Chanzo cha kuwepo kwa jamii ya bushmen nchini Tanzania

Derspiegel

JF-Expert Member
May 30, 2016
285
242
Kwa ajili ya kujifunza asili na mtawanyiko wa jamii za kiafrika nchini, nimeona nilete kwenu members mjadala huu wa chanzo na kwa nini kuna Bushmen ama San nchini Tanzania.
Tanzania ndiyo nchi pekee barani Afrika, ambako makundi (race) makubwa karibu yote ya waafrika, yamekuwa yakiishi nchini kabla ya kuja wakoloni - San/bushmen, Bantu, Nilotes, Semites na Hamites. Kati yao, hakuna wanegro pekee wenye asili ya huko Afrika Magharibi.
Bushmen ndio wa kwanza kabisa kukaa nchini kabla ya makundi mengine kuingia nchini baadaye. Hapa Tanzania, makabila ya Bushmen ni Wasandawe na wahadzabe. Jamii hiyo ya Khoisan ilikuwa imetawala eneo lote la kusini mwa Afrika kuanzia Tanzania hadi Africa Kusini. Wengi wao waliondolewa ama kuuawa na jamii za kibantu zilizokuwa zinasambaa kutokea Afrika Magharibi (tangu 2000 bc).
Hata hivyo katika hali ya kushangaza, nchi zote zinazozunguka Tanzania, walifukuzwa ama kuuawa isipokuwa tu Tanzania na nchi za kusini zikiwemo: S.A, Namibia na Botswana (and may be Angola na Zimbabwe).
Swali, kwa nini hizi jamii zilisalimika onslaught kutoka kwa immigrating racial groups? Kwa nini zilimaintain maeneo yao ya makazi?
 
Kwa ujumla, ni kwamba wasandawe wanaoishi mkoani Dodoma wilaya ya Chemba na wahadzabe waishio mkoani Manyara wilaya ya Mbulu, walifanikiwa kumaintain maeneo yao baada ya kufukuzwa katika maeneo mazuri na jamii mpya, kutokana na maeneo hayo kuwa makame na yasiyo na rutuba kuendesha shughuli za kilimo.
Kwa kuwa jamii hizo hazikuwa na elimu ya kilimo, ziliendelea kujitenga na kuishi maisha ya kuwinda na kuokota matunda, hadi leo. Hata hivyo, wasandawe kwa kiasi fulani waliweza kujifunza namna ya kulima kutoka kwa Wabulunge ambao ni cushitic/Semites.
Je, is it just coincidence, ama kuna sababu nyingine zaidi iliyopelekea kusalimika kwa jamii hizo nchini Tanzania, ilhali kwingine kote, jamii hizo zilimezwa ama kwa kuuawa au kwa kuchanganyikana?
 
Sababu kubwa ya kusalimika kwa jamii hizo ni uduni wa ardhi ya eneo kubwa la kati ya Tanzania, kiasi cha kutopendwa na jamii nyingine hasa za kibantu.
Eneo hilo linapata mvua kidogo wastani wa mm 700 kwa mwaka.
Hivyo kama maeneo hayo, yalionekana mbele za jamii ngeni kuwa hayafai, je si salama kudai kuwa, in east and southern afrika, nchi yetu ndio yenye hali ya hewa mbaya katika maeneo yenye watu wengi katikati mwa nchi yetu kuliko nchi zote za kiafrika
 
Kwa kawaida, kiwango cha mvua cha chini kinachotakiwa kwa mazao yanayostahimili ukame mf. mtama ni mm 760.
Ukiangalia ramani ya Tanzania, utaona kuwa, mikoa yenye kiwango kidogo cha mvua chini ya mm 800 ni Dodoma, Singida, Simiyu, Manyara, Shinyanga, Arusha (not arumeru), Tabora, Mwanza na Kilimanjaro (ukitoa mitelemko ya mlima Kilimanjaro).
Jamii zote zenye asili ya maeneo hayo, zimekuwa zikipata kiwango kidogo cha mavuno na hivyo kujikuta zikikosa ziada (surplus).
Hivi kama mtoto wako, anashinda njaa ama haki vizuri, akili yake itakua vyema. Na ikitokea baba alikuwa hali vizuri na watoto nao wakawa hawapati chakula vyema, wajukuu nao vilevile, halafu na vitukuu. Je hali hiyo ikiendelea kwa vizazi na vizazi haitasababisha udumavu wa akili? Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom