka unapofika umri wa miaka 18 or so ,then baada ya hapo tunakufundisha dini zote ,uislam,Christianity,judaism ,buddhism etc etc.After then tunakupa opportunity uchague dini ile ambayo ime make sense kwako regardless na imani ya wazazi wako ,je Are you sure kuwa Leo ungeendelea kuwa katika imani ambayo unayo sasa? Be honest !

2.Is faith reliable mecanism to truth ?

Kwamba ikiwa leo mimi ninasema " Black people are superior than white people ,and that is based on my faith " Are you going to believe that ? If not ,then how do you test or confirm your faith is not leading you to wrong conclusion ?

Kwamba ,ikiwa Leo unasema Christianity ni dini,fine ,but je hiyo kauli based on what ? Faith or facts and evidence to support that claim ? Kama ni based on faith ,then how do you know kuwa your faith is not misleading you?as the one who believes kuwa black are superior,? kwa sababu you can't judge something kwa kutumia imani yako,na hii ndiyo sababu muslims and Christians can't sit on the same table,Muslims want to judge Christianity based on Islamic faith ,and the opposite is exactly the same .

3.As you have just said kwenye post yako ,Kwamba almost hizi Semitic religions zote zimetoka Middle East ,Kwamba especially kwetu Africa came some people who claimed kuwa waliishi na mitume,so wametuletea ujumbe from God ,Think of it ,Sir ,how do you trust those people ? because hawakuwa mitume,neither malaika,sasa unaamini vipi kuwa hawaku distort the message ? Huoni kwamba kulikuwa na haja na sisi mungu kutuletea mitume wetu ,who came from our own culture,speak our own language,eat own food,kuna ugumu gani katika hilo as in God is everything? Yaani waje watu from Middle East and tell us what to believe,who are they ? How can I trust them na message zao zinazo contradict itself most of the time ,think of it .tuli deserve na sisi To have direct message from God and not from ordinary people .Many things kwenye dini zote don't make sense lakini tunatafuta njia zi make sense.Halafu unaambiwa kuwa hupaswi kuhoji sana mambo ya mungu ,Hell No.

—We Are here to learn ,therefore we must question everything claims to be true•
 
Kwanza kabisa, Mungu hana Dini. Dini ni utaratibu wetu Wanadamu tuliojiwekea na kujitenga makundi makundi kulingana na uhuru wetu wa kuamini. Lakini, kwa kuwa kumkomboa Mwanadamu ni mpango wake Mungu mwenyewe. Na kule kumjua Mungu wa kweli ni mpango wake Mungu mwenyewe, na ndio UKOMBOZI wenyewe, hivyo basi, sina shaka kuwa, hata kwa mazingira uliyosema katika swali lako, bado ningekuwa katika njia sahihi niliyopo sasa. Ushahidi mzuri ni huko Israel kwenyewe. Japokuwa ndiko chimbuko la UKRISTO, lakini kuna WAYAHUDI wasio amini kabisa kuhusu YESU. Mfano mwingine ni mimi mwenyewe, yaani IMANI niliyo nayo mimi, ni tofauti na IMANI ya Baba na Maya yangu. Wao wana IMANI zao, nami nina IMANI YANGU hii niliyonayo.

According to Google; Faith is defined as Follows....
  1. complete trust or confidence in someone or something.

  2. strong belief in God or in the doctrines of a religion, based on spiritual apprehension rather than proof.
If that is the case; How comes to have faith on your own mind.? Faith must base on something else... Empty headed Person can't have faith on anything, since, His/Her mind is empty.

Refer the explanations above.!

Umeongea mambo mengi hapa, lakini, unatakiwa kuelewa kuwa Mungu ana utaratibu wake wa namna anavyoona inafaa yeye ajulikane kwa Wanadamu. Usimfikirie Mungu kwa utashi wa akili zako tu. Ipo wazi katika BIBLIA kuwa, iliamriwa INJILI ienezwe MATAIFA yote. Kwahiyo namna inavyoenezwa INJILI ni mpango wake Mungu mwenyewe. Kila kitu kina mwanzo, baada ya mwanzo kinaongezeka. Ndio maana hata Mungu aliumba Mtu Mke na Mtu Mme, kisha akaweka mechanism ya namna ya Watu kuongezeka. Mbona hauhoji kwa nini Mungu hakuumba Wanadamu wote kwa wakati mmoja.? Kwahiyo, hata ujumbe wa Mungu una mwanzo wake, kisha unaendelea kusambaa zaidi, maana ndiyo mechanism aliona Mungu inafaa. Vilevile, unatakiwa kufahamu kuwa, si kila anayejiita MKRISTO ni mcha Mungu. Kuwa Mcha Mungu ni neema kubwa sana ambayo siyo kila mtu anayo. Ukiwa mcha Mungu sisi tunaamini kuwa unakuwa na Roho wa Mungu ndani yako. Then unakuwa tofauti na Wanadamu wengine wasio wacha Mungu. Endapo utaendelea kufuata taratibu za Mungu hali ya ucha Mungu inakuwa ndani yako kila wakati, unajihisi kabisa kuwa watofauti. Wenye Roho wa Mungu wanajifahamu kabisa hali walizo nazo. Wanakuwa na hali ya kupenda kutenda wema, kutokuwa na hasira, kutokuwa wachoyo, kutokuwa wakorofi, kupenda kuomba Mungu kila wakati, kuwapenda na kuwajali Wanadamu wengine. Hali hizi zote, si kila Mwanadamu anazo. Ni mpaka Roho wa Mungu awe ndani yako. Huwezi tu kusema hutaki uasherati, hutaki kusema uongo, hutaki kuwa mnafiki etc. There must be a certain Power in you. That Power comes from God himself.

Sure, I conquer with you.!
 
Not convinced .

Bado unachoelezea ni your personal faith and experience,ndiyo maana you end up kwa ku quote from Bible .

"Faith " ndiyo tatizo hapa.
Nataka utoke nje ya imani yako and then answer my questions.
 
I'm not here to convince you, I have done my part to disclose the truth on Public Politely as supposed to be. Who consider and follow the way, is beyond my duty. We don't fight with people to make them considerate of the truth on God.

Principle we consider is "To disclose the WORDS on Public as much as We can". If you believe, take them for your own SALVATION. If You don't believe, then, Leave them. Each of Us will be accountable on his/herself at the End, accordingly.
 
Mleta uzi ukiweza kujibu hoja zako zote nje ya biblia ndo utajua mambo mengi kuhusu mungu na usipojizuia sikio lako kupokea idea mpya utajua wanaokataa mungu wa kutoka asia wana nia gani
U cant answer what happen out of box while your still in box itakua crayzest
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom