Chanzo na kumarizika kwa vita baridi kutoka mwaka 1947 - 1991.

Raphael phockus

JF-Expert Member
Nov 4, 2018
778
4,518
Habari ya muda huu wanajanvi.


Kama mada inavyo jieleza hapo juu, baada ya vita kuu ya pili ya dunia (WW ll) kulishuhudiwa mgogoro mkubwa wa kidiplomasia
baina ya Umoja wa kisoviet , Marekan na washirika wake yaani mataifa ya ulaya ikiwemo uingereza (the late Great Britain).
Ungana nami Alseneta Sir...........


Tishio la nyukilia na pingamizi la siasa za Usoviet.

Kutoka mwaka 1947 - 1953 ulikuwa ni mwanzo wa vita hii baridi baina ya muungano wa Usoviet pamoja na Marekan na washilika wake . Aidha vita hii ilipelekea kumarizika kwa vita ya Korea (Korean war) mwaka 1953.
Mwaka 1947, milionea Bernard Baruch aliekuwa mshauli wa Raisi wa Marekani ( Woodrow Wilson na Franklin Roosevelt ) katika maswali ya kiuchuni na kijeshi. Alipendekeza mpango wa kudhibiti nguvu ya nyukilia lakini Umoja wa kisovieti ulipinga mipango hiyo kwa madai kuwa Marekan nayeye anasiraha za nyukilia hivyo kupelekea mwanzo wa mvutano kati ya umoja wa Usoviet na Marekan.




View attachment 1131730




picha; Bernard Baruch mushauli wa maswala ya kijeshi mwaka 1953's

Aidha sababu nyingine iliyopelekea mwanzo wa mgogoro huu ni pale Marekan na Uingereza walipo pingana na siasa za Umoja wa kisoviet mwaka 1945 - 1946.



Kifo cha Joseph Stalin mwaka 1953.



View attachment 1131729



Kufuatia kuuwawa kwa kiongozi dikiteta (Joseph Stalin) ambaye aliongoza umoja huo kutoka mwaka 1928 hadi kifo chake mwaka 1953. Hivyo kupelekea mgogoro wa vita kati ya mataifa hayo hasimu.
Hata ivyo mgogoro wa Cuba ( The October Crisis Of 1962 ), mgogoro uliodumu kwa takilibani siku
kuminatatu ( 13 ). Ulikuwa ni mvutano wa kijeshi kati ya Marekan na Umoja wa kisoviet ambao ulipelekea Marekan kugundua uwepo wa makombora ya Ballistic ya Usoviet nchini Cuba . Aidha mvutano huu ndo ule uliopelekea dunia kutabili uwezekano mkubwa wa kutokea vita ya nyukilia duniani kati ya Marekan na Umoja wa kisovieti.



Kuvunjika kwa makubaliano ya kusitisha vita mwaka 1962 - 1979 " The Détente "


Baada ya kumalizika mgogoro wa Cuba mwaka 1962 , Marekan na Umoja wa kisoviet walisaini makubaliano ya kusitisha tishio la vita mwaka 1969 kupitia makubaliano yaliyo julikana kama "Détente".

Hata ivyo makubaliano hayo yalivunjika baada ya kutokea vita Kati ya North Vietnam (ambayo iliungwa mkono na Usoviet pamoja na Uchina ) na South Soviet ( ambayo iliungwa mkono na Marekan, Korea ya Kusini na washilika wengine ) .
Hivyo kupelekea mataifa hayo kurudi katika kipindi cha vita baridi kwa mara nyingine tena.

Aidha makubaliano ya Détente halihusisha makubaliano kama vile " Partial Test Ban Treaty " ya mwaka 1963 yakiwa na rengo la kutokomeza siraha za nyukilia.
Baadae January mwaka 1967 kulisainiwa makubaliano yaliyojulikana " Outer Space Treaty " yakiwa na rengo la kuweka sheria za pamoja katika shuguri za anga, na " Nuclear Non - Proliferation Treaty " ya July mwaka 1968 yaliyo kuwa na rengo la kudhibiti kusambaa kwa siraha za nyukilia pamoja na tekinolojia ya nyukilia.



Vita ya Afghanistan na shambulizi la ndege ya Korea Air Line 007.


Mapinduzi ya " Saur Revolution " ( Kwa maana nyingine yalijulikana kama "April Revolution" ) ambayo yaliongozwa na PDPA ( People Democratic Party Of Afghanistan ) dhidi ya utawala wa aliekuwa Raisi wa wakati huo "Mohammed Daoud Khan" April 1978. Kutokana na mapinduzi hayo kulipelekea Umoja wa kisoviet kuivamia kivita Afghanistan mnamo mwaka 1979.



View attachment 1131814





View attachment 1131817







Picha; Soviet wakati wa uvamizi wa kivita huko Afghanistan.


Kutokana na uvamizi huo wa kivita dhidi ya Afghanistan kulipelekea Marekan kuingilia vita hiyo iliyo pelekea umoja wa kisoviet kushindwa hivyo kuongeza mvutano na kujenga taswira mpya ya vita ya nyukilia , awamu hii mvutano ulikuwa mkubwa kuzidi ule wa 1962.
Shambulizi la ndege ya kiraia ya shirika la Korea ya Kusin mwaka 1983 kulipelekea Umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi yaani NATO kufanya zoezi kubwa la kijeshi lililo julikana kama " Able Archer 83 " .
Hivyo kuongeza tishio la mashambulizi ya nyukilia kwa Umoja wa kisoviet kutoka kwa majeshi ya NATO, jambo lililo pelekea alarm ya hatari kwa Umoja wa kisoviet na hivyo kujenga wasiwasi mkubwa wa dunia kutumbukia kwenye vita ya nyukilia.




View attachment 1131823





Picha; ramani ya CIA ikionesha mwelekeo na njia ya Ndege ya KAL 007.




Mgogoro na kumarizika kwa vita baridi mwaka 1985 - 1991.



Baada ya mwaka 1985 na kushindwa kwa Usoviet katika vita ya Afghanistan , ulikuwa ni mwanzo wa kumarizika kwa vita baridi baina ya Marekan na Usoviet.
Makubaliano ya December 1987 yaliyo julikana kama " Intermediate - Range Nuclear Forces Treaty " ( INF ) yakiwa na rengo la kuondosha siraha za nyukilia na makombora yenye uwezo wa kulenga hadi kilomita 500 kwa 1000 ( Makombora ya masafa mafupi ) na ( 1,000 - 5,500 ) makombora ya masafa marefu na munamo mwaka 1991 uchunguzi kukamilika kwa pande zote mbili takiribani makombora 27,000 yalikuwa yamesha haribiwa hivyo kupelekea kumarizika kwa vita baridi baina mahasimu wawili wakubwa yaani Marekan na Umoja wa kisoviet.




View attachment 1131827




Picha; Mikhail Gorbachev ( Raisi wa Soviet Union ) na Renald Reagan ( Raisi wa Marekan ) ,wakisaini mkataba wa INF.



Hitimisho.

Aidha kuvunjika kwa muungano wa Soviet munamo mwaka 1991 Ilikuwa ni sababu kubwa ya kumarizika kwa vita baridi kutokana na mahusiano mazuri kati ya Gorbachev na Mikhail .Bwana Gorbachev analaumiwa sana na watu nchini Urusi kwa kuvunja muungano wa Usoviet lakini pia anaonekana kama shujaa aliye saidia kumarizika kwa vita baridi.



By Alseneta Sir.
 
Back
Top Bottom