Chanzo cha matatizo yote ya Tanzania ni JK

sehemu kubwa ya watanzania akili zimeoza na ndio chanzo cha matatizo kazi kupiga domo tu rais mmemuweka wenyewe mliona anafaa leo ooh rais ndio tatizo mambo magumu dunia yote ongezeni juhudi kupambana na umaskini

Kweli kabisa ndugu lakini umesahau maneno ya Mfalme Sulemani kuwa "Rushwa upotosha Taifa..."
juhudi lazima iongezwe na wanaifirisi nchi(walarushwa) ni lazima wawajibishwe..
Hakuna 1 litakalo enda likaliacha lingine nyuma...
ZINDUKA
 
Ukweli pekee ndio utatuweka huru and so be it. Hata kama tutaendelea kujikomba kwa watu kwa kiasi chochote kile, mwisho wa siku, ukweli ni kuwa tuna matatizo makubwa sana ya kiuongozi.
 
Uzuri JK anasaidia kukiua chama chake taratibu,wenzie wakichekelea na kushuudia.Kipindi hichi ndio cha wapinzani kujiimarisha na vijana kujiandikisha kwa wingi ili 2015 wapige kura wote za kuchagua serekali wanayoipenda.CCM PWAAA!!!!Karibuni
sasa ndiyo kuangalia gani huko tuangaliane uso kwa uso
 
Ukweli pekee ndio utatuweka huru and so be it. Hata kama tutaendelea kujikomba kwa watu kwa kiasi chochote kile, mwisho wa siku, ukweli ni kuwa tuna matatizo makubwa sana ya kiuongozi.

And we must face the reality, kiongozi wetu ametuangusha, na hawezi kupima mwenyewe, inabidi wananchi tuamue.
 
Si kweli Rais hawezi kulinda waovu lakini pia Serikali haiongozwi na kila mtu akiamka simamisheni Jaifo, Lumbanga, Mponda kuna taratibu zake kwani kuna mihimili 3 Mahakama, Bunge na Serikali hivi haviingiliani.Lakini kila Kikao kikao cha Bunge lazima hoja lazima kiongozi aambiwe JIUZULU kazi ya Bunge ni kutunga Sheria na kushauri sio kulazimisha au kusema Waziri Mkuu jiuzulu itafuata sasa Rais ambapo naye atavunja Bunge hapo lengo ni nini? Wabunge wengi wamesoma Public Law hata kidato cha 2 somo la Uraia, Magazeti leo yamedokeza Mtaalam wa Siasa UDSM Bw Bana.amesema Bunge ni kutunga. Sheria ntalifuatilia Gazeti hilo namalizia nihukumiwe lkn sio Wabunge wawasimamishe Waziri mkuu au Mawaziri wote 8 wao ndio wamewachagua? Rais atalibadili tu baadhuu ya sura hilo Baraza kabla ya June 12
hapo kuna mihimili miwili hakuna mitatu. mahakama na serikali vinaingiliana. rais ndio anaeteua ma-top wa mahakama. rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ana uwezo wa kumuondoa top yeyote wa mahakama. kama rais angekuwa hawezi kumng'oa top yeyote wa mahakama kweli ungesema mahakama na serikali haviingiliani. Pia inasemekana rais anaweza kulivunja bunge na kila mbunge akagombee upya kwa maana hiyo serikali pia inaingiliana na bunge. KWA KIFUPI HAPO KUNA MUHIMILI MMOJA TU. HAKUNA MITATU. huo usemi wa mihimili mitatu ni wa kuwapumbaza wasio na uwezo wa kupambanua mambo, ambao ndio wengi nchini kwetu na ndio hao wenye kuamini hivyo.
 
kwanza sipendi kumlaumu sana JK kwakua kiongozi legelege wa Taifa hili.
nawalaumu ccm wote waliomshauri huyu jamaa kugombea uongozi wa juu wa taifa letu, nawalaumu na kuwaombea mabaya daima.

Pia nawalaumu watu wote waliompigia kura huyu jamaa 2005 na 2010 wngi wao wanawake waliokua wakimsifu kuwa jamaa ni handsome na kijana .

pia nawalaani waandish wote wa habari wakiongozwa na wale kutoka Habari Corp pale Kijiweni, Uhuru na wale TSN BILA KUWASAHAU tbc kwa kutumika kupotosha umma.

