Chanzo cha mbunge wenje kusema wabunge waache unafiki. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chanzo cha mbunge wenje kusema wabunge waache unafiki.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 15, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Posted: 15th August 2012 by MillardAyo in News

  4
  [​IMG].

  Mbunge wa Nyamagana Mwanza kwa ruhusa ya Chadema na wananchi wa jimbo lake Ezekiah Wenje amewataka wabunge wa bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kuacha unafiki na badala yake waitishe mjadala wa kitaifa kuhusu lugha maalum ya kufundishia kwa shule za msingi.

  Namkariri akisema "lugha kwenye primary school ni Kiingereza au kiswahili? mimi nawachallenge acheni unafiki, kama ni Kiswahili iwe Kiswahili kwenye primary School kama ni Kiingereza basi na hizo shule za Serikali zifundishe kiingereza ili wanafunzi wapate hiyo Knowledge ya kiingereza, wanafunzi wa watu masikini pia wapate kama watoto wenu wanavyopata"

  Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya wizara ya Elimu, Wenje amesema wakati wabunge wakipigia debe matumizi ya kiswahili wenyewe pia wamekua wakisomesha watoto wao kwenye shule zinazotumia lugha ya kiingereza.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kweli Kabisa wakati wetu wa Nyerere tukiwa Primary kulikuwa hakuna Private School Nyingi kama sasa za Kiingereza

  Wabunge, Mawaziri na Rais hawakuwa wanapeleka watoto wao Malawi, South Afrika au English Medium Schools

  Zote Zilikuwa za kiswahili... Sasa kweli tuchague Primary School Iwe Engilsh Medium au Swahili Medium...

  Tusipendelee...
   
 3. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #3
  Aug 15, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Pia tuimarishe mafunzo na motisha kwa walimu, Vitabu na nyenzo za kufundishia ziwepo vya kutosha ili kuinusuru elimu ya msingi inayoporomoka kwa kasi.
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Aug 15, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  si na yeye ni mbunge? Au yeye ni diwani??

  Polished nitoke vipi.
   
 5. w

  wikolo JF-Expert Member

  #5
  Aug 15, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Nadhani ametoa angalizo zuri sana. Kwa nini kuwe na utofauti kwenye lugha ya kufundishia?
   
 6. eumb

  eumb Senior Member

  #6
  Aug 15, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  He's very right, mtafutate mwanafunzi aliyemaliza kidato cha nne Shule za kata halafu muweke na yule Wa darasa la kwanza English medium school halafu uone tofauti ktk kuongea kiingereza!
  Nimeshuhudia ktk English medium school nyingi utakuta walimu na hasa walimu wakuu ni raia Wa Kenya au Uganda! Ni vizuri bunge likafanya mabadiliko makubwa ktk matumizi ya lugha ya kiingereza.
   
 7. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #7
  Aug 15, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Ndio Maana amesema anawataka Wabunge waache fitina... WA[
  inamjumuisha yeye pia]
   
 8. M

  Marketer JF-Expert Member

  #8
  Aug 15, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 261
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  tatizo hata walimu wenyewe kingereza cha kuunga unga, sasa hata wakiwafundisha itabaki not reachable, wenzao st, huko wanaleta walimu wazambia, uganda, wakenya full kutema yai! Mwnyewe product ya kata afu mwanangu nimempeleka Esacs nakwepaje kuongea nae nisije kujiabisha bureee! Namsisitiza aongee kiswahili nyumbani ni lugha ya taifa itamsaidia kumbe kukwepa kuonekana mzazi english not reachable
   
Loading...