Chanzo cha mabadiliko ndani ya CCM na hatma ya upinzani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chanzo cha mabadiliko ndani ya CCM na hatma ya upinzani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Anfaal, Aug 4, 2010.

 1. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ukifikiria kwa haraka haraka, namna watu maarufu walivyoshindwa katika chaguzi za CCM unaweza ukahitimisha kuwa wananchi wameamua kubadilika. Lakini huu ni upande mmoja tu wa angalizo. Upande mwingine ni kwamba mwaka huu kwa kiasi fulani rushwa imedhibitiwa na TAKUKURU na hivyo angalau kuwafanya wagombea wasio na chao ila wenye ushawishi waweze kusikika. Lakini pia mwaka huu, wagombea hawakupigiwa kura na viongozi pekee lakini pia na wananchi walihusika na hivyo kuwachagua hasa wale wanaowataka. Hapo kwenye bold inamaana upinzani hautapata kazi rahisi kuwang'oa hawa CCM waliopitishwa na wananchi ambao kwa mtazamo mwingine wanakubalika na waliowengi. Kwahiyo haitashangaza saana kama viti vya upinzani mwaka huu vikapungua kuliko wakati mwingine wowote.
   
 2. telele

  telele Member

  #2
  Aug 4, 2010
  Joined: Jun 4, 2010
  Messages: 29
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  unaota wewe! tena ndoto za mchana. pole sana
   
 3. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #3
  Aug 4, 2010
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Unaonaje kama ungeshindana naye kwa hoja? unadhani ni ndoto ya mchana kivipi wakati mtu kakupa sababu? Kibaya zaidi kwenye kampeini za kura za maoni wananchi wote hata wasio wanaccm waliruhusiwa kusikiliza na kuzipima sera za wagombea ubunge wa CCM.
   
 4. Ngorunde

  Ngorunde JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2010
  Joined: Nov 17, 2006
  Messages: 1,128
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Hilo ni jambo ambalo ni kama changamoto kwa vyama vya upinzani, nina imani hata viongozi wa upinzani (walio makini) wameliona hilo
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Watanzania wanaweza nadhani hata kwenye uraisi watafanya chaguo lililo bora! Si Mradi raisi eti kwasababu anacheka cheka
   
 6. G

  GEOMO Senior Member

  #6
  Aug 4, 2010
  Joined: Jul 11, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  :hippie: mimi nadhani kama ulivyotangulia kusema kuwa huo ni upande mmoja wa angalizo. Hivyo hata mawazo yako yameelemea kwa mfumo huohuo. Maana laiti ungekumbuka kuwa hata hao walioshindwa wameshindwa kwa kuzidiwa mbinu chafu na walioshinda. Mfano matumizi ya kadi feki, wapiga kura mamruki wasio wa maeneo husika n.k hivyo kubwa la kufahamu ni kwamba bado maamuzi halisi ya hao wana ccm wenyewe hayakupewa nafasi.
   
 7. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #7
  Aug 4, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mawazo ni mazuri tusubiri tuone kwani octoba sio mbali, ila nina kubaliana pia kwamba kwa namna fulani kuna kazi ya kweli ambayo imefanywa na takukuru angalau matangazo kwenye vyombo vya habari kwamba fulani amekamatwa nk. Hii imeleta tofauti ikilinganishwa na miaka iliyopita.
   
 8. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #8
  Aug 5, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Masa, unaweza kuwa sahihi katika hilo. Lakini ugumu wa Urais ni kukosa mizizi vijijini. Kwa kiasi fulani Dr Slaa anakura nyingi saana za watu wanaotumia vyombo vya habari relative to CCM. Lakini hawa watu wamjini wengi si wapiga kura. Maana hujifanya wanashughuli nyingi saana za maisha na wao wanachofaham ni kupiga porojo tu. Hii inathibitishwa na idadi ya majimbo yaliyopo mijini yanayoshikiliwa na wabunge wa upinzani. Kwa maana hiyo licha ya watu wa mjini kuwa na uelewa wa hali ya mambo kwa sasa, lakini wengi hawapigi kura na wanaopiga kura ni aidha wanahimizwa na CCM (chama chao), wanapewa vijisenti wanauza haki yao ya kuchagua nk. Ukiangalia kwa kijijini, mikoa mingi saana kwa mf Dodoma, Singida, Mwanza, Iringa nk. Bado imani ya wanavijijini kwa CCM ni kubwa na kuingamiza kwao si kwa kupima uwezo wa wagombea bali wao chama ndio wameweka mbele.
   
 9. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #9
  Aug 5, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  wamepigiwa kura na wana CCM sio wananchi..... elewa hilo, mwamko wa watanzania kuhusi siasa kwa sasa ni mkubwa sana, viti vya upinzania vitaongezeka tu......
   
 10. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #10
  Aug 5, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Kwa upinzani inakuwa kazi sana kumshinda mtu kama John Malechela kutokana na historia yake ndani ya nchi, lakini akija mtu mpya upinzania unaweza shinda tena kwa kishindo jimbo hilohilo
   
 11. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #11
  Aug 5, 2010
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tatizo la CCM sio jinsi gani wanachaguana kugombea Ubunge wala si nina ni mgombea, ila wanatumia mfumu ambao hata angekuwa nani hawezi kulita mabadiliko Tanzania. Kila mmbunge inabidi atumie akili ya Kikwete kutuletea maendeleo hii akili imeshindwa, imechakaa imejaa dhuluma na kubeba mizoga. Huwezi leta mabadiliko wakati unatumia mbinu zilizoshindwa kwa miaka aroibani, mzuri hawezi kuchagua kilichooza

  Yeyote anatafuta ubunge kupita CCM awe mpya au wa zamani ameoza tayari, hana jipya, kwani wapya kina Masha, Nchimbi, Komba, Kamala Dr. mwinyi wameleta nini wameishia kuwa wala rushwa na wavivu wasio wajibika.

  Sikiliza kauli ya makamba juu ya Ushindi wa January hapo ndipo utajua mvinyo ni uleule kwa mbinu zilezile.
  CHADEMA tumejipanga vizuri, tusibiri Octaber 31, tutajua.

  KURA YAKO KWA DR. W SLAA, KURA YAKO KWA MBUNGE WA CHADEMA KURA YAKO KWA DIWANI WA CHADEMA
  KURA YAKO CHADEMA.
   
 12. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #12
  Aug 5, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Wasio wa CCM ambao ndio wengi hawakupiga kura. Majority ya wa-CCm wengi waliwachagua watu wao baada ya kupewa bahasha-kwa kisingizio cha nauli za kwenda kupigia kura.

  Subiri wakati wa kampeni utaona ikiwa hao waliovhaguliwa wana uwezo hata wa kuieleza kwa wananchi ilani ya uchaguzi wa ccm.
   
 13. Elusive

  Elusive JF-Expert Member

  #13
  Aug 5, 2010
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana na wewe ni kweli CCM imejizatiti vijijini sana eneo ambalo vyama vya upinzani bado
  hawajifanyia kazi vya kutosha, kuna baadhi ya vyama watashindwa kusimamisha wagombea kwenye
  uchaguzi mkuu kwa sababu hawana uwakilishi wa kutosha na hivyo CCM itakua inapeta bila ya shida.
  Kama ulivyosema hata huko mijini wengi hawajajiandikisha kupiga kura lakini utawaona wanahudhuria
  kwa wingi mikutano ya siasa jambo ambalo halileti tija kwa vyama vya upinzani.
   
 14. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #14
  Aug 5, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Hao wametakwa na wanachama wa CCM na si wapigakura wote, kwani wanachama wa CCM ni sehemu gani ya wapiga kula hadi kujihakikishia ushindi?
   
 15. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #15
  Aug 5, 2010
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kama tukiangalia tathmini ya Anfaal kwa makini, ni kweli kuwa CCM inaweza kushinda kwa kishindo zaidi baada ya kushirikisha wanachama wengi zaidi katika uchaguzi wa wawakilishi wao. Pamoja na kuwa, si wanachama wote waliopiga kura kwenye uchaguzi huo na kuwa, wapiga kura katika uchaguzi mkuu si wote ni wananchama wa CCM, ukweli huu unazua tatizo kubwa zaidi ya upinzani kushinda. Tatizo hilo linatokea kwa kuwa uwigo wa wafanya kampeni wa CCM unakuwa mkubwa zaidi. Maana kila mwanachama anakuwa mhusika wa kumnadi mgombea ambae alimchagua kwenye kura za maoni.

  Kwa upande mwingine, inawezekana pia kuwa, wapiga kura waliopewa kadi (ambao inaelekea kuwa ni wengi sana) kupigia baadhi ya wagombea kwenye kura hizo za maoni, wakawa wameandaa mazingira ya upinzani kushinda. Kwakuwa, ni dhahiri kuwa, hawakuwa wanachama halisi wa CCM (na ndio maana hawakuwa na kadi). Kama hivyo ndivyo, basi CCM inaweza kupata anguko la ajabu.

  Lolote linawezekana katika uchaguzi mkuu. Tusubiri tuone.
   
 16. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #16
  Aug 5, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Wananchi wamepewa nafasi kwenye kura ya maoni tu but uwamuzi wa mwisho ni mkutamo mkuu CC - NEC hapo ndipo watakapochambua pumba zipi na mahindi ni yapi sasa pale ndipo Upinzani utakapo jipamba na ikumbukwe CCM wanabebana mafisadi kivyao, wanamtandao kivyao na wale mbavu mbili nao kivyao sasa mwenye kisu kikali ndio mla nyama hapo JK inabidi awe makini kwenye uchaguzi huo wa Agosti 14 jmosi ijayo. Nauhakika mwaka huu Upinzani utapata viti vingi sana bungeni, maana CCM wenyewe kwa wenyewe wamesha geukana, wamedhulumiana, wanahongana wenyewe kwa wenyewe tena sehemu nyingine unaona wanahongana mchana kweupe. Sasa tayari imesha tia DOA ndani yao, ukiangalia huu uchaguzi baadhi ya maeneo wanachama wametupa kadi zao za uwanachama, wengine wamehama rasmi chama chao.

  Hivyo basi wananchi msifanye makosa kuwarudisha Mafisadi BUNGENI tunataka Mabadiliko na Maendeleo ya kweli tumechoshwa kudanganywa kama watoto.
   
Loading...