Mh.KIKWETE NI ISHARA MBAYA KWA TAIFA, NI ISHARA YA TAIFA DHAIFU LA WATU WASIOFiKIRI SAWASAWA maana alichaguliwa kwa vigezo potovu na sera rojo .
 
Kabla ya JK kuwa Rais kumbe Tanzania ilikuwa aina matatizo.

Matatizo yalikuwepo na hayatakaa kuja kwisha.But when we lack boldness to face them! It become a pain in the urse. Lazima tufike mahali tuwe owners of the destination we want to go. Naona sasa hivi tunakwenda na neutral gear wakati tunapanda mlima. Only in Tanzania!!!
 
Makamanda nilishawatonya humu ndani. Kwa mtu unaeelewa mfumo wa utawala hapa Tanzania kwa mjibu wa katiba mbovu na dhalimu ya sasa huwezi kumnyoshea kidole kiongozi yeyote ktk serikali kwa mambo kwenda mlama. Ila Rais kwa kuwa yeye amepewa madaraka ya ku-hire and fire, hivyo mambo yanapokwenda vibaya hadi nchi kufilisika na yeye kukaa kimya ni kwa kuwa anajua kila kitu na ana interest.
Kwa kifupi wabongo jueni kuwa hakuna deal iwe mbovu au nzuri ktk nchi hii itapita bila mkuu wa kaya kujua. Hivyo watanzania tutaendelea kulia hadi 2015 na mkuu hatachukua hatua yoyote maana anajua hana la kupoteza cause kura zenu hataziitaji 2015. Unless wachache waajitolee mhanga kunusuru nchi hii kwa ajili ya wengi watakaobaki.
 
Kikwete ni kama umedandia basi kwa tiketi ya wizi, usisingizie dini wala nini kazi huwezi. Maendeleo hasi uliyotuletea hapa tanzania ni balaa kwa vizazi vya leo na vijavyo bora ya chifu mangungo wa msowero aliyesaIni mikataba ya kuuza nchi yake mbele ya mtutu wa bunduki kuliko wewe unayezunguka dunia nzima kutafuta wanunuzi wa nchi yetu kwa bei poa ukiongozana na madalali uchwara bila mikwaruzo yoyote . Ulaaniwe kwa matendo yako maovu kwenye uso wa ardhi tukufu ya Tanganyika. mzimu wa nyerere na ukupate kwenye kisogo uanguke kama nazi mbovu.
 
Kuwa Great thinker japo kidogo. Mbona inapotokea mambo yanakwenda vema duniani huwa hatuoni matokeo yake nchini kwetu? Ila yakienda kombo utasikia "Hii hali ni kwa sababu ya msukosuko wa uchumi duniani kote". To HELL!! Hebu jiulize

  • Kupakia Twiga, Tembo n.k kwenye ndege ni kwa sababu ya mambo magumu duniani,
  • Kuua reli ili malori yenu yapate kazi ya kusafirisha mizigo ni kwa sabubu ya mambo magumu duniani,
  • Kuua bandari a Tanga ili wajanja wa Dar waendelee kutesa ni kwa sabubu ya mambo magumu duniani,
  • Kuuza bandari ya Mtwara ni kwa sabubu ya mambo magumu duniani,
  • Jairo na Uwajibikaji ni kwa sabubu ya mambo magumu duniani,
  • Richmond ni kwa sabubu ya mambo magumu duniani,
  • Meremeta, TanGold, Kagoda ni kwa sabubu ya mambo magumu duniani,
  • Ufisadi kwenye Tamisemi ni kwa sabubu ya mambo magumu duniani,
  • Safari zisizo na ukomo za Rais wako ni kwa sabubu ya mambo magumu duniani,
  • Kuua shirika la ndege wakati Precision ikistawi katika mazingira hayo hayo ni kwa sabubu ya mambo magumu duniani,
  • Mrahaba mdogo kwenye madini ni kwa sabubu ya mambo magumu duniani,
  • Stimulus package fraud ni kwa sabubu ya mambo magumu duniani,
  • Mabilioni ya JK ni kwa sabubu ya mambo magumu duniani,
  • Ukosefu wa madawati wakati 50% ya nchi ni misitu ni kwa sabubu ya mambo magumu duniani,
  • Ukosefu wa walimu wakati nchi ina rasilimali watu zaidi ya milioni 40 ni kwa sabubu ya mambo magumu duniani,
  • Na mengine mengi............

Ndio haya tunayosema kuwa tatizo la pili ni wananchi wenyewe kuwa bongo lala. Tunasumbuliwa na ujinga tu. Ukishapewa Ukatibu kata basi huo ni mtaji tosha wa kukuwezesha kudai rushwa na mfumo huu ni safi kwako.

Ipo poa sana hii. Watanganyika ni watu amani sana. Tunabaki na maumivu moyoni kwa nini?. Tumeshagundua huyu handsome ndiye tatizo, Je tuendelee kuumia hadi 2015?. Mihimili mikuu ya nchi yote ameishikia yeye (Serekali - ni yake, anafanya anachotaka. Mahakama - anateua jaji mkuu,hivyo itatekeleza anachotaka yeye. Bunge -limetoa ushauri hadi limechoka, limebaki kupiga kelele tu, halina ubavu). Sasa nini kifanyike?
 
Mbona mkuu hilo linajulikana!!! sijui huyu mtu tulitokana naye wapi? ni sawa na kununua jini halafu unashindwa kulitimua linakunyonya damu tuu au linaanza kudai damu ya mtoto, mke mwishoni wewe. Navyokumbuka mwaka 2000 wanawake walivutiwa kuwa ni handsome wakahamasisha akapata kura nyingi kumbe ni mkenge tumeingia mwaka 2010 akakosa kabisa akaiba kura .kwahiyo hayupo kwa ridhaa ya wananchi sasa kwanini tusimtimue?
 
Kabla ya JK kuwa Rais kumbe Tanzania ilikuwa aina matatizo.

Matatizo yalikuwepo, tatizo ni kuwa JK hajui kuwa kuna matatizo ndiyo maana kutwa nzima anakenua tu. Kujua tatizo ndiyo mwanzo wa kutafuta ufumbuzi.
 
Matatizo yalikuwepo tangu awamu zilizopita, isipokuwa uhuru wa kuongea kwa uwazi haukuwepo vipindi hivyo. Utandawazi na technohama ilikuwa duni. Miaka 10 iliyopita ungeweza kutoa mawazo yako kama hivi na kwa kupitia wapi? Kwa hili sina budi kumsifu Kikwete, kwa kawaida mabaya huvuma kuliko mazuri. Wapi katika Afrika kuna hali nzuri kama mnavyotaka nyie? Umasikini umejikita, maradhi ndio usipime, uongozi mbovu kama kawa, acheni hizo...Wapinzani jipangeni vizuri kwa chaguzi zijazo sasa hivi hata mkiachiwa nchi hamtaiweza.
 
Dhambi tuliifanya; Tena kwa makusudi sasa inatumaliza. Dhambi yenyewe ni kupuuza maelekezo ya mwalimu Nyerere kuwa jamaa ni mkubwa umri tu sio kichwani, tukaona mzee anazengwe tu, lakni hebu fikiria tena rais mstaafu atakuwa na zengwe gani na Mtz yoyote anayetaka kwenda ikulu? tulikosea lazima tulipe gharama.
 
Tumesha ongea tena kwa machozi ya damu wakuu!
Tatizo tulio wengi tunaitaka pepo lakini kufa hatutaki!
 
Wala msihofu ndugu zangu kama JK ameamua kuwalinda mawaziri wake wasijiuzulu wananchi wa Tanzania sasa hivi uelewa wao umepanuka sana wanaelewa vizuri kwamba nchi hii imetekwa na kikosi cha mwamvuli ( mawaziri wa JK) ambao kazi yao sasa ni moja tu kupora fedha za wanyonge,iko siku watahukumiwa na kura ya huyo mwananchi anayeporwa mali zake.Ingawa siku hizi kuna usemi unaosema aliye juu mfuate huko huko,ninawaomba mvumilie hadi hapo mwaka 2015 pale ambapo tutakapokihukumu hiki kikosi cha miamvuli (mawaziri).

Naomba kuwasilisha
 
Mtazunguka wee , mtalalamika sana mtaongea huku hamtaki kumgusa huyu mtu ila chanzo cha hizi shida zote ni JK. hakuna mtu mwingine wa kushikwa shati ..huyu ndio tatizo la kila kitu hata kama mtamtetea .huyu mtu ni kama mkosi kwenye nchi yetu
nawasilisha..na nimetoa kilichokuwa moyoni mwangu siwezi kuwa mbaya kwa kusema ukweli

Yani Mkuu we ndo hili unalijua leo,sie tulijua tokea 2005 kuwa Mkwe.re ni Janga kwa Taifa letu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom