Chanzo cha vurugu za zanzibar chaanikwa na mkuu mmoja serikalini!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chanzo cha vurugu za zanzibar chaanikwa na mkuu mmoja serikalini!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by lybenito, Oct 30, 2012.

 1. l

  lybenito Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  UKWELI KUHUSU UTEKWAJI WA SHEIKH FARID - ZIMEPATIKANA KUTOKA KWA MNENE MMOJA SERIKALINI

  Ukweli ni kwamba kuna viongozi wa juu kwenye serikali ya Zanzibar ambao kwa kushirikiana na Idara ya Usalama wa Taifa ya Tanzania wanahusika moja kwa moja kwenye machafuko ya Zanzibar kuanzia yale ya kwenye uchaguzi mdogo wa Bububu hadi haya ya sasa. Lengo kubwa ni kuhakikisha kwamba ajenda ya Wazanzibari kudai mamlaka kamili kupitia mchakato wa Katiba Mpya inashindwa kwa kuiua kabisa serikali ya Umoja wa Kitaifa na Maridhiano. Makubaliano ya pamoja kati ya Dodoma, kundi la vibaraka wao kwenye GNU na CCM Zanzibar na Idara ya Usalama wa Taifa, ni kwamba Maridhiano yaliyozaa GNU ndio adui nambari moja wa mfumo wa Muungano uliopo. Sasa ili kuulinda mfumo huu wa Muungano, ni lazima kumuangamiza adui huyo.Na ndicho kinachofanyika sasa.

  Tukio la kutekwa kwa Ustaadh Farid lilikuwa la kweli na lilikuwa ni sehemu ya programu hiyo kubwa ambayo inagharimu mamilioni ya fedha za walipa kodi wa Tanzania nzima na si wa Zanzibar peke yake
  . Kiasi cha mwezi mzima kabla ya Ustaadh Farid kutekwa, kijana mmoja wa Idara ya Usalama wa Taifa anayefanya kazi Zanzibar, alijenga mahusiano makubwana viongozi wa juu wa Uamsho, hasa Sheikh Farid. Kijana huyu, ambaye hakujificha kwamba ni mtu wa Usalama wa Taifa,alijitokeza kama sehemu ya kundi la watu waliomo kwenye taasisi za dola na ambao wanaunga mkono Ajenda ya Zanzibar. Kwa maslahi ya ajenda hiyo, na kwa maslahi ya Zanzibar, bahati mbaya viongozi wa Uamsho walimuamini. Ni yeye ndiye aliyekuwa mtu wa mwanzo kabisa kumpigia simu Sheikh Msellem saa 2:00 usiku wa siku ya kutekwa kwa Imamu Farid,kumjuulisha kwamba Usalama wa Taifa wamemkamata Sheikh Farid.

  Ndani ya siku tatu za sintofahamu hiyo, ni yeye aliyekuwa akiwashinikiza viongozi wa Uamsho na vijana kwamba ni lazima shinikizo kubwa lifanyike kama kweli wanataka kiongozi wao aachiwe akiwa salama. Kwa hakika, siku ya pili yake aliwasiliana na kukutana na Sheikh Msellem, na kumuambia kwamba alikuwa tayari kumpeleka aliko Sheikh Farid. Baada ya kuingia kwenye gari, hakumpeleka kwa Sheikh Farid,bali alimwambia kwamba wazungumze naye kwa simu kwanza, akiwa tayari ameshaipiga simu hiyo, kwa alivyosema.

  Kwenye simu, ni kweli Sheikh Msellem alisikia sauti ya Sheikh Farid ikimuambia kwamba ametekwa na wanamtesa, na kwamba kama hawakujikaza basi wanaweza hata kumuua. Alipotaka kuuliza mengi zaidi, Sheikh Msellem hakuweza maana ile simu ilikatwa. Kumbe kilichokuwa kimefanyika, ni kuwa Sheikh Msellem alisikilizishwa sauti ya kurekodi ya Sheikh Farid na hakuwa anazungumza naye moja kwa moja. Ilikuwa ni baadaye sana, viongozi wa Uamsho walipokuja kung’amua hayo.

  Ndani ya kipindi hicho cha kupotea kwa Ustaadh Farid, viongozi wa serikali ya Zanzibar wanaohusika na programu yao, waliyatoa makundi ya vijana wao kuchoma maskani za Kisonge, kuharibu mali, kuiba, kupiga,kujeruhi, na hata kuua. Katika purukushani hizo, vijana hao walikuwa wakipigana na kuumizana wenyewe kwa wenyewe. Miongoni mwao ni askari aliyepigwa risasi na kuuawa na wenzake, lakini huyo hatajwi kabisa na vyombo vya habari,badala yake anatajwa askari aliyeuawa Bububu kwa kukatwa mapanga, na ambaye huenda kabisa asiwe na uhusiano na matukio haya.

