Chanzo cha vitambi, uzito na unene kupita kiasi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chanzo cha vitambi, uzito na unene kupita kiasi

Discussion in 'JF Doctor' started by Pdidy, May 7, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,358
  Likes Received: 5,656
  Trophy Points: 280
  Jamani kuna ndugu yangu anateseka sana na kitambi amejaribu kunywa whisky za aina yote akiamini atapunguza kitambi jawabu -ve...kwenu wapendwa...afya bora kwa kila mtanzania...
   
 2. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  sasa mama si ungepeleka jukwaa la afya? make katumbo kanene na siasa wapi na wapi?
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mwambie aachane na whisky. Apunguze kula nyama na atembee angalau kilomita 8 kila asubuhi. Na asiache pushups.
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,358
  Likes Received: 5,656
  Trophy Points: 280
  one step;
  Mwambie aachane na whisky. Apunguze kula nyama na atembee angalau kilomita 8 kila asubuhi. Na asiache pushups

  thanks
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,358
  Likes Received: 5,656
  Trophy Points: 280
  sasa mama si ungepeleka jukwaa la afya? make katumbo kanene na siasa wapi na wapi?

  ni kweli mkuu rwagubiri ila wengine mpaka waende jukww la AFYA UJUE NDUGU ZAO WAKO MAUTIUTI...at least huku mtu akiona anatoa mawazo yake na msaada unaoitajika ni wa haraka si mpaka mtu aende afya...samahani kwa kukukwaza...ubarikiwe
   
 6. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Apunguze kula vyakula vya wanga kwa wingi...

  Asubuhi - breakfast nyepesi (matunda + mboga na wanga kidogo kama mkate wa brown)

  Lunch - Wanga kidogo + Maharage + Mboga za Majani kwa wingi

  Dinner - Mboga za Majani + Matunda (Dinner iliwe walau Masaa 2 kabla ya kuingia kulala).

  Anywe walau Lita 1 ya maji kwa siku.

  Apate walau Masaa nane ya usingizi.

  Afanye mazoezi ya viungo ikiwamo situps walau mara 3 kwa wiki.

  ASINYWE POMBE.

  Mifano ya Chakula ni "mifano tu" awe mbunifu kulingana na taste yake...ili mradi aepuke milo mizito kama Ugali, Wali, Mihogo, Vitumbua mara 3 kwa siku.
   
 7. Saikosisi

  Saikosisi JF-Expert Member

  #7
  May 7, 2009
  Joined: May 4, 2007
  Messages: 528
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Sahihi kabisa, msisitizo ni kwamba huu ndio uwe mfumo wake wa maisha asitarajie makubwa - ni kupungua kilo 5 kwa mwaka, taratibu ndio mwendo.
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Pombe anaweza kunywa in moderation. Ama chupa mbili za bia kwa siku au glasi moja ya mvinyo mwekundu kwa siku.
   
 9. K

  Koba JF-Expert Member

  #9
  May 7, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ...sema tu ni bwana yako,mwambie apunguze kula na afanye mazoezi!
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  May 7, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  mwambie awe anapiga sit ups 100 jumatatu jumatano na ijumaa
   
 11. K

  Koba JF-Expert Member

  #11
  May 7, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ...jtatu,jtano..ijumaa,wewe huo uganga wako wa kienyeji kawaibie huko kwenu sio humu!
   
 12. C

  Chuma JF-Expert Member

  #12
  May 7, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Pole kwa Kitambi...

  Ushauri wangu

  1. Afunge...alau kwa wiki mara 2
  2. kama anauwezo afunge swaumu kwa mwezi mara 15, afunge na kula kesho yake...na Ulaji wa vyakula Kitaalamu.

  3.Awe na muda kufikiria matatizo yanayowakabili watanzania wengi ambao hawana elimu, tiba hafifu,mlo haba na mengineyo, namna kuondoa utawala mbovu vitamfanya apungue kitambi kwa kushughulishwa matatizo hayo.

  4. Pombe zote aache.(naomba kutofautiana nao na wadau hapo Juu)
  5. Apate Belt za kufunga Tumboni kupunguza ufumukaj wa tumbo.
  6. Mazoezi hapaswi kuyaacha. Kila zoezi litakalopelekea kupunguza mwili asiache.

  Kikubwa Uvivu(Kujiachia) na kulala Hovyo, Ulevi ndizo sababu kadhaa za Kufumuka matumbo.
   
