Chanzo cha kuchokana, kununiana katika mahusiano/ndoa na jinsi ya kukabiliana na tatizo hili

Purple dadavua tafadhali

siku zote mtu akizoea kitu hukiona cha kawaida na ladha hupungua..hata ukila chakula kimoja kila siku tena chenye ladha ile lazma utachoka..
Hivyo basi ubunifu ni muhimu sana kwenye mapenzi,usipende kufanya mambo yale yake kila siku..mfn:sio kila siku unaimuita baby badilisha acording to time and context,suprise za hapa na pale,vijizawadi vya 'here and there' lol..,sio kila siku umevaa vitenge tu na dira siku nyingine mini skirt,pedo n.k
 
is there another way?
,mbona wapo wasiochokana na hawakupata mafunzo ya aina yoyote?

unaweza kuichoka nyumba yako?

unajua boss hilo ndo swali la msingi kwakila mtu, huwaga mimi nasema tatizo siyo kupendana bali tatizo lipo kulea penzi. je waweza kuvumilia kweli?
 
Last edited by a moderator:
unajua boss hilo ndo swali la msingi kwakila mtu, huwaga mimi nasema tatizo siyo kupendana bali tatizo lipo kulea penzi. je waweza kuvumilia kweli?

mwenza ni kama nyumba
utaichoka nyumba yako?
mbona mwisho unarudi tu nyumbani?
 
Kuchokana,sijui ila kuna ka msemo kanasema love is timeless!
 
Bora umeanzisha huu mtazamo nami natoe ninachojua, japo sio mtaalamu sana wa haya mambo lakini naweza sema kitu hapo. Tatizo kubwa tunafanana mfumo wetu wa mapenzi na kuiga kwingi.

Kuna kila sababu ya kufuata hali harisi ya wapendanao kwa mfano wapenzi wengi siku hizi wanapenda kuchati kuliko kitu kingine hili ni tatizo, lakini pia kufanya mapenzi kwa mfululizo mpaka watu mnachokana kwa hyo ni lazima kuwe na muda wa kufanya hivyo ili kila mmoja ajipange na kuwa na hamu ya kukutana na mwenzie.

Tukubaliane na ukweli jamani kwamba wazuri ni wengi lakini utakuwa nao wangapi? Kwa hiyo lazima kuwa na kitu kuridhika(satisficity) japo ni ngumu lakini ukiwa na akili yenye maamuzi na sio maamuzi yenye akili utafanikiwa.

Na la mwisho kwa leo ni suala la kuambizana ukweli pale mmoja anapoona au kutoridhika kwa jambo fulani. Kuwa mbali sio tija kwani mnaweza kukutana kwa muda fulani na bado penzi lenu likawa zito.

Mahusiano ya mapenzi ni zaidi ya fikra hivyo yahitaji busara ya hali ya juu sana la sivyo ndio kama hayo.

Jamani mie bado sijaoa ni maono tu hayo waungwana
 
Tatizo watu wengi wanaunganishwa na ngono au tendo la ndoa basi. Ikiwa watu wamekuwa wapenzi au mke na mume kwa sabau nyingi, sex ikiwa just among them; hata mkichokana ki sex (ambayo hutokea sometimes) mnakuwa na sababu za kuendelea kuwa pamoja mpaka hamu inaporudi tena.

Hata kwenye ndoa kwa wale ambao ni marafiki basi ndoa yao hudumu hata kukitokea mawimbi; kwa sababu friendship ni ngumu kuisha.

Sasa unakuta watu wameoana lakini si mke wala mume ana details za maisha ya kila siku ya mke/mumewe kwani kila mtu ana marafiki zake wa kushare nao mambo ya maisha; akikutana na mkewe/mumewe shughuli moja tuuuu hamna story; sexxxxxx, kwa nini msichokane????
Bora umeanzisha huu mtazamo nami natoe ninachojua, japo sio mtaalamu sana wa haya mambo lakini naweza sema kitu hapo. Tatizo kubwa tunafanana mfumo wetu wa mapenzi na kuiga kwingi.
 
Tatizo watu wengi wanaunganishwa na ngono au tendo la ndoa basi. Ikiwa watu wamekuwa wapenzi au mke na mume kwa sabau nyingi, sex ikiwa just among them; hata mkichokana ki sex (ambayo hutokea sometimes) mnakuwa na sababu za kuendelea kuwa pamoja mpaka hamu inaporudi tena.

Hata kwenye ndoa kwa wale ambao ni marafiki basi ndoa yao hudumu hata kukitokea mawimbi; kwa sababu friendship ni ngumu kuisha.

Sasa unakuta watu wameoana lakini si mke wala mume ana details za maisha ya kila siku ya mke/mumewe kwani kila mtu ana marafiki zake wa kushare nao mambo ya maisha; akikutana na mkewe/mumewe shughuli moja tuuuu hamna story; sexxxxxx, kwa nini msichokane????

nimekuongea like lol,mie bora nisiolewe ila kama kuolewa nitaolewa na my best friend.:A S-baby:
 
Back
Top Bottom