CHANZO, MADHARA NA JINSI YA KUONDOA KITAMBI

IKWETA KONZO M

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2013
Messages
616
Points
1,000

IKWETA KONZO M

JF-Expert Member
Joined Oct 3, 2013
616 1,000
Kitambi ni mkusanyiko wa mafuta na takamwili zisizohitajika katika mwili wa mwanadamu. Katika hali isiyo ya kawaida mwili wa binadamu huanza kuhifadhi mafuta katika sehemu mbalimbali kutoka kwenye vyakula vinywaji na hata vilevi hasa vyenye ngano.
Zipo hatua kadhaa za mwili kutengeneza kitambi ambapo kwa kawaida huwa ni vigumu kwa wengi wetu kutambua.

Binadamu mwenye afya njema hupaswa kuwa na uwiano sawa kati ya urefu na uzito ambao hupimwa na kubainishwa na kipimo kiitwacho body mass index (BMI). Licha ya vipimo mbalimbali kutumika kama mzingo wa kiuno, umri n.k.
Kipimo cha BMI hulenga kuonyesha iwapo kama mtu yupo chini ya uzito, ana uzito sahihi, anauzito uliozidi au ana kitambi.
*Mfano.*
•BMI kuanzia 0-18.4. huonyesha chini ya uzito (Underweight)
•BMI kuanzia 18.5-24.9 uzito sahihi (ideal/normal weight)
•BMI kuanzia 25-29.9 uzito uliozidi (overweight)
•BMI kuanzia 30+ obesity
Ili kufahamu uwiano wako unaweza kupima urefu wako kisha badilisha kutoka metre au futi kwenda sentimetre na utoe 100 kinachobaki ndio uzito wako sahihi au tumia kipimo cha BMI CALCULATOR katika simu yako

*SABABU NA CHANZO CHA UZITO.*
Zipo sababu nyingi zinazosababisha mtu kuwa na uzito mkubwa huku nyingi zikiwa ni za kijamii, kibiolojia na kimazingira. Baadhi ya tafiti zinabainisha kuwepo na waathirika wengi watokanao na mifumo mibovu ya maisha yaani (poor life styles). Ulaji wa ovyo, kutokunywa maji mengi, kutofanya mazoezi utumiaji pombe na vinywaji vya ngano, sukari ndio sababu kuu ya ongezeko la unene. Takribani asilimia 70 ya watu waishio mijini huanza kufuga seli za unene toka utotoni huku wengi wakianza kuwa wanene kipindi wakianza kubadili hali za maisha yao kiuchumi.
Kwa mfano ulaji wa vyakula vya wanga iliyokobolewa, mafuta mabaya, sukari, ngano, chumvi ya kuongeza huweza kubadilishwa na kuwa mafuta. Hali hii hulazimu mwili kuanza kuyahifadhi kama ziada ya chakula cha badae. Mafuta haya yakiendelea kuhifadhiwa huweza kuzingira viungo mhimu kama moyo, figo, ini, kongosho ili kuviepusha na shambulio la sumu na kemikali mbalimbali (free radicals). Mazoezi hufanya utendaji kazi wa mwili kuwa thabiti, moyo kufanya kazi vizuri, ngozi kutoa sumu, misuli kuunguza mafuta vizuri na kufanya mfumo wa usagaji chakula kufanya kazi vizuri. Pia tatizo la kutokunywa maji kwa wingi hupelekea chakula kuganda ndani ya utumbo kwani chakula huhitaji maji mengi ili kulainishwa licha ya kemikali na unyevu uliopo mwilini na figo kupatwa na mawe

Sambamba na mfumo wa maisha lipo tatizo la kuwa na sumu nyingi mwilini kutoka kwenye nafaka zilizohifadhiwa kwa dawa, mboga, matunda, madawa tunayotumia kujitibia, vilevi, vinywaji vya viwandani, hewa, mioshi ya magari, viwandani na vumbi ambapo mwili hulazimika kuzalisha mafuta ili kuzuia athari zitokanazo na sumu. Zipo sababu za kibiolojia kutoka kwa baadhi ya familia kuwa na vinasaba vya unene (genes) japo wataalam wanabainisha ni kurithishana life style mbovu katika maisha kwani katika karne hii watu wengi wanakumbana na mlolongo wa ulaji usiozingatia afya. Sumu huchosha figo, ini, kinga ya mwili kuharibu utendaji kazi wake.

Utumiaji wa njia za kuzuia mimba kwa akinamama huweza kuvuruga vichochezi yaani homoni na kusababisha mzunguko wa hedhi kuharibika hali ambayo hupekekea uzito kuongezeka.
Mimba na malezi ya mtoto, katika hali isiyo ya kawaida wanawake hujikuta wakiwa dhaifu kipindi cha ujauzito na kuifanya miili kujenga mafuta kutokana na kupendelea aina ya vyakula fulani huku muda mwingi wakiwa nyumbani, baadhi yao huongezeka uzito mara tu baada ya kujifungua kutokana na kubadili ulaji ili kuruhusu mtoto apate maziwa na lishe iliyokamilika, kutumia muda mwingi kukaa na kupumuzika. Kufanyiwa upasuaji, homoni,na hata kuwa na matatizo ya viungo kama miguu kuuma au kuvunjika ni moja ya sababu za kuongezeka kwa uzito.


