Chapter 001: Maana/Tafsiri ya kuota kufa, maiti na yanayoambatana na mazishi

Je ukiota upo na mtu ambaye alishakufa lakini kwenye ndoto unamuona hajafa mpo kama zamani maanake nn?
 
Mbona matokeo yake hayana deadline?

Inamaana hata kama nimeota Leo likaja kutokea baada ya miaka 40 sa kuna faida gani ya ubashiri?
 
walivyo anza kukudukua na ww ulikua unaota hivyo, ..?? maana rafiki yangu ndo analo hillo tatizo, kama walianza hivyo nambie nmshauri awai maombi asije kua gwiji la kudukuliwa kama ww
Hahaha ah hapana don't take it serious, muulize last time aliota kitu gani , halafu dalili za kudukuliwa rejea Uzi utaalam wanaotumia wachawi katika kuumiza watu.Hapo utaweza kuona namna gani wanafanya .
 
Je ukiota upo na mtu ambaye alishakufa lakini kwenye ndoto unamuona hajafa mpo kama zamani maanake nn?
Inaonesha maisha yake huko alipo namna alivyo, unajua sababu ya kifo chake? Halafu mavazi anayojitokeza nayo usingizini yakoje chakavu au mapya?
 
Ukiota umelala mara inaingizwa maiti ndani chumbani ulikolala na inalazwa kitandani ulipolala na unaiona kama ni mtu uliyekuwa unamfaham ila hujumbuki ni nani, na hapohapo anafumbua macho kama kafufuka vile, maana ya hii ndoto ni nini?
 
Ukiota umelala mara inaingizwa maiti ndani chumbani ulikolala na inalazwa kitandani ulipolala na unaiona kama ni mtu uliyekuwa unamfaham ila hujumbuki ni nani, na hapohapo anafumbua macho kama kafufuka vile, maana ya hii ndoto ni nini?
Umesoma lakini Uzi wote au ulisoma heading tu ,nahisi kama nimeeleza au kama hayo maelezo hayo directly basi ukimaliza kusoma Uzi wote chapter 001 utaweza kufaham hio maana
 
Chapter 003: Tafsri/ maana ya kuota harusi na yanayofungamana nayo katika tendo la ndoa.
Atakae ota usingizini kuwa amekuwa bwana harusi lakini hakumuona bibi harusi wala hamjui wala hajanasibishwa nae basi maana yake atakufa au ataua mtu na atatolewa ushahidi mahakamani.
Na atakaeota ameoa atapata uongozi kwa kiwango cha uzuri wa yule mwanamke ambae amemuoa na ubora wake na maana ya jina lake.
Atakae ota amefanya tendo la ndoa na mwanamke maarufu basi maana yake familia yake itapata manufaa ya kidunia.
Na atakaeota au akaotwa na mtu mwengine kuwa yeye amemuoa mama yake au dada yake au yoyote katika familia yake maana yake ni kuwa ataitelekeza familia yake na wala hatowajua kwa lolote.
Anatakae ota anambusu mwanamme pasi na kumbusu kwa matamanio maana yake mfanyaji atapata manufaa kutoka kwa aliefanyiwa .
Na mwanamme akiota kuwa yeye ni mjamzito mana yake kuwa atapata manufaa ya kidunia.
Atakae ota amezaa mtoto wa kiume maana yake atapata depression na atakaeota amezaa mtoto wa kike maana yake atapata raha. Vile vile atakaeota amenunua mtoto wa kiume au wa kike.
Na atakae ota amefunga ndoa na mnyama maarufu basi atapata manufaa sehemu ambayo hana haki nayo au ambayo hajaajiriwa.
Na atakaeota amefunga ndoa na maaiti maarufu maana yake maaiti atapata manufaa kutoka kwa yule aliemuoa.
Na mwanamke alie katika ndoa akiota ameolewa na mwanamme mwengine atapata mambo mazuri na atapata uheshimiwa.
Na mwanamme alie katika ndoa akiota ameoa mwanamke mwengine basi atapata uongozi.
Na atakae ota mkewe yupo katika piriadi basi maana yake huyo mwanamme mambo yake yatafungika.Na akiota kuwa amejamiana nae na hali yakuwa yupo katika hali hio basi mambo yake yatakua mepesi.
Ama tendo la ndoa katika ndoto maaana yake ni kufikia upeo wa jambo ambalo binaadamu analitafuta katika dunia.
Na atakae ota amemuoa mwanamme mwenzake ikiwa mwanamme alieolewa ni kijana basi muotaji atashinda kwa adui anaemuwinda. Na atakae muoa akiwa mtoto basi atafanya yale ambayo hayampasi yeye kufanya na atabebeshwa mzigo wa matatatizo.
Na atakaeota amekuwa gay maana yake atapata mfazaaiko na huzuni.
Na mwanamme akiota ametazama au kugusa uchi wa mwanamke maana yake atafanya biashsra yenye kuchukiza.
Ama liwati wapo waliosema maana yake ni kushinda zidi ya adui na wapo waliosema mfanyaji atafilisika.
 
Back
Top Bottom