 13. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #13
  May 7, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kuna jamaa alikuwa na tatizo kama hilo, ilikuwa kazi kukata kucha za miguu mpaka mtu amkate. Alivyoenda kwa wataalamu, akaambiwa kwa wiki mbili ale mboga mboga na matunda tu, akitaka sharubati basi iwe ya chungwa ama zabibu na vizuri iwe fresh. Baada ya wiki mbili alikuwa kaambiwa ale wanga mchana tu kwa wiki tatu na aliambiwa apunguze kama atashindwa kuacha kwa wiki hizo tatu nyama, ale samaki na kuku tena kwa uchache mno. Ila vizuri aliambiwa ale maharagwe ya soya na mihogo kiasi mchana, kwa wingi matunda na mboga mboga. Baada ya miezi miwili usingeweza kujua ni yule.

  Mwingine alikuwa mhindi, huyu yeye alikuwa mnene ile ya kutisha. Ushauri wote aliopewa haukupunguza unene wake kabisa. Alihangaika sana kwa hilo manake alikuwa anapata shida na huo unene. Siku moja akaenda kwa daktari akamueleza yote jinsi alivyohangaika kupunguza unene imeshindikana. Daktari akamchukua vipimo, halafu akamwambia kuwa kwa unene ule ana tatizo kubwa sana linaloweza kumsababishia moyo usimame ghafla kufanya kazi, sababu hata moyo wake una tatizo kaligundua. Akampa dawa akamwambia kuwa baada ya mwezi arudi bila kukosa huenda kama dawa hazitofanya kazi watamfanyia uperesheni na itahitajika haraka kuokoa maisha. Jamaa akatokwa jasho vibaya mno, akaenda kutumia dawa, baada ya mwezi aliporudi hospitali alikuwa kwisha kabisa kwa kuogopa kifo. Daktari akamwambia nilikutisha ili upone, na dawa nilizokupa ni Aspirin, hivyo sasa fuata ushauri wa chakula usinenepe tena. Kilichotokea kumbe jamaa alikonda kwa kuogopa kifo, baada ya mwaka unene ukarudi kama kawaida.

  Chukua ushauri wa kwanza.
   
 14. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #14
  May 7, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu, akinywa chupa 2 za bia kwa siku..hapungui ngooo..!!!
   
 15. H

  Hondo Member

  #15
  May 7, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nafikiri huyo bwana anatakiwa afanye mazoezi kidogo halafu awe nakiasi kwenye kula .Halafu aache pombe badala yake anywe maji mengi kila siku.
   
 16. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #16
  May 7, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,358
  Likes Received: 5,656
  Trophy Points: 280
  mwambie awe anapiga sit ups 100 jumatatu jumatano na ijumaa
  __________________
  nyani ngabu umesomea usheikh yahaya nini???
   
 17. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #17
  May 7, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Mpe glass mbili za aloe vera kila siku ikipita mwezi atakuwa flat kama Shamsi Vuai Nahodha, akiongezea sit ups basi atakuwa na six pack kama Pinda.
   
 18. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #18
  May 7, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,761
  Trophy Points: 280
  Bongo tambarare..

  watu wanajadili namna ya kupunguza miili yao wakati wengine hata uhakika wa huo mlo wa mchana haupo?
   
 19. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #19
  May 7, 2009
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Watu wengi Tz sahivi wanatatizo kubwa la kua na uzito wa ziada (overweight) na hiyo inasababishwa na mambo mengi kubwa likiwa ni kutokuwajibika kwa Wizara ya Afya (kutotoa elimu ya afya kwa watz), utamaduni wetu (kufikiri kua kula nyama, bia na vyakula vyenye mafuta mengi kila siku ni ufahari au ishara ya maisha bora,kutojali mazoezi pengine kutokua na maeneo ya wazi ya kufanyia mazoezi(maana si wote wanaoweza kumudu gym za kulipia), kupenda kutumia usafiri wa gari hata maeneo ya karibu ambayo unaweza kutembea kwa miguu, kutumia lift badala ya ngazi hata kama ni kushuka floor mbili tu chini. Listi ni ndefu ila kujibu swali lako mwambie ajalibu kuepuka hayo madogo madogo kwanza halafu afuate ushauri uliokwisha kutolewa hapo juu na wadau wengine.
   
 20. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #20
  May 7, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hey people, vitambi vingine ni vya urithi... Sasa wadau mngefuatilia kwanza kwa Mama Mia, je huyu jamaa (..mume wake??) ana historia gani...!!!! Mi sina utaalamu, but ni mtazmo tu.. ha..haaa...haaaaa!!!
   
Loading...