Muhindila
Member
- Jul 12, 2015
- 46
- 30
Licha ya rais wetu kuonesha jitihada mbalimbali katika kuiletea maendeleo nchi yetu, wapo wengi wanoonesha kutokuunga mkono jitihada hizo na hata kubeza, mfano mzuri ni hili suala la mchanga wa madini, kila siku tulikuwa tukilalamika hujuma tunazofanyiwa na haya makampuni yanayojihusisha na uchimbaji na usafirishaji wa madini mpaka ikaonekana tutaachiwa mashimo tu bila kufaidika na hii rasilimali hadimu kabisa. Leo hii rais wetu anaonesha njia na jitihada za kuhakikisha madini yanatunufaisha, watu tunabeza jitihada hizo. Kuweni wazalendo si kubeza kila kitu, tuungane na rais wetu kuhakikisha tunalipeleka taifa mbele