  Miongoni mwa vijana walioumizwa wako waliojeruhiwa vibaya na ambao hadi sasa wamelazwa kwenye hospitali ya jeshi ya Bububu, lakini taarifa zao zimewekwa siri sana. Kilichotokea, ikiwa ni sehemu ya programu hiyo kubwa, ni kwa Idara ya Habari Maelezo ya SMZ kutoa agizo kwa vyombo vyote vya ndani vya habari kutokutangaza kabisa matukio ya sasa, tangu kukamatwa kwa Sheikh Farid. Kwa hakika, hata katika kamatakamata ya polisi, nao pia wamewakamata vijana kadhaa wa makundi hayo lakini huwa wanawaachia kwa amri ya Kamishna Mussa Ali Mussa, Mkuu wa Jeshi la Polisi la Zanzibar, ambaye ni sehemu ya programu hiyo ya kuivunja GNU.

  Sheikh Farid aliachiliwa baada ya uingiliaji kati viongozi wawili wajuu GNU, kwa kuanzia na Makamo wa Kwanza wa Rais Seif Sharif ambaye baada ya kufahamishwa undani wa mkasa mzima alimwendea Rais Ali Shein,na kumuambia maneno yafuatayo: “Mhe. Rais ninasikitika sana kwamba sisi wenyewe ndio tunaohusika na haya yanayotokezea hivi sasa. Watu wetu wanajua wapi alipo Sheikh Farid. Wanafanya hivi kukuharibia wewe uonekane kwamba huna uwezo wa kuongoza na kwamba unaiwachia nchi iingie kwenye machafuko. Lakini zaidi wanafanya hivi ili kuivunja GNU,maana watatufanya sisi tujihisi kwamba ni sehemu ya uozo huo nasi hatutakubali. Sasa waambie watu wako ambao wako chini ya ofisi yako (akamtaja kwa jina yule kijana wa Idara ya Usalama wa Taifa) wakuoneshe walipomueka Farid.” Usiku wake, saa 2:00 Sheikh Farid akaachiliwa.

  Hadi kuachiliwa kwa Sheikh Farid, tayari sehemu ya lengo moja kwenye mkakati wao ilishafanikiwa: nayo ni kutengeneza mazingira ya fujo na kuhalalisha matumizi ya nguvu, ghasia na uvunjwaji wa haki za binaadamu kama yanayoendelea sasa. Pia kwa sababu ya kuficha uovu na asili ya mkasa mzima, wamemkamata Sheikh Farid na viongozi wa Uamsho ambao wanaujua ukweli wote wa mkasahuu, na sasa wamewaweka ndani na kuwafungulia mashitaka kadhaa, ili wasiwe nje wakaweza kuueleza umma kile hasa kilichotokea. Kwa upande mwingine, wanavilisha vyombo vya habari vya Tanzania Bara na vile vya Zanzibar vinavyopinga Maridhiano na Umoja wa Kitaifa,taarifa za uongo kuhusu viongozi hao wa Uamsho na wafuasi wao.

  Picha inayojengwa ni kwamba Uamsho ni magaidi na hivyo wapate kuhalalisha kuongeza wanajeshi na matumizi ya nguvu ya vyombo vya dola dhidi ya wanaodai mfumo wa Muungano wa Mkataba. Hivi sasa operesheni ya kijeshi imeimarishwa kisiwani Unguja, hasa kwenye mkoa wa Mjini Magharibi, ambako Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba Mpya inakuja hivi karibuni.

  Wananchi wanatishwa na wanatiwa hofu na mazingira yanajengwa ya kuzuia maoni ya wananchi hao mbele yaTume, maana hadi sasa wengi waliokwishatoa maoni yao, wameshasema wazi kuwa wanataka mabadiliko ya msingi kwenye Muungano. Matokeo wanayoyatarajia ni aidha kwa wananchi wanaopigwa na makundi waliyoyatayarisha na vikosi vya SMZ kujibu mapigo na hivyo kuiingiza nchi moja kwa moja kwenye fujo za kudumu, au kwa wajumbe wa CUF kwenye GNU kuja juu na kujitoa kwa kupinga dhuluma hii. Lolote kati ya mawili hayo, mwisho wake ni kuyavunja maridhiano na umoja wa kitaifa na hivyo kuiua na kuizika kabisa Ajenda ya Zanzibar.

