Chanzo cha Ujambazi Tanzania ni hiki

Bowbow

JF-Expert Member
Oct 20, 2007
541
32
Kampuni binafsi za ulinzi nchini, zimekataa kulipa kima kipya cha mshahara wa Sh. 80,000 kwa wafanyakazi wake, licha ya serikali kuagiza viwango hivyo kulipwa na sekta binafsi kuanzia Januari, mwakani.

Wakurugenzi na Mameneja wa Makampuni ya Ulinzi Mkoa wa Mbeya walitoa uamuzi huo jana wakati wa mkutano ulioitishwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Sekta ya Ulinzi Tanzania (TSIA), Bw. Athuman Maige, na kufanyika katika hoteli ya JM Jijini hapa.

Wakurugenzi na Mameneja hao walisema hawako tayari kulipa kiwango kipya cha mshahara cha Sh. 80,000 hadi hapo serikali itakapo washirikisha upya kutoa mapendekezo mapya ya kupanga kiwango cha chini cha mshahara kwa makampuni ya ulinzi kwa kuzingatia uchumi wa kila mkoa.

Mwenyekiti wa Chama cha Sekta ya Ulinzi Tanzania, Bw. Maige, alisema katika mkutano huo kuwa serikali imeharakisha kutangaza kima cha chini cha Sh. 80,000 kwa kampuni binafsi za ulinzi, bila kufanya tathmini kuona kampuni hizo zinalipwa kiasi gani na wateja wao katika malindo.

Bw. Maige alisema katika utafiti alioufanya katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Morogogoro na Tanga, alibaini kuwa kampuni za ulinzi zinalipwa na wateja wao kati ya Sh .45,000 hadi 50,000 kwa kila lindo, kiwango ambacho hakitoshi kulipa askari msharaha mpya wa Sh. 80,000.

``Mvurugano wa kima cha chini cha mshahara umekuwa kama hadithi ya kuku na yai, nani alitangulia, haiwezekani serikali isema tuanze kulipa mshahara wa Sh. 80,000 wakati malindo tunayolinda tunalipwa Sh. 50,000, hivi tutakuwa tunafanya kazi gaini,`` alihoji.

Mwenyekiti huyo alisema kutokana na agizo hilo la kulipa mishahara ya Sh. 80,000 ni wazi kuwa yapo makampuni ambayo yatafunga kuendesha kazi hiyo kwasababu hayawezi kulipa askari wao kiwango hicho ambacho serikali inataka, wakati wao wanalipwa na wateja wao Sh. 50,000 kwa mwezi.

Alisema kampuni za ulinzi zipo tayari kujadili upya na serikali kuhusu hatma ya mishahara hiyo, lakini kwa sasa hayatakuwa tayari na wala hawakubaliani na tangazo la serikali la kuanza kulipa mishahara mipya ya Sh. 80,000.

Aliwaagiza Wakurugenzi na Mameneja wa kampuni za ulinzi kumpelekea orodha ya askari wa makampuni hao ambao wamefutwa kazi kwasababu malindo waliyokuwa wanalinda wateja wamekataa kuongeza malipo ili ampelekee Waziri wa Maendeleo ya Vijana na Ajira.

Naye Mwenyekiti wa kampuni za ulinzi Mkoa wa Mbeya na Kanda ya Nyanda za juu Kusini Bw. Kasmali Kubaja, alisema baada ya serikali kutoa tangazo la kutaka sekta binafsi kuanza kulipa mishara Sh. 80,000, kampuni binafsi za ulinzi zilipo wajulisha wateja wao ili waongeze kiwango cha malipo kwa lindo kufikia Sh.120,000 walikataa na kufuta mkataba wa kulinda maeneo yao.

Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa kamwe hawatakuwa tayari kulipa kima cha chini cha mshahara wa Sh. 80,000 kwa mwezi na kwamba malindo ambayo wateja wao wamekataa kuongeza malipo ili kwenda sanjari na ongezeko la kima cha chini cha mshahara watalazimika kufunga shughuli zao.

Tamko hilo la makampuni ya ulinzi limekuja wiki moja tu tangu serikali iliposisitiza na kukiagiza Chama cha Waajiri Nchini (ATE) kuhakikisha kuwa waajiri katika sekta binafsi, wanawalipa wafanyakazi wao viwango vipya vya mishahara vilivyotangazwa na serikali.
Source ippmedia.com

Mishahara wanayolipa ni kidogo kwa nini wasishirikiane na majambazi kutoa siri za ndani pale walindapo.

Ulinzi ni Jukumu la serikali kama watu wanapenda kuwa na ulinzi binafsi basi waongezewe kiasi maana naamini mlala hoi wa kawaida haadhiriki kabisa bali atafaidi mshahara walau wa 80,000.
 
Back
Top Bottom