Chanzo cha matatizo bodi ya mikopo ya elimu ya juu hiki hapa

Didia

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
719
258
Bodi ya mikopo imekuwa ikilalamikiwa mara kwa mara karibia na kila kundi miongoni mwa jamii ya watanzania kwamba haifanyi kazi kwa ufanisi na hasa imekuwa ikichelewesha mikopo kwa wanafunzi.

Mojawapo ya makundi ambayo yameonesha kutoridhika na hata kulaumu utendaji wa bodi hii kuahidi/nakupendekezani ivunjwe ni Rais Kikwete, hivi Karibuni Waziri wa Elimu na UVCCM. Wangeni ni wanafunzi wa vyuo vikuu. Makundi yote haya yamekuwa na mtazamo kuwa ucheleweshwaji wa mikopo unatokana na bodi yenyewe!

Hivi majuzi wakati wafunzi wa Aridhi University wamelipoenda kudai feza zao Afisa Uhusiano wa bodi ya mikopo alitufumbua macho watanzania. Kwa maneno yake bodi haikuwa nafedha yoyote kwenye account hivyo isingeweza kuandika check ya malipo. Hapa ndipo jibu la swali la ucheleweshaji wa fedha za wanafunzi linapatikana. TATIZO SI BODI ILA NI SERIKALI KUSHINDWA KUIPA FEDHA MAPEMA! Tatizo hili limekuwa haliathiri tu wanafunzi bali pia utendaji kazi vyuoni maana hata ada za wanafunzi hucheleweshwa sana kwa majibu kuwa bodi haijapata fedha kutoka hazina!


Wito wangu: VIONGOZI WA SERIKALI/CHAMA TAWALA WAACHE KUTUPA MZIGO NA LAWAMA kwa BODI YA MIKOPO MAANA WAO NDO CHANZO CHA MATATIZO, HASA UCHELEWESHWAJI WA FEDHA ZA MIKOPO.
 
Back
Top Bottom