*DALILI ZA UNENE ULIOZIDI*.
~zinazoonekana(physical)
»Tumbo la chini kuanza kuning'inia
»Kuota matiti kwa wanaume
»Kutokwa na michirizi (stretch marks)
»Kushindwa kuona sehemu za siri ukiwa umesimama
»Miguu kuvimba

~Zisizoonekana (invisible)
»Moyo kwenda mbio
»Kuchoka ovyo
»kuhema mara kwa mara japo wengine ni kutokana na kutifanya mazoezi
»Ganzi ya miguu na mikono sababu ya damu kushindwa kusafiri vizuri

*MADHARA YA UZITO*.
Uzito na kitambi huweza kusababisha madhara mengi na makubwa katika maisha yetu. Vipo vifo vingi visivyo rasmi hutokea pasipo jamii kutegemea na kuwapoteza wapendwa wetu sababu ya uzito mkubwa. Yote haya ni kutokana na mafuta kuzidi na kuibana mishipa ya damu ipelekayo chakula, oxygen na hata damu katika sehemu mbalimbali za mwili. Kushindwa kwa mishipa hii kutanuka vizuri hupelekea hitikafu katika vishipa vidogo vya ubongo au moyo na kupasuka hivyo mtu huweza kupata kiarusi (stroke au heart attack). Ongezeko la sukari katika damu huathiri utendaji kazi wa kongosho na kushusha uzalishaji wa insuline kemikali mhimu katika kuweka uwiano wa sukari hatimaye kusababisha kisukari aina ya 2.
Kwa ufupi madhara ya unene ni kama
-Kisukari
-shinikizo la juu la damu
-kuathirika kwa mfumo wa usagaji chakula kutokana na mafuta kuganda katika tumbo
-kuathirika kwa mfumo wa uzazi wa mwanamke na kupelekea kushindwa kushika ujauzito
-kusagika kwa pingili za uti wa mgongo na kusababisha tatizo la mgongo
-Kuathirika kwa nerves
-Kuchangia tatizo la tezi kukua kwa kasi
-miguu kuvimba na kupelekea ulemavu usio rasimi

*JINSI YA KUONDOA KITAMBI*.

Kama ilivyo katika shughuli zetu za usafi wa kila siku majumbani kupitia hatua kadhaa hata miili yetu huhitaji utayari na mpangilio ulio sahihi ili kuondokana na unene. Watu wengi hufikiri kuwa na afya njema ni jambo jepesi rahasha ni lazima ujitoe kwa kupenda usivyovipenda na kuchukia unavyovipenda. Afya njema huuanza na wewe kwa kuzingatia fomula ya (H+3Ws) yaani
HOW YOU LIVE,
WHAT YOU EAT
WHICH AMOUT YOU EAT
WHEN YOU EAT.
Kwani yapo makundi kadhaa ya vyakula na yote ni mhimu kuzingatiwa na kuangaliwa kwa ukaribu mfano, wanga, vitamins, proteins, mafuta, madini. Vyote hivi hutakiwa kwa kiwango fulani kwa siku (daily allowance). Inashauriwa kula kiwango ambacho mwili unaweza kutumia pasipo kuruhusu kubakisha hifadhi ya mafuta mengi. Epuka ulaji wa nafaka zilizokoborewa kwani hukaa sana mwilini na huweza kubadilishwa kuwa mafuta na sukari kwa haraka.

Yapo maswali matatu mhimu kujiuliza kila unapotaka kudhibiti uzito wako. Maswali haya yatakupa mongozo sahihi na kuweza kutimiza lengo lako.
1.Kwanini unanenepa (wewe)?
2.Kwanini unataka kupungua(wewe)?
3. Njia gani sahihi isiyoathiri afya yako ungependa uitumie?

Kabla hujaanza safari yako ya kupungua ni mhimu sana kufahamu chanzo cha tatizo kwani huwezi kufanya marekebisho kabla hujajua kosa, baada ya kufahamu chanzo ni mhimu pia kufahamu sababu gani inakusukuma kupungua, huenda ni afya yako na familia, huenda ni monekano mzuri, huenda ni ufanisi kazini, huenda ni kutojisikia vizuri sababu marafiki na ndugu wanakushangaa lakini ifanye sababu hii itoke ndani mwako kwani (internal reason is so powerful). Ni mhimu pia kuchagua njia sahihi kuli gana na mazingira, afya yako, uzito wako na ufahamu wa njia hizo. Zipo njia kadhaa ambazo wengi hutumia aidha kwa kufuata ushari wa madkatari, wataalamu wa lishe au marafiki. Hebu fuatilia njia hizi 3 hapo chini...

Mtaalamu mmoja aliwahi kusema "There must be power to start, to continue and to finish".
1)Kula kwa usahihi, kunywa maji ya kutosha na kufanya mazoezi. Njia hii hutumika na kila mtu bila kujali afya yako lengo ni kuepuka unene usiohitajika.

2).Diet.njia hii inahusisha kuacha au kupunguza baadhi ya vyakula na kuendeleza aina fulani ya chakula.
*Health diet. Hii ni aina ya diet inayofuata ushsuri wa wataalam wa lishe na afya.
*Unhealth diet. Hii hutumiwa na watu kwa kushauriana pasipo kuwa na elimu sahihi na hatimaye kupelekea madhara kiafya mfano madonda ya tumbo, kuzimia, kupungukiwa damu na ngozi kuchoka.

3) Virutubisho. Njia hii ni ya kisasa ambayo inashauriwa kutumika na mtu yeyote anaehitaji kudhibiti uzito kwani huweza kumpitisha mtu katika hatua mhimu sana mfano kuondoa sumu na takamwili, kusafisha utumbo, kuunguza mafuta, kujenga misuli na hatimaye kupunguza uzito na kuweza kubakia na uzito sahihi (maintenance). Njia hii itakupa utaratibu wa ulaji, ufanyaji mazoezi, unywaji maji na mengine mengi. Kwa kuwa ni virutubisho husaidia mifumo yote ya mwili kufanya kazi vizuri huku mwili ukizidi kupungua.


Moja ya bidhaa ambazo ningependa nikushauri uzitumie kulingana na ubora wake na kutumia kwa miaka takribani 40 ni C9 na F15 programs.

Programu hizi zina muunganiko wa bidhaa tofauti ambazo kwa pamoja husaidia mwili kupungua.

I.ALE VERA GEL
Hiki ni kinywaji ambacho hufanya kazi ya kusafisha uchafu katika mfumo wa chakula ili kutoruhusu mabaki kuathiri utoaji taka, kitendo hiki huweza kusaidia mwili kitokuwa na uchafu unaoweza kuongeza uzito.
Kinywaji hiki husaidia kuondosha sumu mwilini (free radicals) ambazo ndicho chanzo kikubwa cha mwili kuzalisha mafuta. Mwili kuzalisha mafuta ili kuzuia sumu zisiathiri viungo mhimu kama moyo, figo, INI,mapafu n.k. kuupa mwili lishe kama vitamins, madini.

II. GARCINIA PLUS .
Hii ni moja ya bidhaa mhimu katika zoezi la kupunguza uzito kwani, husaidia kubadili mafuta kuwa nishati hivyo kusaidia mwili kutohitaji chakula kingi toka nje. Husaidia kuratibu hamu ya kula (appetite suppression) lengo ni kuruhusu hifadhi ya mafuta mwilini kutumia kama chakula na nguvu.

III. THERM.
Hii ni bidhaa mhimu katika mwili husaidia kuongeza joto la mwili kwa asilimia 1% ili kuruhusu mafuta yaliyoganda chini ya ngozi kuyeyushwa. Kupitia mfumo uitwao thermogenesis therm huchukua mafuta na kuyapeleka katika seli za misuli ili yaunguzwe. Bidhaa hii huongeza ufanisi ikitumika pamoja na mazoezi ya viungo.

IV. FIBER
Ni moja ya nyuzi nyuzi zilizopo katika mfumo wa unga ili kurahisisha umeng'enywaji katika mwili. Fiber husaidia afya ya mfumo wa usagaji chakula, kuweka uwiano sawa wa bakteria katika mwili, kusaidia utoaji taka mwili kwa njia ya haja kubwa.

V. ULTRA LITE VANILLA.
Ni lishe na protein mhimu kupitia kiasi kwani ni moja ya chakula cha misuli hivyo husaidia misuli kuwa imara ili kuwezesha mafuta kuunguzwa na seli. Pia hutumika kama mbadala wa chakula wakati wa kupunguza. Pia husaidia kuupa mwili Nguvu na lishe sahihi.
Huchukua muda mfupi kutumiwa na mwili.


Nani atumie? Mtu yeyote isipokuwamama mjamzito na anae nyonyesha

HAWA NI BAADHI YA WATU WALIOAMUA KUTUMIA BIDHAA ZETU NA KUPATA MATOKEO MAZURI PAMOJA NA MWONEKANO SAHIHI.
usingoje kusimuliwa kwani ni wakati sahihi kwako kubadili afya yako na mwonekano wako.

Inafaa kwa wenye uzito mkubwa na wameshindwa kupungua kutokana na miguu kuvimba au kuuma, wenye changamoto za kiafya kama nerves na mgongo, operation, walipo bize na majukumu ya kila siku na kukosa muda wa kutosha kufanya mazoezi.
 

leipzig

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2013
Messages
2,750
Points
2,000

leipzig

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2013
2,750 2,000
Umetoa elimu yenye manufaa sana lakini hapo kwenye matangazo ya biashara ndio sijaelewa.

Hata hivyo hizo bidhaa nitazipataje? Matumizi yake ni ya mfululizo kila siku mpaka utakapopata matokeo chanya?
 

Forum statistics

Threads 1,344,367
Members 515,441
Posts 32,817,581
Top