  Kwa upande wa wananchi, programu hiyo inalenga kuwavunja moyo wao kwa serikali ya GNU, hasa kwa wafuasi wa CUF mbele ya Makamo wa Kwanza Seif Sharif, ambaye wanajengewa picha ya kwamba amewasaliti na haguswi na mateso wanayoyapata. Mwenyewe Maalim Seif analijua na analifuatilia kwa karibu kilalinalotokea na anamshauri Rais Shein kama ulivyo wajibu wake kama makamo wa kwanza wa Rais. Amechukua na anaendelea kuchukua kila jitihada za kumsaidia Rais Shein na kuilinda GNU isianguke, maana ikianguka ndio hatima ya Zanzibar imekwenda pamoja nayo. Katika ghasia zinazoendelea sasa kwenye jimbo la Bububu,amemfahamisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayehusika na vikosi vya SMZ, Dkt. Mwinyihaji Makame, na amemueleza wazi kwamba kinachofanyika ni uvunjaji wa haki za binaadamu, mateso na udhalilishaji, ambao mwisho wake ni kwa wananchi kuamua kujilinda; na machafuko yakisambaa,hakuna hata mmoja atakayenusurika, si Dkt. Mwinyihaji wala si yeye Maalim Seif.

  Laiti Rais Ali Mohammed Shein ana dhamira, nia na uwezo wa kuinusuru ndiye mwenye nafasi ya juu kufanya hivyo. Wapinzani wa Maridhiano na Umoja wa Kitaifa walikuwapo pia wakati wa muasisi wake, Rais Amani Karume, lakini alikuwa na uthubutu wa kuwadhibiti. Rais Shein kwa upande ake anaonekana kuelemewa vibaya na kundi la wapinzani wa Maridhiano na Umoja wa Kitaifa waliomo kwenye serikali yake, chama chake na vyombo vyake vya usalama. Kundi hilo ambalo linatumikia ajenda ya Tanganyika dhidi ya Zanzibar, kama ilivyoonekana wazi, liko tayari hata kukanyaga maiti za Wazanzibari alimradi tu lifikie kwenye lengo lake.
   
 2. meddie

  meddie JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 413
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Kwenye red hapo ndo center ya ujinga/ushenzi wa wazanzibari awe kasoma amahakusoma....ni watu wakuambiana mambo ya uongo/mambo husiyoweza kudhibitisha na kupata uhalisia wake lakini ukaambiwa NDIO UKWELI
  Mambo ya uongo yanaelezwa kama mambo ya kweli. Kwenye miazala yao wanakaa kusikiliza mpaka kurekodi ujinga wa namna hii. Mitaani unakuta watu wamekaa wanasikiliza cd za kipuuzi ilimuradi anaeleza anaitwa shehe ama ustaadhi basi!!

  huyo ni ustadhi farid ama muuni farid!
   
 3. njeeseka

  njeeseka JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 19, 2012
  Messages: 1,240
  Likes Received: 612
  Trophy Points: 280
  mmh! hapo pa kupigiwa simu na kujibu kwamba anateswa mh mbona sijaelewa! uko mrengo ngani ule wa kutetea...... au kufichua?
   
 4. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Naona hili ni trela tu picha lenyewe linakuja!!!
   
 5. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  lybenito Unashauriwa kuwahadithia kule vijiweni kwenu, si muda mrefu utatuambia SMZ ilichoma makanisa huko Zenj na Uamsho wakazima moto huo!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. T

  Tabby JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 8, 2008
  Messages: 9,901
  Likes Received: 5,543
  Trophy Points: 280
  Honestly speaking mmezidi kuwafanya watu wapambaff hat katika masuala yaliyo wazi. Ninyi ni binadamu gani msiotaka kukubali ukweli hata pale ulipo bayana? Fujo zenu za uamsho leo mnasema ziliasisiwa na kutekelezwa na serikali. Juzi mmechoma makanisa kwa kisingizio cha kukojolewa Qoran leo mnasema Wakristo ndio waliokodisha wahuni, wakachoma makanisa ili kuwachafua waislam!. Ujinga mtupu. Kitabu kimekojolewa na mtoto, adhabu mnaipeleka kanisani kana kwamba mnajua kanisa ndilo lilimtuma mtoto yule akojolee. Wala hamtaki kumwongelea yule mtoto na waliokuwa nyuma yake katika mkakati wa kumshawishi yule mwingine akojolee!. Mna matatizo gani ninyi binadamu?
   
 7. P

  PSM JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 543
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa ni wakuombewa tu ndugu Mbona vichwa hivi vilishashindikana tangu zamani,akili zao Hawa ni nzito sana !
   
 8. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Majuzi kuna jamaa (Mwislamu) huko Pemba amekojolea Quran na kuivika Quran Mbwa. Baadae akaenda kujisalimisha. Isije ikawa nayo hiyo ni program ya kufifia ajenda ya Zanzibar huru au Muungano wa Mkataba.

  Tutasikia mengi kabla katiba mpya.
   
 9. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Siku zote historia haifichiki na siku zote inajirudia.

  Tanganyika na Znz kwa aina yoyote haziwezi kuungana kutokana na historia zao. Muungano umekuwa ni wa kulazimishana na kuburuzana na kuacha masuala mengi na manung'uniko mengi sana kwa pande zote.

  SERA BORA kwa wote ni KUHISHIMIANA na SIO KUVUMILIANA.

  Na kwa maana ya kilugha NENO KUHISHIMIANA na KUVUMILIANA ni maneno tofauti sana sana. Kwa Kuvumilana siku zote kunazaa kubebana na kulindana. Wakti Kuhishimiana kunazaa kufuata utaratibu wa sharia na kuleta haki na usawa wa jamii
   
 10. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Waislamu bwana hawaishiwi nyimbo
   
 11. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Anzisheni muswaada wa kujitoa katika muungano, mpige kura halafu muondoke huku bara .... mnatukera.
   
 12. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  SMZ na Zanzibar vim,eshakufa na wala wasilaumu mtu mwingine zaidi yao wenyewe kwa sababu walianzisha ajenda bila, 1. kukubaliana wanataka kufanya nini na 2. kutopia uwezo wao wa kuitekeleza ajenda hiyo.
  Kama lengo lilikuwa ni kudai Zanzibar kwa nini muafaka ukafanywa siri ya Karume na Maalim Seif? Mpaka leo hii wazanzibari wengi wanalazimishwas tu waidai zanzibar wakati kiuhalisia hawajaambiwa misingi ya kufanya hivyo. KInachoendelea Zanzibar hivi sasa hakian tofauti sana na kilichotokea 1964 wakati Nyerere na Karume walipokubaliana kuunganisha nchi zao bila ridhaa ya wananchi. Hiyo Zanzibat inayodauiwa haitadumu hata kama ikipatikana kesho
   
 13. don12

  don12 JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 11, 2012
  Messages: 676
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  mnatutia shombo la ujinga, bila shaka mleta umbeya ni mwenzao, to hell na upumbavu wenu, ingekuwa vema muungano ungevunjika waende kwao,
   
 14. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Maoni yangu katiba mpya ifute dini ya kiislamu maana mungu wao anawafundisha uuaji,wizi,uongo,umalaya,ubishi,unafiki,wivu,fitina,uuchoyo,ubaguzi,ubakaji,ufilaji,ujinga na dhambi mbayambaya zoote ni zao.
   
 15. james chapacha

  james chapacha JF-Expert Member

  #15
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 942
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Mkuu sjakuelewa unachotaka kukisafisha,kama niswala la UAMUSHO nisawa kupamba JENEZA,kwajinsi ulivyo shusha uzi wako unataka tuamini kwamba serikali ndio inausika na uchomaji wa makanisa.na swala lakutekwa niwewe unalisema!!!mbona Farid hajawahi kutamka kwa kinywa chake kama alitekwa?au wewe ndio msemaji wake?au ujawaona waliotekwa?acheni uzushi.
   
 16. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Du ndugu yangu vyote hivo nakubaliana navo lakini kufilana na wizi HAPANA bana mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni
   
 17. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #17
  Oct 30, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,005
  Trophy Points: 280
  inawezekana kabisa kwa hali ya sasa zanzibar....na si mageni kila anaeonesha kupinga mfumo wa mungano huangamizwa..wengine watatukana ,watakejeli lakini huo ndio ukweli..WANAHUSIKA MOJA KWA MOJA KUFANYA UHARAMIA HUU...
   
 18. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #18
  Oct 30, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,005
  Trophy Points: 280
  5. ALCOHOL: devilish advice in God's (?) Book? (a) "Alcohol is for people who are DYING, for those
  who are in MISERY. Let them drink and FORGET their poverty and unhappiness." (From the
  "Good News Bible In Today's English") PROVERBS 31:6-7 Alcohol recommended in preference to
  water! (b) "Drink no longer water, but use a little wine for thy stomach's sake and thine often
  infirmities 1 TIMOTHY 5:23 What does the AA (Alcoholics Anonymous) say
   
 19. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #19
  Oct 30, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,005
  Trophy Points: 280
  BASTARD: This word occurs in the Bible THREE times (a) "The BASTARD shall not enter the
  congregation of the Lord; even to his tenth generation . . . DEUTERONOMY 23:2 (b) "And a
  BASTARD shall dwell in Ashdod . .ZECHARIAH 9:6 (c) "But if ye be without chastisement, whereof
  all are partakers, then ye are BASTARDS and not sons. " HERREWS 12:8
   
 20. M

  Mchokozi JF-Expert Member

  #20
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nimesoma aya moja nikaona ni Ushenzi mtupu ngoa nitamalizia baadaye nikipata muda
   
Loading...