Chanzo cha maneno kama "Mngekomaje"

MTAMBOKITAMBO

Senior Member
Jun 2, 2011
194
39
Wakuu ningependa kujuzwa chanzo cha maneno kama hayo yenye je mwishoni.Nasikia wengi wanatumia huo mtindo siku hizi.
 
Nimewasikia watu wa arusha wakitumia sana huo msemo. utasikia angepigwaje! Arushaaaaaaaaaa
 
Si linatokana na "kukoma" yaani "kumaliza" .`Kwa hiyo maana moja ya neno "mngekomaje" labda ni "mngemalizaje" kwa kimombo "how would you complete/finish". Siyo?
 
Si linatokana na "kukoma" yaani "kumaliza" .`Kwa hiyo maana moja ya neno "mngekomaje" labda ni "mngemalizaje" kwa kimombo "how would you complete/finish". Siyo?
Hujanielewa mkuu,huu ni msemo mpya na una maana tofauti na ulijoizoea.Mfano,leo angekuja Obama Tanzania,wabongo tungepagawaje!Yaan hapo inamaanisha wangepagawa sana kupita kiasi.Sasa nataka kuja chimbuko la hii lugha.
 
Back
Top Bottom